Niliacha kutazama hizi filamu za kitanzania kwa sababu ya makosa mengi ya dhahiri

BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
1,630
2,000
Niliacha kutazama hizi filamu za kitanzania kwa sababu ya makosa mengi ya dhahiri kuanzia uigizaji na matukio yanayoendana na filamu zao.
Kuna mwigizaji hivi karibuni amejitokeza kwa filamu zenye misemo ya kiswahili hivyo kujizolea umaarufu. Alianza kunivutia kuangalia tena hizi movie zao ila naona hata yeye bado hayuko vizuri kwenye uhariri.
Kwa mfano kwenye mtirirko wa filamu yake inayoendelea sasa, kwenye kurudisha nyuma matukio ya mojawapo ya mhusika ambapo mwaka unaorejeshwa nyuma ni 1990 halafu linaonyeshwa gari Lina namba za usajili T...647,.DN...
Kwenye hilo hilo mhusika yuko barabarani na Bajaj na boda boda zinapita kwa wingi Jambo ambalo sidhani kama zilikuwepo mwaka 1990.
Ila sio shida kwa sababu hata watazamaji wao nao uwezo wao wa kupambanua ni mdogo.
Ahsanteni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom