Nilichekwa sana Style yangu ya malezi ila leo hii watu wanatamani kuniiga

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Ni changamoto kubwa katika malezi hasa kwa sisi ambao kuna visenti kidogo huwa tunajikuta tunataka kulea watoto kizungu sana na kuwa na visingizio kama "sitaki mtoto wangu apitie shida nilizopitia" na kujikuta tunalea watoto ndivyo sivyo

1. Mwanzoni mtoto wangu alikuwa anasoma wanatoka saa 11 jioni na shuleni wapo wachache, darasani hawazidi 20. Kwangu kama mzazi nilipoona mtoto wangu navyoenda kumchukua hana marafiki alikua nae moja tu ambae ni jirani na kamzidi darasa, nikajiongeza nikaona hii hali imechochewa na wanafunzi wachache darasani kujumlisha shule kutowapa watoto muda wa kutoka wa kucheza, kujuana, n.k maana pale ilikuwa ni shule ya darasani mtindo moja,

Pesa ya muhula mzima nilikuwa nimeshalipa ila nikamuhamisha shule nyingine ambayo wanawaigi kutoka mchana na darasani wamo kama 60 hivi, shule pia ina ratiba za vipindi wanafunzi kufanya shughuli za kujenga social skills mfano vipindi vya michezo katika ratiba, vipindi vya story telling, vocational skills, n.k Niliona mwanangu akiwa na maendeleo katika social skills alipata marafiki shuleni, zamani alikuwa mkimya sana na mpole ila akaanza kuwa muongeaji na mchangamfu, pia ule mda wanapowahi kutoka mchana unachangia sana kusocialize tofauti na zamani wakitoka saa 11 jioni wanakuwa wamechoka.

Kuhusu ubora wa elimu bado sijaona tofauti katika shule ya zamani na sasa (zote ni za english) nami pia kila siku za shule nahakikisha usiku nakaa nae lisaa kumsaidia masomo maana nilipewa syllabus na vitabu wanavyotymia kuwafundishia na hakuna chochote kinachoweza kunispiga chenga elimu ya shule ya msingi.

2. School bus silipii, sioni umuhimu wake labda mwanafunzi awe mtoto asiezidi miaka mitano au shule ipo mbali sana, Shule anayosoma mwanangu ni mwendo wa dakika 25 tu na wapo wenzake wachache ambao hawalipii school bus wanapitaga njia hii pamoja na wengine wengi wanaosoma shule ya serikali iliyopo karibu na shule yao, School bus niliona ni kumdumaza tu mtoto, anatwanga mguu na wala hakuna tatizo, Wenzake wengi pia wanaopanda school bus ananiambiaga huwa wanatamani sana kutembea ila wazazi hawataki, Kutembea kuna raha yake ya kufanya zoezi, kujimix / kusocialize, n.k.

3. Saizi namruhusu awe anacheza na wenzake nyumbani kwangu au kwa marafiki zake kwa kutoa taarifa mapema tutamkuta nyumba ya rafiki yake yupi, zamani nlikuwa nampiga geti kali na sikuona faida, kwa style hii pia amekuwa msaada mkubwa kwa wenzake wasioruhusiwa kutoka nje maana huu mtaa naoishi wengi hawataki watoto watoke nje, kuna jirani aliniomba mtoto wangu awe anaenda pale kila jumapili maana ni siku ambayo mtoto wake anakuwa hajabanwa na shule , hana homework, n.k ila yeye hataki kabisa mtoto wake kutoka nje, mi nikamkubalia maana yule mtoto ndio alikuwa best wake wa shule ya zamani na hata wazazi wake tunajuana nao na ni mfano wa familia bora yenye maadili kwa hio huwa sina shaka, japo nilimuambia mwanangu akijiona hataki au kachoka kwenda awe free kuniambia, haniogopi huwa hasiti kuniambia chochote

4. Zamani nilimwekea Playstation (game ya tv) na katuni nikijidanganya ndio vitampa kampani kama marafiki, kiukweli nilijidanganya, kwanza hii playstation ikaanza kumpa kama uraibu flani wa kuwa teja, yani aliigeuza game kuwa kama mbadala wa marafiki watu, weekend ikifika ndo kabisa anaweza kushinda hapo kwenye screen hadi mnashangaaa. Kiukweli nikaona hizo kampani zake za katuni na magem yatamuharibu , Ikabidi nimletee mpira awe anacheza cheza nje maana alikuwa anashinda sana ndani, ile game nikaficha nikamdanganya ipo kwa fundi, kidogo kidogo akaanza kuzoea nje, nikamletea na ka mbwa kadogo basi akawa anakapenda sana saizi ni mbwa mkubwa wa ulinzi hapa, furaha yangu ni kumuona akiwa nje, nikaamwamisha shule akaanza kuwa na marafiki kadhaa, nikaacha kulipia schoolbus ili awe ananyoosha vimiguu, n.k basi ndo namimi nafurahi hapo

5. Kuna kipindi flani nilipokuwa naenda kijijini (ni mwendo wa saa moja ) kwenye vikao hivi na kuwajulia hali ndugu zangu, nilikuwa naenda na huyu mwanagu nae, navyoendelea na shughuli zangu alikuwa anachangamana na wenzake, akiwa huko na wenzake aliweza kufundishwa kujipikia ugali maana kule kijijini kujipikia ni kitu cha lazima kukijua, Hii hali inamwandaa mapema hata atakapoanza maisha yake asiwe mpya kwenye kujilisha, Mke wangu hili jambo mwanzoni alichukizwa nalo sana na kuanza kuniambia mtoto wetu hafai kupika hadi awe mkubwa kwa sasa asome tu lakini kwangu nilipingana nae nikamwambia hakuna tatizo mtoto wetu kujua kupika, ipo siku atahitaji hiki alichojifunza, Hapa fundisho kuu ni kwamba mtoto inabidi ajue kujilisha, Isiwe tu kwa watoto wa kike bali hata wa kiume.

6. Michezo - hapa kwanza kabisa nianze na kuelezea kwamba niligharamia ajifunze kuogelea, maana kule kijijini nilihofia kuna siku wataenda huko mtoni akiwa hajui kuogelea, kwa hio nilichukua hii tahadhari haraka, Nawaasa sana wazazi mambo kama kuogelea msiyapuuze, ni kitu kinachoweza kuokoa maisha ya mwanao au yeye kuokoa maisha ya wengine.

Pia kijijini kule alifundishwa hizi sarakasi aliteguka mkono mama yake tuligombana sana hii ishu, ila hakuacha aliendelea na kufanikiwa kuweza kuruka sarakasi za aina nyingi na pia katika shule ya karibu ya serikali aliendeleza kipaji chake hapo kwa kuwa kulikuwa na wanafunzi wengi wanaojua sarakasi, Mwaka jana siku ya wazazi wanapofunga shule nilipata kujisikia vizuri nilipomuona mwanagu akiwa anaonyesha ujuzi wake mbele ya umati wa wanafunzi wenzake na wazazi tuliofika hapo, Ni jambo lililonifurahisha na hata marafiki zangu na wa mke wangu walipoona zile video tulipewa pongezi kidgo, basi hata wife zile hasira zake za mtoto kujifunza sarakasi zikawa zimeisha baada ya kusifiwa na wenzake hahaha.

7. Kuhusu kumlimbikizia kazi house girl mbazo ni wajibu wa mtoto kuzifanya nimezingatia hili suala japo tumekorofishana sana na mke wangu anaetaka housegirl afanye karibu kila kitu mtoto wakae tu, Binafsi nilikataa kabisa huu mpango kumle mtoto mtindo ambao hata mimi wala mke wangu hajalelewa, alianza kutekeleza wajibu kwa mtoto katika kusaidia kazi za nyumbani ni kujua mapema kwamba maisha ni kusaidiana na majukumu, Hata hivyo leo hii au kesho hali yetu inaweza ikawa mbaya watoto wakapata wakati mgumu maana hakutakuwa na house girl, kwa sasa kazi zilizokuwa zinafanywa na house girl anazifanya huyu mwanangu ama wanapeana zamu inapobidi, baadhi ya kazi ni : Kabla hajalala inabidi apasi nguo zake, Inabidi atandike kitanda chake kila siku, asafishe chumba chake, akitoka shuleni afue uniform zake, Asubuhi akiamka anafagia uwanja kwa zamu na house girl , Vyombo anavyolia inabidi aoshe yeye, n.k Mwanzoni alikuwa mgumu ila saizi kazoea, anapozembea namuonya, na inapobidi bakora hazikwepeki.

8. Matumizi ya bakora yanatumika kwa sasa, mwanangu napomfundisha kitu flani au tabia flani aiache, akarudia nikamuonya, akarudia tena nikamkaripia basi kinachofuata kunadawa flani imejaa sana hapa nyumbani kwenye mti wa mpera ni kitendo cha kuichuma tu na kuanza kuitumia, hio dawa si nyingine bali ni viboko, Matumizi ya viboko kwa usahihi ni muhimu sana katika malezi ya watoto, Yapasa atambue kuna madhara ya kutofata kitu sahihi anachofundishwa na wazazi wake na kutokiheshimu, Hii pia inamuandaa hata akiwa mkubwa atakuwa anajua kabisa kwamba asipofata hizi sheria jela inamhusu au atafunzwa na walimwengu, Wazazi msipuuzie viboko hivi, kuna maana kubwa sana vimeruhusiwa kutumika enzi toka enzi na mababu zetu mpaka sasa na hata kwenye biblia na korani, haya malezi ya wazungu mnayoyaiga ni kuikataa asili yenu, Narudi tena tuvitumie viboko kwa njia sahihi sio kila mda unapiga tu.
 
Umefanya sahihi kasoro kumruhusu aende nyumba za watu.

Anaweza kuwa abused huko sexually usijue.

Na mtoto mwenzie au watoto wakubwa wanaokuja nyumba hiyo hata houseboy au housegirl.

Siku hizi kuna shule za serikali English medium, naona kama Better kuliko private English medium.
 
Umefanya sahihi kasoro kumruhusu aende nyumba za watu.

Anaweza kuwa abused huko sexually usijue.

Na mtoto mwenzie au watoto wakubwa wanaokuja nyumba hiyo hata houseboy au housegirl.

Siku hizi kuna shule za serikali English medium. Naona kama Better kuliko private English medium.
 
Umefanya vema, umebakiza kimoja tu

Mruhusu likizo akale matunda pori kijijini.

Kuna fulu,sada na majina mengine kutegemea na mkoa atakaoenda.

Mruhusu akawinde,ndege,senene,panya na vingine kutegemeana na mkoa.

Mruhusu akafundishwe kutega mitego ya kware,njiwa na ngedere na kutafuta uyoga, inategemea namkoa atakao enda.

Ukifanikiwa kumpeleka likizo zote

Huta kuwa na haja ya kumpeleka jkt kwa mujibu wa seria.
 
Umefanya vema, umebakiza kimoja tu

Mruhusu likizo akale matunda pori kijijini.

Kuna fulu,sada na majina mengine kutegemea na mkoa atakaoenda.

Mruhusu akawinde,ndege,senene,panya na vingine kutegemeana na mkoa.

Mruhusu akafundishwe kutega mitego ya kware,njiwa na ngedere na kutafuta uyoga, inategemea namkoa atakao enda.

Ukifanikiwa kumpeleka likizo zote

Huta kuwa na haja ya kumpeleka jkt kwa mujibu wa seria.
Kijijini huko anaenda maana mkoa ninao fanya kazi ndio bibi yake alipo na ni umbali wa kama dakika 45 tu, nilikuwa nampeleka nikienda kwa bibi ila cha kushangaza watu hawakosi cha kusema.

Wengi nilikuwa nawasgangaa wanasema ni mambo yaliyopitwa na wakati mi nikawa nacheka tu kwamba eti atafundishwa vitu vibaya na watoto wa kijijini, atarogwa, atazama mtoni, atapigwa jiwe anapowinda, n.k. Yes ni hatari zinazoweza kutokea lakini thia is life, haya ndio maisha ya Mwafrika.

Kwa ufupi kuna kioindi flani nlikuwa naenda sana huko kwenye vikao flani vya huko nikifika namwacha kwa bibi,

nachokumbuka kwa sana wenzake wa kule huwa wanajipikiaga chakula kwa hio nae ndo akajifunzaga huko kujisongea ugali,
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%
Umefanya vema, umebakiza kimoja tu

Mruhusu likizo akale matunda pori kijijini.

Kuna fulu,sada na majina mengine kutegemea na mkoa atakaoenda.

Mruhusu akawinde,ndege,senene,panya na vingine kutegemeana na mkoa.

Mruhusu akafundishwe kutega mitego ya kware,njiwa na ngedere na kutafuta uyoga, inategemea namkoa atakao enda.

Ukifanikiwa kumpeleka likizo zote

Huta kuwa na haja ya kumpeleka jkt kwa mujibu wa seria.
 
138806748_5630843853607815_5369486947780058212_o.jpg
 
Umefanya vema, umebakiza kimoja tu

Mruhusu likizo akale matunda pori kijijini.

Kuna fulu,sada na majina mengine kutegemea na mkoa atakaoenda.

Mruhusu akawinde,ndege,senene,panya na vingine kutegemeana na mkoa.

Mruhusu akafundishwe kutega mitego ya kware,njiwa na ngedere na kutafuta uyoga, inategemea namkoa atakao enda.

Ukifanikiwa kumpeleka likizo zote

Huta kuwa na haja ya kumpeleka jkt kwa mujibu wa seria.
Sawa mlongo tukupiliki
 
Mleta mada inaonyesha unakaa eneo la low class kwa Walala hoi ila wewe una kanafuu kidogo ni kama wewe ni katajiri fulani katikati ya maskini kwa ulivyojieleza lakini ungekuwa unakaa high class areas hicho ulichoandika chote ni hopeless mfano hakuna mtoto high class anatembea kwa miguu dakika 25 kwenda shule
 
Back
Top Bottom