gigabyte
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 5,203
- 5,780
Ukipata huo ufafanuzi wa hiyo sheria na kanuni ulete hapa jukwaani tuelimike wote.Naendelea kusema, haya ni mapya kwangu na sikuyajua kabla, sikujua kama mchezaji kuubetua mpira kwa miguu na kisha kuurudisha kwa kipa wake kwa kutumia kichwa ni kosa, lakini mchezaji huyo huyo kuupiga mpira moja kwa moja kwa kipa wake kwa kutumia mguu sio kosa, bila kujali kipa amekamata au hajakamata mpira kwa mikono. Hakika elimu haina mwisho. Hata hivyo nasisitiza sitayapokea moja kwa moja, nitayachunguza kwanza
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app