Nilichogundua kwa watumishi wa umma zama hizi za Rais Magufuli

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Habari Wana wa JF.
Niende madani.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, kumekuwa na mabadiliko katika utumishi wa umma. Kuna mengi ila nizungumzie haya machache.

1. Mosi, Watumishi wa umma wengi wamefungua maduka madogo ya rejareja ili kujikimu kimaisha.

2. Pili, Watumishi wengi wa umma wanajituma na wamekuwa waoga kazini kwa viongozi wa serikali.

3 Tatu, Watumishi wa umma wanaelekeza hasira zao kwa viongozi wao wanaowasimamia vituoni. Mkuu wa ofisi asipokuwa makini atagombana na wenzake wote.

4. Nne, Watumishi wa umma wengi wanaombeana mabaya na hufurahi Sana kusikia fulani katumbuliwa. Mtu husuuzika nafsi yake kisa kasikia kiongozi wa ofisini kwao, jirani au hata kiongozi mkubwa huko juu katumbuliwa.

5. Tano, watumishi wa umma wamejawa na wivu na majungu miongoni mwao na wengi wanaombeana mabaya.

Ni hayo machache tu nimeyagundua kipindi hiki.
 
Namba 2 sikubaliani nayo. Maigizo tu, rushwa, njoo kesho, wiki ijayo kama kawaida.

Nyingine karibu zote, zinaakisi matendo au tabia ya kiongozi wao mkuu, kwa ujumla hana upendo kwao wala hafurahii uwepo wao, hivyo na wao baina yao, hali ni hiyo hiyo.
 
Wangekuwa wanajiamini wangeandamana kudai haki zao
Hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuandamana, sio Watumishi wa Umma, waliojiajiri binafsi wala wananchi wasio na kazi.

Hakuna, hakuna, hakuna, wangekuwepo wenye uthubutu huo Hawa wanafunzi jobless waliomaliza vyuo tangu 2015 wangeshaandamana.

Watanzania wana nidhamu ya uoga tangu enzi.
 
Nyie mnasahau nchi hii tangu imepata uhuru haijawahi kubahatika kupata serikali. Kuna majinamizi tu yanapishana kkila baada ya muda yaliyojipangia
 
Namba 2 sikubaliani nayo. Maigizo tu, rushwa, njoo kesho, wiki ijayo kama kawaida.
Nyingine karibu zote, zinaakisi matendo au tabia ya kiongozi wao mkuu, kwa ujumla hana upendo kwao wala hafurahii uwepo wao, hivyo na wao baina yao, hali ni hiyo hiyo.
Wivu wako umekufanya kipofu. Pole, punguza uone huduma zinavyotolewa kwa uhakika na kwa haraka.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuandamana, sio Watumishi wa Umma, waliojiajiri binafsi wala wananchi wasio na kazi.

Hakuna, hakuna, hakuna, wangekuwepo wenye uthubutu huo Hawa wanafunzi jobless waliomaliza vyuo yangu 2015 wangeshaandamana.

Watanzania wana nidhamu ya uoga tangu enzi.
Uwezo wanao, isipokuwa wamekosa leadership.

Wakati Dr SLAA anaongoza maandamano hapa duniani ulikuwa haujazaliwa ?
 
Iko hivi, pesa inakusaidia kumsomesha mtoto wako shule nzuri na akapata elimu bora, kinyume chake usipokuwa na pesa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mjinga, ukiwa mjinga ni rahisi sana kuwa mtu wa kujipendekeza, ambako huzaa wivu wa kijinga na kukufanya kuwa na roho mbaya, ambayo ndiyo inayokusukuma kufurahia mabaya yanayomkuta mwenzio.

Sehemu ukibaini kuna chuki baina ya wafanyakazi, chunguza, utabaini asilimia kubwa wana elimu ya kuunga unga au hawana elimu kabisa, kwa kifupi wengi wao ni wajinga. Na inaathiri hadi wale wenye akili kugeuka kuwa wajinga.
 
Wangekuwa wanajiamini wangeandamana kudai haki zao

Unadhani kuandamana ndiyo njia pekee ya kudai haki kwa mtumishi wa umma au mfanyakazi yeyote yule! You are wrong! Kuna njia mbadala nyingi sana kwa taarifa yako! Na uzuri tulishaanza kuzitekeleza kitambo tu.

Hivyo hata huyo dikteta uchwara atukandamize kwa namna gani, bado tutatafuta tu njia mbadala za kutokea na mwisho wa siku kujikomboa kiuchumi na kijamii kama makundi mengine.
 
Hakuna mwenye akili hiyo kati yenu, magufuli amewabana kisawasawa, hampumui
 
Matumishi ya umma hayana akili!

Yaani hata wewe form four failure unayetembeza maji mtaani unapata kabisa ujasiri wa kuwaambia watu waliokuzidi kila kitu eti hawana akili!!

Kweli magufuli amewajaza ujinga! Yaani siku hizi wanyonge mnajiona kama mna unafuu wa maisha vile! Kumbe shida zenu ziko pale pale.
 
Back
Top Bottom