Siasa Basi
JF-Expert Member
- Jul 10, 2016
- 1,493
- 4,276
Jamani dunia hii ina mambo sana, wanadamu wamekuwa kama wanyama. Twende kwenye mada.
Tulizaliwa katika familia ya kikristo, mama na baba yangu wote walikuwa wakatoliki. Kuna kipindi mama yangu aliugua sana, tukampeleka hospitali lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya. Siku moja tumekaa tukaona tangazo kwenye TV channel ten, leteni wagonjwa waombewe, vilema, viziwa, vipofu, wagonjwa ukimwi, kisukari n.k
Tukaona na sisi tuna mgonjwa nyumbani, kwa hiyo lile tangazo na mahubiri yalitusawishi kwenda kumuona huyo Nabii. Siku ya jumapili ilipofika fika tulikwenda wote kama familia kumpeleka mama kuombewa.
Tulikuta kanisa limejaa sana, watu kutoka sehemu mbalimbali walikuwepo. Waibaji wakubwa siku hiyo walikiwepo. Nabii huyu ni maarufu sana hapa Dar es salaam, na mpaka sasa yupo anaendelea na huduma. Baada kufika tulifurahi ibada sana, mama aliombewa akaanguka chini akaanza kulia na kutamka mambo ya ajabu.
Nabii akasema mngemchelewesha angekufa lakini Leo ndio muujiza wake umefika. Tulipomaliza maombi tukarudi nyumbani. Siku zilivyokwenda hali ya mama iliendelea kuimarika vizuri. Tukawa tunaendelea kwenda kanisani kila Juma Pili. Mwisho tukazoe na mama akaamia kabisa humo kanisani.
Nina mdogo wangu wa kike alikuwa anasoma kidato cha tatu, alikuwa Mrembo kweli kweli si mchezo bwana; maana hata mi kakaake ni handsome kweli napangawisha sana mademu huku kitaani. Mdogo wangu huyu mwanzo walikuwa wanaenda na mama kwa nabii kwenye maombi ya Jtano.
Chakushangaza huyu mdogo wangu alizidi sana kwenda kanisa hilo kupita wote. Ilifika wakati eti nabii anapiga simu nyumbani kupitia kwa mdogo wangu kumsalimia mama, wakati mama nae ana simu yake. Na wakati mdogo wangu akiongea na huyu nabii anakuwa na furaha kuliko kawaida.
Mtu mzima nikashitukia dili, nikamhuliza mdogo wangu kwani we na nabii mlizoanaje kwa kiasi hicho. Ananijibu unajua kaka nabii ametabiria Sijui nini na nini…....... Dah! Nikashangaa nikamdokeza mama, nikamwambia huyu binti yako na nabii kuna kitu kinaendelea hapa.
Mama aliposikia hivyo alinirukia na matusi juu, we mtoto umeisha hasi, unampa nafasi shetani kumsikizia mtumishia wa Mungu uongo na ujinga. Tena ukome nisije kukusikia tena, kwani utaki mdogo wako akaombewa na nabii ili afanye vizuri kwenye masomo yake? Aisee kwa majibu ya mama nikabidi nitulie tu nitazame movie.
Mdogo wangu alizidi sana kuongea na nabii, siku asipoenda shule lazima akashindie kwa nabii, nikimuuliza anasema nilikwenda kumsaidia mke wa nabii shughuli za nyumbani. Wakati huo baba ni mtu wa kusafiri sana yeye ajui kinachoendelea kati ya nabii na binti yake. Mama alikuwa akimsifia sana binti yake kwamba wokovu umekolea na neema imemshukia. Maisha yaliendelea kama kawa.
Siku moja nimetulia zangu nyumbani siku ya Jmosi namuona mdogo wangu anatapika na kulala sana, nikashitukia dili nikamwambia mama huyu mtoto wako naona kama ana mimba vile. Kama kawaida ya mama akaniwakia umempa wew hiyo mimba ni mchafuko wa tumbo na maralia yanamsumbua. Nikatulia. Mara akaanza utoro shule kisa anaumwa. Siku mama ananiita kwa aibu kubwa, kweli ulisema mdogo wako ana mimba tena mimba hiyo kampa nabii.
Kizaazaa kikaanza, Mimi nikaonekana mshindi kwa Yale niliyoyasema, wakati nabwatuka kwa hasira mama kimya, anasema Sijui nitamweleza nini baba yako. Ikabidi tumsubiri baba aje atoe maamuzi. Baba alipokuja, akapata habari siku hiyo kidogo watu walale nje . kesho yake bila kuchelewa tukaenda kwa Nabii. Kufika ofisini kwa nabii mhudumu akatupokea, tukamuuliza nabii yumo akasema yumo maana alijua ni wagonjwa.
Tukaingia ndani nabii kutoana akataka kukimbia ofisi yake. Baba yangu mstaarabu alichomwambia nabii wewe ni mtumishi wa Mungu ninakuheshim sana lakini kwa kitendo ulichomfanyia binti yangu lazima nikumalize. Nabii akaomba msamaha pale, mwisho baba akamwambia atunze huo ujazito na akijifungua amlee huyo mtoto na amusomeshe mdogo wangu mpaka amalize shule.
Nabii akakubali lakini akaomba tuitunze siri isije kufika kwa waumini wake, na sisi tukasema ni aibu kutangaza kitu kama hiki kwa nabii mkubwa kama wewe kubaka vibinti kidogo. kwa hiyo akamsomesha na kumlea mtoto wake. Kwa sasa huyu mdogo wangu anamaliza chuo mwaka huu.
Lakini tokea kipindi hicho nilikosa hamu na kanisa na kuwaamini hawa manabii. Nimeanza kwenda kanisani hivi karibuni baada ya kuamia kwangu na kuoa .
NB: Onyo usimwamini binadamu kwa asilimia 100℅. Mzazi kuwa makini na hawa manabii.