Nilichobaini kwa Wachungaji, Mashekhe, Waganga na Mapadri

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Baada ya uchunguzi na kukusanya maoni na kuwasikiliza wengi nimebaini kuwa:

1. Wapo Wachungaji, Mashekhe, Mapadri ambao wakifungisha ndoa popote pale lazima ndoa hiyo ivunjike baada ya kukaa siku nyingi au siku chache hii haina ubishi, nikajiuliza kwanini ndoa zilizofungwa na fulani nikiziangalia zote zinakuwa na utata mkubwa hazikai, huenda wengi wetu tuna majibu mtusaidie kujua kwanini hili hutokea,

2. Kuna watu wanaumwa sana wanapelekwa kwa Waganga wa kienyeji kutibiwa na marafiki au ndugu mwisho wa siku huyo mtu lazima afe tu, na ni wengi sana mganga huyo anakua ana nini haswa mpaka vifo hivyo vitokee kila anapopelekwa Mgonjwa kwake.

3. Wanaume wengi wanao wachukua wasichana kuwaoa kwa nguvu za waganga huwa wanaachwa kwa aibu sana na hasa Mwanamke akimshtukia huwa ni aibu sana kwake, sasa nauliza kwanini mtu aende kwa mganga ili amsaidie kumpata mke na anasisitiza kuwa anataka apendwe sana, ule upendo wa kawaida haupogi tena au, kwani lazima huyohuyo mwanamke?

Mnafikiri tatizo huwa ni nini haswa.

grrrr.jpg

hjjt.jpg

marr.jpg

mj.jpg
 
Back
Top Bottom