Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,497
- 6,957
Walisema tembea uone mengi pia uliza ujifunze.
Katika zoezi la CCM kusajili wanachama wake, kuna mengi wananchi wanaojitokeza kuandikishwa hawajui au wamefichwa. Wengi wanaenda na kadi za tume ya uchaguzi wakitaka kuandikisha taarifa zao na kukuta watu wamevaa sare za chama.
Hapo huambiwa usiwe na shaka leta hiki na kile na baada ya hapo usajili huanza na watu wengi wasivyo waelewa hudhani wameandikishwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Nachojiuliza kwa haya maeneo ambapo daftari la kudumu la wapiga kura bado halijapita, si itakuja kuwa ngumu kuwaita watu hawa wasajiliwe?
NB: Watu wanajitokeza kwa wingi na wameitikia wito kwelikweli.