Niliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo - Edwin Mtei

Hapa mtasababisha hata sisi tusio washabiki tuanze kuogopa siasa ya Tanzania. Katika hali ya kawaida Zitto amechemka kutangaza nia mapema tena wakati M4C yao ikiwa hot yeye kaja na ajenda ya Urais kupunguza makali ya M4C. For real kumwunga mkono huyu jamaa ni kudhoofisha upinzani.
Sasa utabiri wa Wasira utatimia hata kabla ya 2014 kama CDM hawatakuwa makini and its so bad to see this.

Mkuu nikuhakikishie ondoa hofu.Mbinu ya Wassira haitafanikiwa.Na ndiyo maana waasisi wa chama wameingia ulingoni kuhakikisha hakuna ujinga wa kuvuruga chama.
 
Kwa nini mtu atangaze nia kipindi hiki CDM ikiwa inakubalika sana na si kipindi kingine? Hii ni kuonesha kuwa uwezekano wa kuingia IKULU ni mkubwa hivyo kwa Tamaa ya madaraka au kutumiwa mtu anadivert fikra za watu wawaze urais badala ya elimu ya uraia.
 
TRUTH REMAIN TRUTH DO NOT HIDE IT; MZEE MTEI AMENENA KWELI, Nimuhimu watanzania tukakubali kuwa kwa sasa CDM kinahitaji kuenezwa kijijini na sehemu nyingine ambako hakijafahamika,lkn hivi kweli zito anatimiza wajibu wake ndani ya chama?kwa yeye kama naibu katibu mkuu alishindwa hata kuandaa JIMBO MOJA KIGOMA AMBALO CDM WANGEONGEZA HUKO KG,ni muhimu tukakubali hakutimiza wajibu wake na hata sasa yeye anahangaika kujitangaza binafisi KULIKO CHAMA.sina shaka na uwezo wake lkn aungane na wenzake kujenga chama halafu muda ukifika aombe kuteuliwa akipata basi apeperushe bendera MWISHO KUNA HAJA TUKAFANYA MENGINE YA MUHIMU KWANI HATA KATIBA KWA SS HAIMULUHUSU By MASIKINI MASIKINI
 
Kwa nini mtu atangaze nia kipindi hiki CDM ikiwa inakubalika sana na si kipindi kingine? Hii ni kuonesha kuwa uwezekano wa kuingia IKULU ni mkubwa hivyo kwa Tamaa ya madaraka au kutumiwa mtu anadivert fikra za watu wawaze urais badala ya elimu ya uraia.
hapo umenena
Ukijaribu kufikiri sana unapata majibu mengi, wanachotaka ni kuacha kujenga chama ili tuanze na vurumai nani anafaa nani hafai kabla hatujashtuka 2015 on the door hakuna shina wala tawi. Ni kuuliza wale wanaoutaka Uraisi leo je ni nini wamejifunza kushindwa 2005, 2010?? Je hatukushindwa pamoja na wizi na hujuma ni pamoja na kutokuwa na mashina nchi nzima, wanachama nchi nzima?? mtandao mzuri wa chama nchi nzima?? bila kufix hili tatizo leo kweli tutashinda?? Kasi ya ushindi inawafanya CCM na mamluki waanze kutuvuruga na tumesema haiwezekani.

Ushindi wa chadema ni mkubwa sana na kishindo chake kimemwamsha adui na wapambe wake wote. Tutachambuana mpaka tupate mchele bila chenga.
 
Mkuu Molemo palilieni demokrasia ndani ya Chama. Watu wajitokeze mapema watangaze nia zao tuwajue kwa matendo yao.

Democratia gani unaongelea??? Makubaliano ya wengi ndani ya chama ni kujenga chama kwa kipindi hiki na sio kutangaza nia. Mbona ahuitaji hekima kubwa sana kulielewa hili....

CDM hatuna utaratibu wa kutangaza nia kabla ya chama kufungua mlango, tangu Mbowe hata kipindi cha dr slaa. ukifanya hivyo automatically unabadili mazungumzo na mtizamo kutoka kwenye siasa za kujenga chama na kuhamia kwenye uchaguzi.

Lets do our things in a matured manner.
 
Zittooooo kama hajatumwa nini sasa? 2015 atakuwa bado hana sifa ya kugombea kwa sababu ya kigezo cha umri, sasa basi ni bora angefanya kampeni ya kifungu husika cha katiba kibadilishwe kwanza kuliko yeye kung'ang'ania kutangaza kugombea urais, je kama katiba haitabadilishwaje? Zitto umekuja kuwaje?
 
Tuangalie na upande wa pili wa shilingi...kwa nini kutangaza nia kwa Zitto kuchukuliwe kama njia ya kutaka 'kuisambaratisha' Chadema? Hivi kila kiongozi, mwanachama, shabiki/mpenzi wa Chadema angeichukulia kama kauli ya kawaida labda kumpongeza Zitto kwa kutangaza nia then tukasahau tukisubiri wakati muafaka mchakato utakapoanza..kungekuwa na malumbano yanayotishia 'kusambaratisha' Chadema?
Tatizo tunampa Zitto uzito mkubwa (overrate) hasiostahili...zikipigwa kura za maoni nani awe candidate wa uRais Chadema Zitto hatatokea kama favourite...hizi kura zinazoendelea hapa JF kati ya Dr Slaa na Zitto zinaonyesha jinsi Dr alivyomuacha kwa mbali. Kwa nini wanaChadema tuchachawe na kudhani Zitto anatishia kusambaratika kwa Chadema?

Katika hali ya kawaida mtu anaweza kutangaza nia halafu akakaa akatulia tu bila kufanya mishemishe za kutimiza malengo yake?
Ukiwa mkweli utaona vurumai zinazotokea miongoni mwa wanaChadema wale wanaomuungamkono kwa uapnde mmoja na wale wasiomuunga mkono kwa upande wa pili. Hoja ya msingi hapa ni kuhakikisha mshikamano wa wanachama ili chama kitakapotangaza kwamba ni muda muafaka kwa wasaka uraisi kutangaza basi aanze kampeni za kutafuta hiyo nafasi.

Natambua kwamba wapo wengi tu wanaowish kugombea uraisi lakini hawajajitokeza hadharani kwa kutambua madhara yatakayokipata chama kwa kufanya hivyo. Kinachotokea ccm ilipaswa kuwa somo tosha kwetu sisi ili tuendelee kulinda mshikamano na umoja uliopo.

Kusema tumuache aendelee kutangaza kila mara akikumbushia nia yake ya kutaka uraisi, tena huku akitambua hadi sasa bado katiba inambana kwa kipengele cha umri hiyo tu inatosha kukufikirisha kwanini anakuwa na matamanio hayo kwamba lazima iwe 2015 huku akifahamu hicho kikwazo, hapa ndipo wasiwasi unapoanzia, huenda ana agenda ya siri na ni muhimu kumueleza kwamba anachokifanya si sahihi hata kidogo, na unafahamu kwamba ana wafuasi wengi tu ndani ya Chadema.
 
Umtumwa, umeziba milango ya kuelewa alichokisema mzee Mtei. Nimshakugundua uko upande gani?
 
Hii ndio laha ya kuwa na waasisi kama MTEI,sasa nimejua pumba ni ipi na mchele ni upi! kwa kauli hii ya muasisi wa chama yeyote atakae kwenda kinyume na kauli ya busara kama hii tutamwita ni msariti,sasa dawa ya msariti wadau nadhani mnaijua! ni kumfukuza tu! m4c na hasa vijana ni lazima tuungane,na wakati muafaka ni sasa! peoplessssssss........
 
Mkuu Molemo palilieni demokrasia ndani ya Chama. Watu wajitokeze mapema watangaze nia zao tuwajue kwa matendo yao.

Kutangaza nia ya kuwania uraisi huku ukitambua huna sifa ya umri kwa mujibu wa katiba ya sasa na wakati ambapo si kipaumbele cha chama ni sawa na kutangaza nia ya kukibomoa.

Demokrasia si kufanya kitu chochote unachojisikia wakati wowote pasipo kuzingatia maslahi ya chama. Tukikubali kufanya demokrasia ya aina hiyo tutakuwa tunaendekeza ubinafsi badala ya maslahi mapana ya umma.
 
Katika hali ya kawaida mtu anaweza kutangaza nia halafu akakaa akatulia tu bila kufanya mishemishe za kutimiza malengo yake?
Ukiwa mkweli utaona vurumai zinazotokea miongoni mwa wanaChadema wale wanaomuungamkono kwa uapnde mmoja na wale wasiomuunga mkono kwa upande wa pili. Hoja ya msingi hapa ni kuhakikisha mshikamano wa wanachama ili chama kitakapotangaza kwamba ni muda muafaka kwa wasaka uraisi kutangaza basi aanze kampeni za kutafuta hiyo nafasi.

Natambua kwamba wapo wengi tu wanaowish kugombea uraisi lakini hawajajitokeza hadharani kwa kutambua madhara yatakayokipata chama kwa kufanya hivyo. Kinachotokea ccm ilipaswa kuwa somo tosha kwetu sisi ili tuendelee kulinda mshikamano na umoja uliopo.

Kusema tumuache aendelee kutangaza kila mara akikumbushia nia yake ya kutaka uraisi, tena huku akitambua hadi sasa bado katiba inambana kwa kipengele cha umri hiyo tu inatosha kukufikirisha kwanini anakuwa na matamanio hayo kwamba lazima iwe 2015 huku akifahamu hicho kikwazo, hapa ndipo wasiwasi unapoanzia, huenda ana agenda ya siri na ni muhimu kumueleza kwamba anachokifanya si sahihi hata kidogo, na unafahamu kwamba ana wafuasi wengi tu ndani ya Chadema.

Mkuu bandiko lako ni somo tosha.Thankyou!
 
Hii ndio laha ya kuwa na waasisi kama MTEI,sasa nimejua pumba ni ipi na mchele ni upi! kwa kauli hii ya muasisi wa chama yeyote atakae kwenda kinyume na kauli ya busara kama hii tutamwita ni msariti,sasa dawa ya msariti wadau nadhani mnaijua! ni kumfukuza tu! m4c na hasa vijana ni lazima tuungane,na wakati muafaka ni sasa! peoplessssssss........

You are right.Atakayempinga tena mzee Mtei ni mchawi mkubwa wa CDM.
 
Nampongeza sna mzee wetu kwa maneno mazuri yaliyojaa busara.Hata CCM wenyewe
mpaka sasa hakuna hata mmoja amethubutu kusema hadharani kuwa anautaka urais 2015
japokuwa matendo yao yanaonekana wazi.Huyu dogo akicheza anafutika katika siasa.
Kuna siku nuilipiga nae picha lakini natamani hata kuichana.
 
Tuangalie na upande wa pili wa shilingi...kwa nini kutangaza nia kwa Zitto kuchukuliwe kama njia ya kutaka 'kuisambaratisha' Chadema? Hivi kila kiongozi, mwanachama, shabiki/mpenzi wa Chadema angeichukulia kama kauli ya kawaida labda kumpongeza Zitto kwa kutangaza nia then tukasahau tukisubiri wakati muafaka mchakato utakapoanza..kungekuwa na malumbano yanayotishia 'kusambaratisha' Chadema?
Tatizo tunampa Zitto uzito mkubwa (overrate) hasiostahili...zikipigwa kura za maoni nani awe candidate wa uRais Chadema Zitto hatatokea kama favourite...hizi kura zinazoendelea hapa JF kati ya Dr Slaa na Zitto zinaonyesha jinsi Dr alivyomuacha kwa mbali. Kwa nini wanaChadema tuchachawe na kudhani Zitto anatishia kusambaratika kwa Chadema?

Hivyo ndo inatakiwa kuwa, CHADEMA ni chama kikubwa kwa sasa, kuna kila dalili za watu wengi kutaka urais kupitia chadema, ubunge kupitia chadema na udiwani kupitia chadema! Nina uhakika hakuna jimbo, kata ambayo haitakuwa na mgombea 2015, hakuna kijiji wala,kitongoji ambacho hakitakuwa na mgombea 2014 serikali za mitaa! Mimi nafikiri ni wakati muafaka sasa chama kikajiandaa kupokea changamoto za chama kukua! Tuamini busara za wanachama na viongozi kufanya maamuzi yenye busara! Zitto amesema wazi na sisi tumesikia kwamba chama kikimpa ridhaa atagombea, akikosa ridhaa atamnadi yule aliyepata ridhaa ya chama, na kamwe amesema hatoingia kwenye histtoria ya kurudisha nyuma haraki za Upinzani kuchukua dola! Let us give him the benefit of the doubt! Na tuachane na huu ungonjwa wa Zittophobia!
 
Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei amesema anaamini chama chake kitaingia madarakani mwaka 2015 lakini hilo haliwezi kutokea kama viongozi wake wataanza malumbano na kuwagawa wanachama kwa lengo la kutafuta uungwaji mkono wa Urais.

Amebainisha kuwa CHADEMA kwa sasa hivi ndiyo mkombozi wa wananchi waliochoshwa na utawala wa CCM hivyo ni vema viongozi wake wakatumia muda mwingi kukijenga chama hapa nchini.

Mzee Mtei amesema CHADEMA kina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wa Urais lakini kama viongozi wake wataanza kutoa kauli za kuwania vyeo hivyo kuna kila dalili ya kuzaliwa makundi yatakayokimega chama.

Mzee Mtei amesema yeye aliasisi CHADEMA si kwa lengo la kutafuta vyeo bali alishirikiana na wenzake ili kiwe kimbilio la wanyonge na kiwasaidie kuboresha maisha yao.

Mzee Mtei kwa kauli yake amesema ''Nimemsihi Zitto kuwa kauli yake ya kutaka kuwania urais inabomoa timu yetu kuliko kuijenga na nimemtaka asubiri mpaka chama kitakapoanza mchakato wa wa kumsaka yule atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao''

Mzee Mtei amesema kuwa Dk Slaa aliteuliwa na vikao vya chama kugombea urais 2010 na ndiyo maana umoja na mshikamano ndani ya chama ulikuwa mkubwa kiasi cha kukifanya Chadema kipate idadi kubwa ya wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mzee Mtei amesema pia alishauriana na viongozi wakuu wa Chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa kwamba wakati huu si wa kuwaza Urais bali wa kukifikisha Chadema vijijini na mijini ambako wananchi wanahitaji ukombozi.

Mzee Mtei alimalizia kwa kusema..''Unaweza kutangaza nia ya kuwania Urais lakini tujiulize kwanini sasa? Kwanini tusiutumie muda mwingi kujenga timu ya kuiunganisha Chadema badala ya kuisambaratisha?

Source: DIRA ya Mtanzania.

Zitto komaa ,mtei kitu gani,nia unayo na uwezo unao

Mtu kugombea urais kupitia chama chake.Tena kwa ridhaa ya chama Tatizo liko wapi.Kwa sababu Yeye sio Baba mkwe wake Au kwa sababu Zitto ni muislam nadhani Kama sio sababu hizo mbili basi moja lazima imuhusu.Mwanzilishi ndio anayeweza kukiua Kama anavyofanya sasa Manake kwa Udini huyu yumo sana.
 
Thamani ya kitu huwezi kujua mpaka ukipoteze.Ichane halafu 2015 uone utakavyojutia.
Nampongeza sna mzee wetu kwa maneno mazuri yaliyojaa busara.Hata CCM wenyewe
mpaka sasa hakuna hata mmoja amethubutu kusema hadharani kuwa anautaka urais 2015
japokuwa matendo yao yanaonekana wazi.Huyu dogo akicheza anafutika katika siasa.
Kuna siku nuilipiga nae picha lakini natamani hata kuichana.
 
Hivi CDM ilianzishwa na Mtei peke yake nadhani heading ilitakiwa isomeke waliasisi siyo niliasisi au tuliasisi.
 
Back
Top Bottom