Niliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo - Edwin Mtei

matamko yanazidi kuongezeka kutoka kwa huyu mzee kisa zitto ametangaza kugombea urais.yeye kama mzee hapaswi kuonyesha mapenzi kwa mkwe wake,yeye ni mzee wa chama.

kwa kauli yako unamaanisha amemsifia nani?maana hajamtaja mtu yeyote zaidi ya kutoa mapendekezo
 
.... lakini hilo haliwezi kutokea kama viongozi wake wataanza malumbano na kuwagawa wanachama kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Urais.

......lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama.

Mzee Mtei kwa kauli yake amesema ''Nimemsihi Zitto kuwa kauli yake ya kutaka kuwania urais inabomoa timu yetu kuliko kuijenga na nimemtaka asubiri mpaka chama kitakapoanza mchakato wa wa kumsaka yule atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao''

Mzee Mtei alimalizia kwa kusema..''Unaweza kutangaza nia ya kuwania Urais lakini tujiulize kwanini sasa? Kwanini tusiutumie muda mwingi kujenga timu ya kuiunganisha Chadema badala ya kuisambaratisha?

Source: DIRA ya Mtanzania.
1) Kuna malumbano ya makusudi na yana lengo moja kubwa la kuwagawa wananchama wa CHADEMA.
2) Kuna makundi yaliyoanzishwa kimkakati yenye makusudi ya kuimega CHADEMA
3) Mtu anapotangaza nia yake sasa hajengi bali anabomoa. PERIOD.

Mwisho kwa vile sifa moja wapo ya kiongozi mzuri ni kuwa mstahivu, msikivu na mwepesi kujifunza kutokana na makosa.

So kwa vigezo hivyo hapo naamini CHADEMA wanajua namna ya kushughulika naye. Tusimpe tena publicity maana huko ni sawa na kumpa mlevi wa gongo bange.
 
Hili suala la vijana na wazee limejitokeza sana siku hizi. na linaanza kuwa tatizo. tujue kuwa hakuna vijana bila kuwepo wazee na hakuna wazee bila kuwepo vijana. it is becoming a typical discrimination. we need the minds of our elders just as we need the energy of the youths. both have to work jointly for development of humankind. both have to be listened. maendeleoya dunia hii ni matokeo ya constructive ideas mbalimbali za watu. kila wazo halipaswi kupuuzwa bali kutafakariwa. LET'S THINK OVER AGAIN OF OUR STATUS OF BEING GREAT THINKERS?

Mtu yeyote anayebagua watu kwa misingi ya Umri akiingia madarakani ataanza kuwabagua watu kwa misingi ya udini na ukabila.
 
Mtu yeyote anayebagua watu kwa misingi ya Umri akiingia madarakani ataanza kuwabagua watu kwa misingi ya udini na ukabila.Ubaguzi ni ubaguzi tu ukishaanza ni sawa na kula nyama ya mtu.
 
kuna haja ya kujua demokrasia ya mh.zito ndani ya chama hasa tukizingatia historia ya kigoma tuangalie ,uzalendo wa zito uko wapi kwa kina ,dr kabouru .aliwakilisha jimbo moja miaka ya nyuma alifanya vizuri ,historia haitafutika kwa alichofanya miaka hiyo .
 
Mtu yeyote anayebagua watu kwa misingi ya Umri akiingia madarakani ataanza kuwabagua watu kwa misingi ya udini na ukabila.
Nimeshasema tena humu ndan HILI SWALA LA UBAGUZ WA UMR LIMGHARIMU ZITTO KISIASA
 
luna watu wanatamani sana watanzania wajitenga kwa makundi ya kila style, vyama, dini, sex, umri, kabila. Utawaona tu hata humu JF jinsi wanavyoshabikia
makundi CCM,
makundi CDM,
kutokuelewana kwa vyama vya upinzani
zbar na bara
waislamu na wakristu
wabara na wa pwani
wasomi na wasiosoma
vijana na wazee

yani mnataka hadi tuafarakane na wazee wetu? auu wakwe?

Mshindwe!!
 
Nimeshasema tena humu ndan HILI SWALA LA UBAGUZ WA UMR LIMGHARIMU ZITTO KISIASA

Mkuu Magesi
Ubaguzi ni ubaguzi tu ukishaanza huachi.Nyerere alituambia ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu.
 
Hivi Masumbuko Lamwai, Thomas Ngawaiya na Jesse Makundi nao pia walikuwa ni Watu Kigoma na Waislamu!?
 
Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei amesema anaamini chama chake kitaingia madarakani mwaka 2015 lakini hilo haliwezi kutokea kama viongozi wake wataanza malumbano na kuwagawa wanachama kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Urais.

Amebainisha kuwa CHADEMA kwa sasa hivi ndiyo mkombozi wa wananchi waliochoshwa na utawala wa CCM hivyo ni vema viongozi wake wakatumia muda mwingi kukijenga chama hapa nchini.

Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama.

Mzee Mtei amesema yeye aliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo bali alishirikiana na wenzake ili kiwe kimbilio la wanyonge na kiwasaidie kuboresha maisha yao.

Mzee Mtei kwa kauli yake amesema ''Nimemsihi Zitto kuwa kauli yake ya kutaka kuwania urais inabomoa timu yetu kuliko kuijenga na nimemtaka asubiri mpaka chama kitakapoanza mchakato wa wa kumsaka yule atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao''

Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mzee Mtei amesema pia alishauriana na viongozi wakuu wa Chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwamba wakati huu si wa kuwaza Urais bali wa kukifikisha Chadema vijijini na mijini ambako wananchi wanahitaji ukombozi.

Mzee Mtei alimalizia kwa kusema..''Unaweza kutangaza nia ya kuwania Urais lakini tujiulize kwanini sasa? Kwanini tusiutumie muda mwingi kujenga timu ya kuiunganisha Chadema badala ya kuisambaratisha?

Source: DIRA ya Mtanzania.

Unganisha nukuu Hizi mbili hapa chini utapata utaratibu mzuri kwa muujibu wa Mtei wa kumpata ngombea urais ndani ya CHADEMA.

1 ) "Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama."

2 ) "Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita."

Vijana msikubali, huyu mzee kachanganyikiwa, tena kalewa pombe ya kienyeji (mnazi, chibuku au mbege), huyu si mzima. Hawawezi kukaa na kumteua mgombea uchaguzi wa urais, Mgombea uchaguzi atachaguliwa ndani ya taratibu za chama kwa muujibu wa katiba ya chama na sio kwa matakwa ya Mtei na Familia yake.

Anataka kutuletea zile nadharia za Nyerere, Eti kila uchaguzi wa Rais ni NYERERE na KIVULI. Mtei staafu, tena leo hii, nasikia kichefuchefu kumsikiliza huyu kikongwe.

Vijana msikubali, tena msikubali kabisa, Pambaneni mpaka mwisho. Hivi vyama vya kiukoo ni lazima vibadilishwe na vijana toka vyama vya kiukoo mpaka vyama vya kisiasa, na kazi hiyo ni yenu vijana.

Sasa vyama vingine vyote vya upinzani tutaelekeza nguvu zote kwa kushirikiana na vijana CHADEMA kubadili udikiteta ndani ya chama. Hii ni priority Namba 1.
 
Hapo kwenye wekundu:

Kwani wanaotangaza kwamba watagombea urais kupitia CDM (Kama Zitto) wamesema kwamba watajiteua? Namsikia kila siku Zitto akisema "...kama nitapata ridhaa ya chama changu...." Hii inadhihirisha kwamba atatafuta ridhaa ya chama chake (CDM).
Inawezekana sana watu wengi tu ndani ya CDM wanautaka uraisi. Fikiria kesho Mbowe atoke aseme..kama ntapata ridhaa......, halafu jioni yake Lisu atoke naye aseme ...kama ntapata ridhaa...., na JJ naye keshokutwa atoke na aseme pia kama ntapata ridhaa.... kutaleta picha gani kwa wananchi? Pamoja na kwamba ni haki yao lakini ni ujinga kutumia haki yako kuwavuruga wananchi. Common sense will tell you where and when to say what. But at this point CDM leaders have better priorities than dreaming urais. Inamshangaza kila mwenye akili timamu kuona wakati viongozi wenzake pamoja na wananchi wanatafakari jinsi ya kuvishinda vikwazo na mauaji ya Polisi ili kuidhibiti CDM, mikakati ya Tendwa kukifuta CDM yeye anajitokeza kutumia haki yake kutangaza anavyoutamani urais.
 
maneno mazuri yenye hekima. me nashangaa kwanini zitoo kutangaza nia ccm wengi wanamuunga mkono? je ikitokea chama kimempitisha kuwa mgombea wa cdm watamuunga mkono kama sasa wanavyofanya? au wanataka cdm igawanyike tu kama kilivyo chama chao?
 
Baba Usiogope,mgombea wetu tutamjua wakati ukifika. hiki kijamaa kingine kinatoa taarifa kwa uchaguzi wa 2020 na 2025.:lol:
 
mkuu unakosea sana kusema mzee kachanganyikiwa au amelewa. kama una hoja mpinge kwa hoja sio kumdahalilisha. ye katoa maoni yake jinsi anavyoona. sasa kama hukubaliani naye toa hoja na sio kumtusi.
 
Unganisha nukuu Hizi mbili hapa chini utapata utaratibu mzuri kwa muujibu wa Mtei wa kumpata ngombea urais ndani ya CHADEMA.

1 ) "Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama."

2 ) "Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita."

Vijana msikubali, huyu mzee kachanganyikiwa, tena kalewa pombe ya kienyeji (mnazi, chibuku au mbege), huyu si mzima. Hawawezi kukaa na kumteua mgombea uchaguzi wa urais, Mgombea uchaguzi atachaguliwa ndani ya taratibu za chama kwa muujibu wa katiba ya chama na sio kwa matakwa ya Mtei na Familia yake.

Anataka kutuletea zile nadharia za Nyerere, Eti kila uchaguzi wa Rais ni NYERERE na KIVULI. Mtei staafu, tena leo hii, nasikia kichefuchefu kumsikiliza huyu kikongwe.

Vijana msikubali, tena msikubali kabisa, Pambaneni mpaka mwisho. Hivi vyama vya kiukoo ni lazima vibadilishwe na vijana toka vyama vya kiukoo mpaka vyama vya kisiasa, na kazi hiyo ni yenu vijana.

Sasa vyama vingine vyote vya upinzani tutaelekeza nguvu zote kwa kushirikiana na vijana CHADEMA kubadili udikiteta ndani ya chama. Hii ni priority Namba 1.

Someni huu ushauri wa magamba.Viongozi CDM nadhani mnaelewa ninamaanisha nini.
 
Huyu mzee ameshindwa kueleza ni kanuni au sheria gani imevunjwa kwa kutangaza nia mapema na km anaona si vyema watu kutangaza nia mapema angeshauri uongozi wa cdm kuanda sheria au kanuni za muda sahihi wa kutangaza nia
 
mkuu unakosea sana kusema mzee kachanganyikiwa au amelewa. kama una hoja mpinge kwa hoja sio kumdahalilisha. ye katoa maoni yake jinsi anavyoona. sasa kama hukubaliani naye toa hoja na sio kumtusi.

Mkuu wangu hilo ndilo kundi linalotaka lipewe nafasi ya kugombea Urais.Kundi ambalo limeshakuja na kete ya kusema wazee wa kabla ya Uhuru hawafai kukabidhiwa nchi.Unadhani kundi la namna hiyo litaacha kuwatusi wazee wetu?
 
Tuangalie na upande wa pili wa shilingi...kwa nini kutangaza nia kwa Zitto kuchukuliwe kama njia ya kutaka 'kuisambaratisha' Chadema? Hivi kila kiongozi, mwanachama, shabiki/mpenzi wa Chadema angeichukulia kama kauli ya kawaida labda kumpongeza Zitto kwa kutangaza nia then tukasahau tukisubiri wakati muafaka mchakato utakapoanza..kungekuwa na malumbano yanayotishia 'kusambaratisha' Chadema?
Tatizo tunampa Zitto uzito mkubwa (overrate) hasiostahili...zikipigwa kura za maoni nani awe candidate wa uRais Chadema Zitto hatatokea kama favourite...hizi kura zinazoendelea hapa JF kati ya Dr Slaa na Zitto zinaonyesha jinsi Dr alivyomuacha kwa mbali. Kwa nini wanaChadema tuchachawe na kudhani Zitto anatishia kusambaratika kwa Chadema?

Nikweli,lakini si muda muafaka kutangaza nia ya kugombea urais sasa,let us wait,time'll tell us who's who.CHADEMA kwa ukombozi wa kweli wa MTZ.
 
Back
Top Bottom