Niliahirisha uamuzi wangu wa kumtongoza baada ya kuniuliza nafanya kazi wapi

Balqior

JF-Expert Member
Jun 8, 2021
1,678
5,582
Kuna mdada mmoja nilikutana naye kwenye mgahawa wa mama ntilie akiwa kama mpishi na muhudumu, alikuwa mrembo nikaona huyu akinikubali na tukiendana, atanifaa for long term relationship even marriage if possible..na nlivomu-approach huyu dada sikujitutumua na kujifanya nina pesa.

Nikaanza kujifaragua kwake nkamshobokeea, nikaflirt naye, though sikumwambia nia yangu on the spot, na sikumwomba namba, ingawa yeye alijua namaanisha nini, which brings me to third paragraph.

Siku hiyo nimeenda kwenye mgahawa wake kula, mdada ananiuliza nafanya wapi kazi wakati sijawahi kukopa wala kumuomba chakula kwake, taa nyekundu Iliwaka kichwani kwangu, nikasema mapema hivi anauliza nafanya wapi kazi (kiuhalisia mimi bodaboda), Kaniona danga au? Kwanini asiniulize wazazi wangu, ukoo wangu, ndugu zangu, hobbies zangu, straight to the point akaniuliza nafanyia wapi kazi, nikamjibu kuwa nitamwambia siku nyingine.

Ghafla nilikata mazoea na huyo dada..Na mgahawani kwake sikwenda tena na plan ya mimi kumtongoza niliihairisha maana nliona Hana hisia na mimi, baadae atakuja nichuna pesa halafu asepe, sababu mapema yote anauliza nafanyia wapi kazi Ili aone atanipiga mizinga ya tshs ngapi.
 
Amekuuliza swali la msingi sana na nia yake wala sio mbaya kama unavyofikiria. Kama ameona unaonyesha nia kwake kwa nini asiulize habari zako ili aweze kupata information kamili kwa ajili ya kufanya maamuzi.

Kwa ufupi wewe ndio umejistukia na ungemweleza tu kazi yako ili afanye maamuzi sahihi kwa wakati sahihi

Wakati niko kijana "barobaro" niliwahi kukutana na dada mmoja mzuri sana mwanafunzi wa chuo kikuu, tulizoeana nikamtongoza nae akaniuliza unafanya kazi gani (nilikuwa benki) nikamdanganya mimi ni fundi majenerata (nilijishusha nimuone).

Yule dada alinikubali ingawa sikumuoa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Sometimes ukiwa mkweli au ukijishusha unaweza kupata mtu sahihi
 
Kuna mdada mmoja nilikutana naye kwenye mgahawa Wa mama ntilie akiwa kama mpishi na muhudumu, alikua mrembo nikaona huyu akinikubali Na tukiendana, atanifaa for long term relationship even marriage if possible..na nlivomu-approach huyu dada sikujitutumua na kujifanya nina pesa.

Nikaanza kujifaragua kwake nkamshobokeea, nikaflirt naye, though sikumwambia nia yangu on the spot, na sikumwomba namba, ingawa yeye alijua Namaanisha nn, which brings me to third paragraph.

Siku iyo nimeenda kwenye mgahawa wake kula, mdada ananiuliza nafanya wapi kazi wakati sijawahi kukopa wala kumuomba chakula kwake, taa nyekundu Iliwaka kichwani kwangu, nikasema mapema hivi anauliza nafanya wapi kazi (kiuhalisia mm bodaboda), Kaniona danga au? Kwann asiniulize wazazi wangu, ukoo wangu, ndugu zangu, hobbies zangu, straight to the point akaniuliza nafanyia wapi kazi, nikamjibu kuwa ntamwambia siku nyingine.

Ghafla nilikata mazoea na huyo dada..Na mgahawani kwake sikwenda tena na plan ya mm kumtongoza niliihairisha maana nliona Hana hisia na mm, baadae atakuja nichuna pesa hlf asepe, sababu mapema yote anauliza nafanyia wapi kazi Ili aone atanipiga mizinga ya tshs ngapi.
Amekuuliza swali la msingi sana na nia yake wala sio mbaya kama unavyofikiria. Kama ameona unaonyesha nia kwake kwa nini asiulize habari zako ili aweze kupata information kamili kwa ajili ya kufanya maamuzi.

Kwa ufupi wewe ndio umejistukia na ungemweleza tu kazi yako ili afanye maamuzi sahihi kwa wakati sahihi

Wakati niko kijana "barobaro" niliwahi kukutana na dada mmoja mzuri sana mwanafunzi wa chuo kikuu, tulizoeana nikamtongoza nae akaniuliza unafanya kazi gani (nilikuwa benki) nikamdanganya mimi ni fundi majenerata (nilijishusha nimuone).

Yule dada alinikubali ingawa sikumuoa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Sometimes ukiwa mkweli au ukijishusha unaweza kupata mtu sahihi
Hapo mafundi utuombe radhi maana pesa yetu inatoka at once na sio kusubiri mwisho wa mwezi mzee,tafadhali sana
 
Wakati mwingine mtu hujiwekea mipaka ili kama hupendi kitu hicho bas taa ya hatar huwaka ili kuashiria kimbia hapo kuna jambo baya!

Kwa upande wangu hali kama hiyo iliwahi nitokea katika mahusiano ya kutafuta mrembo wa kuishi nae ili kuyajenga maisha ya familia.

Ilikuwa hivi," Mimi nikiwa mfanyakazi kama fundi na ninakutana na vijana wengi wanaopita katika ufundi, nikiwa na maisha mazuri ya pekee yangu wakati nimepanga nyumba kitaa na nina mshahara mzuri tu wa keendesha maisha yangu.

Katika mizunguko yangu na rafiki yangu ( R.I.P) na baiskel zetu za mountain, jioni mizunguko hapa na pale baada ya kazi ni lazima tukanywe uji wa ulezi shilabela(code zimezingatiwa)!

Kuna mzee wa makamu alikuwa ni rafiki yetu wa makamo tulikuwa tunakutana mara kwa mara hapo senta shilabela kwenye uji pia mahitaji ya home kidogo, hivyo alitufahamu vizuri na kuna wakati alikuja ofisini pia nyumbani kwa ushauri na mambo mengine ya kifamilia kwa kusaidiana.

Pia ikatokea nikawa na mazoea ya karibu sana na familia yake kama ni mmoja pia wa familia yake.
Kutoka na hayo yote ikapelekea mama (mke wake) kuwa aniuliza kuhusu mahusiano ya kuwa na mwenza hii ni kwa sababu aliniona mimi si mwingi wa totoz kuliko rafiki yangu, na ni kwel rafiki yangu alikuwa ni mwingi hasa kwani ilibaki kidogo tu apite na binti yake wa kwanza alikuwa ndio sitafel linanukia juu ya mti ila hulioni! Kikwazo ikawa mimi sote tunaishi nyumba moja na binti aliniogopa sana kupitia baba yake.

Hivyo basi kwa hayo mazingira wote mtu na mke wake wakawa wananihusia sana kuwa na mke, na kama niko tayari wangenitafutia binti mzur mcha Mungu na angenifaa, pia ni mchapa kazi kweli!

Kutoka na kile kilichomfanya jamaa akakimbia ni mazingira ya nafsi yako yanavyo kutuma kuona hapa sio, ndivyo ilivyokuwa kwangu kuhusu huyu binti ambaye nilitafutiwa.

Huyu binti alikuwa ni mzuri na ni wife material kabisa alikuwa ni mwajiriwa ktk kampuni ya madini hapo kijijini enzi hizo na nilimpenda nilipokutana naye kwa mara ya kwanza alikuja kunipokea stand ya basi, tulikuwa na mawasiliano na yeye ila hakuwani niona wala kwa picha mimi pia.

Kutokana na kumwomba Mungu anijalie nipate mke mwema, nikiwa katika safari kwenda kumwona huyo mrembo ili tuwe na maamuzi kuna kitu kilikuja katika nafsi yangu "kikaniambia kama huyo bint ni kabila moja na huyo mzee acha naye utakuwa ni kama kitega uchumi yake" hiki kitu kilinikaa kichwani na nikatembea nacho.

Wakati ulipofika nikaonana na binti alifurahi kwa kuniona na tukaelekea kwa yule mzee kwa mazungumzo ya awali kwa heshima.

Tukiwa njian Kweli Mungu hujidhilisha pindi umwombapo, tulikutana na mtoto wa yule mzee kabla ya kufika kwao yule kijana aliniamkia shikamoo kaka kwa heshima ya mimi na wazazi wake pia yule dada wakaongea kwa kilugha!!!? Hapo hapo ile taa ya hatari ikawaka na moyo wangu ukapoa na nikaendelea na safari kutimiza wajibu tu.

Siku ya siku nilimwambia ukweli akanielewa akaendelea na maisha yake.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom