Nilichojifunza kuna haja kubwa ya Wachezaji wetu kuwa na mawakala, mawakala walioidhinishwa na TFF mpaka FIFA

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,186
8,212
Kwenye siku mbili tatu za sakata la Mohamed Hussein kuna vitu vingi binafsi nimejifunza ambavyo baadhi nimepata majibu na baadhi sijapata majibu.

Nilichojifunza kuna haja kubwa ya Wachezaji wetu kuwa na mawakala, mawakala walioidhinishwa na TFF mpaka FIFA, wachezaji wetu wanapaswa kuwa na wawakilishi wa kusimama kwenye masuala muhimu.

Wakala atakuwa na lugha sahihi za kuzungumza, wakala atakuwa na uchambuzi sahihi wa faida na hasara ya dili lolote la Mchezaji, lakini pia Wakala ambaye atatenganisha vitu viwili kati ya kumzungumzia Mchezaji na kuzungumza kama Mteja wake.

Nilichojifunza ni kuwa kuna changamoto kwenye muda wa mkataba (duration of the contract) nimefanya utafiti wangu na nimejiridhisha kuwa Wachezaji na wawakilishi wanapenda mikataba mifupi na sio klabu wakati mwingine.

Kwanini? Nikagundua sababu ni kuwa wanajua wakichukua miaka miwili, kuna uhakika wa kupiga dili lingine ndani ya muda mfupi sana, wengi wakigoma kuongeza mkataba wakati timu zikianza mazungumzo ya mkataba mpya kwa maksudi.

Hii inatokana na nini? Hii inatokana na udhaifu wa kimfumo, huku kwetu tuna signing fee ambayo anapewa Mchezaji moja kwa moja na bakshishi zingine kisha asaini na alipwe Mshahara na wakati mwingine Wakala anapata commission au zawadi kutoka kwa klabu husika.

Kwanini ni Udhaifu? Kimsingi ni kuwa klabu hulipa transfer fee kama wamekununua kutoka klabu nyingine, ila ufikapo klabuni kwenye kurenew contract ni kukubaliana mambo kadhaa tu, huku kwetu watu wanakwepa.

Hiki kitu kwa Tafiti yangu ndogo ndicho kilichowafanya baadhi ya wachezaji kuondoka Azam, hivyo kwa mujibu wa Tafiti zangu nimegundua klabu zetu zinapitia wakati mgumu kwenye usajili kutokana na mambo hayo kadhaa.

Simba anaweza kutaka kuendesha mambo kiweledi ila mfumo wa wengine unaruhusu? Azam anaweza kutaka kwenda kiweledi je wengine wanaruhusu? Huu ni mjadala wa Kitaifa ili kunusuru vurugu kwenye mauzo au mikataba ya wachezaji.
 
Huyu ni agent wa chama hata ukiingia kwenye page yake unajua kuna utofauti na kina mzozo

camara ibrahim.JPG
 
Back
Top Bottom