nilichojifunza kutokana na uchaguzi wa Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nilichojifunza kutokana na uchaguzi wa Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by NYAMKANG'ILI, Apr 2, 2012.

 1. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Uchaguzi mdogo wa Arumeru umenifundisha kwamba (1) nchi inaelekea kubaya sana kiusalama kwani waheshimiwa wanaotutawala wamepungukiwa na busara isiyo kifani katika historia ya nchi hii. Mambo ya hovyo kabisa yanafanywa na wao hao hao, bila aibu hakuna wa kuwakemea. Wazee wenye heshima zao (?) au waliowahi kuheshimiwa nao kama Jaji Warioba na Balozi Salimu wako kimya (wazee wangu mbona hamsemi, hivi Waziri anaposema mkichagua CDM hatutaleta maendeleo, mtu huyo anatumia Katiba ya nchi gani: Tanzania? Ina maana CDM ni wahaini, au?). Wanaoitwa wazee wa DAR (kama wapo) huu ndio uliokuwa wakati wao wa kutoa busara zao, lakini mmmmmmmmmmmmmmhhhhhh kimya; (2) adhabu kwa CCM ni stahili kwani ni aibu kwa CCM kufanya siasa za uanaharakati (activism) kama vile ni chama cha upinzani. CCM inapaswa kuwaambia wananchi imefanya nini kwa miaka 51 ya utawala wake, siyo itafanya nini kwa miaka 2 na miezi 9 ijayo hadi 2015. CCM hawakufanya, walitukana. Vyema, wameadhibiwa na wananchi; (3) pesa siyo kila kitu; (4) vyombo vya usalama kama polisi, TAKUKURU na TISS ndivyo vinavyohatarisha uhai na usalama wa taifa hili kwa kutofanya kazi kwa haki na kwa kuzingatia sheria. CCM wakilalamikia wapinzani wao, wanasikilizwa. Wapinzani wakilalamikia CCM wanadundwa --------hatutafika salama; na (5) mwisho, nampongeza mshindi NASSARI na NEC, kwa wahisha matokeo. NASSARI nakutakia kila heri katika kutumikia wananchi.
   
 2. M

  MSTU New Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahaaaaaaaaaaaaaaa wasira
   
Loading...