Nilichapa bakora mtoto wa jirani akafa

Dr Msweden

JF-Expert Member
Nov 3, 2020
2,632
9,440
Baada ya kumaliza diploma yangu ya clinical medicine katika chuo cha mafinga ile nimefika tu mtaani siku ya pili nikakuta watoto wawili wa wapangaji wetu walikuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile umri wao ulikuwa miaka 10.

Nilichukua bakora nikawachapa ,bakora 20 kila mtu wakati natoa adhabu hiyo wazazi wao walikuwepo tena walikuwa wanasema wachape bakora za kutosha waache tabia zao chafu,baada ya kucharaza bakora kila mtoto akaenda kwao.

Kesho asubuhi bahati mbaya mtoto mmoja akuweza kuamka (alifariki) sasa balaa likanijia mimi wale wazazi hawakunielewa wakaenda polisi wakasema mimi ndio nimeua nimempiga mtoto na gongo na mateke kisa ameiba nyama daaaaaah!

Kufupisha huu mkasa kifupi nilikaa mahabusu miezi 11 nashukuru MUNGU nikapewa msamaha kwa kuua bila kukusudia,sasa hivi nikikuta watoto wanafanya Mambo ya ajabu nawaacha kama walivyo sifatishi ule msemo "mtoto wa mwenzio muone Kama mtoto wako".

NB:Aisee tuishi kibepari tuachane na ujamaa, kama mtoto hakuhusu au hata kama unamjua awe ameiba, watoro shuleni nakusihi nk.. nakushauri achana nao jifanye kama hauwaoni kila mzazi afe na mzigo wake.
 
halafu unasikia zezeta moja linasema,kiboko ni ujima.

shida ni kuchapa mtoto wa mtu mwenye maradhi yake,ungewaripotisha ru kwa wazazi wao kisha uendelee na mambo yako.

linapokuja swala la mtu kufa bana hakuna anayeweza kukuelewa.
 
Baada ya kumaliza diploma yangu ya clinical medicine katika chuo cha mafinga ile nimefika tu mtaani siku ya pili nikakuta watoto wawili wa wapangaji wetu walikuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile umri wao ulikuwa miaka 10.
Nilichukua bakora nikawachapa ,bakora 20 kila mtu wakati natoa adhabu hiyo wazazi wao walikuwepo tena walikuwa wanasema wachape bakora za kutosha waache tabia zao chafu,baada ya kucharaza bakora kila mtoto akaenda kwao.
Kesho asubuhi bahati mbaya mtoto mmoja akuweza kuamka (alifariki) sasa balaa likanijia mimi wale wazazi hawakunielewa wakaenda polisi wakasema mimi ndio nimeua nimempiga mtoto na gongo na mateke kisa ameiba nyama daaaaaah!!!!!
Kufupisha huu mkasa kifupi nilikaa mahabusu miezi 11 nashukuru MUNGU nikapewa msamaha kwa kuua bila kukusudia,sasa hivi nikikuta watoto wanafanya Mambo ya ajabu nawaacha kama walivyo sifatishi ule msemo "mtoto wa mwenzio muone Kama mtoto wako".

NB:Aisee tuishi kibepari tuachane na ujamaa,kama mtoto akuhusu au hata Kama unamjua awe ameiba,wanafirana,watoro shuleni nakusihi nk.. nakushauri achana nao jifanye kama hauwaoni kila mzazi afe na mzigo wake
Kudadadeki!
 
Kitendo walichofanya watoto sio kizuri na.kilistahili adhabu

Lakini Shida sio kuchapa....ila unatakiwa uchape kwa kiasi kama umri wa mtoto

Miaka kumi unamchapaje viboko 20??????

Na mzazi kakaa anashangilia!!!!(ingawa watoto wana makosa ndio... ila ku a limit...sio unamaliza ugalj wako wote kwa watoto wa miaka 10)
 
Kosa la kuua bila kukusudia lina adhabu yake. Sasa ukisema ulipewa msamaha kwa kuua bila kukusudia ina walakini kidogo.

Labda useme mahakama ilikukuta huna hatia.

Au useme ulifungwa gerezani na baadae ukapata msamaha wa Rais au bodi ya parole ikakuachia.
 
Pia atuambie ni rais gani alie mpa msamaha jiwe au ssh ama jk ama mwinyi kama siyo Mkapa au Kambarage.
 
Back
Top Bottom