Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 20,690
- 20,451
Mwamuzi Nassir Salim wa Zanzibar aliyechezesha fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Azam FC na Simba SC hakuwa na ufahamu kuhusu sheria ya mchezaji kurudisha mpira kwa golikipa wake. Mwamuzi huyu alikuwa anajua kwamba mpira wowote uakaorudishwa na mchezaji kwa golikipa wake ni faulo. Alifanya hivyo katika matukio mawili:
1. Wakati golikipa Mathias Kigonya alipomchezea rafu mbaya Pape Sackho, mwamuzi alikuwa hajaliona tukio hili la rafu, ila alikuwa ameliona na kulitolea adhabu tukio lililofanyika kabla Kigonya hajacheza faulo. Alichokiona ni beki wa Azam akirudisha kwa golikipa wake akitumia kichwa. Mwamuzi akatafsiri ni kosa na ndio maana akatoa adhabu ya indirect kick ndani ya box la Azam. Tukio hili waliligundua wachache maana lilikuja kufunikwa na maamuzi mapya baada ya mwamuzi msaidizi na fourth official kumuita kwenye kibendera na kumueleza kuwa kuna faulo mbaya amefanyiwa Sackho, na ndipo ikawa penati, otherwise isingekuwa Sackho amfanyiwa faulo wengi mngeshangazwa na uamuzi wa indirect kick kwa sababu kipa amerudishiwa mpira, wakati sheria inaruhusu kurudishiwa kwa kichwa au kifua
2. Tukio la pili ni pale Onyango alipourudisha mpira nyuma, Henock Inonga akaubetua na kuuinua kisha akaupiga kichwa kumpa Manula. Cha kushangaza mwamuzi akakimbilia aliposimama Inonga na kuamuru ipigwe indirect kick, na hii ndio iliyakuwa dhahiri maana ilipigwa ingawa kila anayejua sheria za soka alishangaa