Niliacha chuo ili nifanye biashara, sasa mtaji umekatika sijui nifanye nini?

genius mvivu

Senior Member
Apr 19, 2019
156
274
Naanza kwa kuwasalimu ndugu zangu wa JF,

Moja kwa moja niende kwenye mada, mimi ni kijana umri wa miaka 21, nilimalza A-LEVEL mwaka jana na nikachaguliwa kujiunga chuo.

Ingawaje nilikidhi vigezo ila sikuweza kuchaguliwa kozi niliyoitaka. Kutokana na umasikini na ufukara ulioikumba familia yangu ilinilazimu nikasome kozi hiyo hiyo, hivyo maisha yangu ya chuo sikuwah kuwa na furaha kutokana na kusoma kitu ambacho sikipendi hali iliyopelekea kupata supplementary kozi nne kati ya saba kwa muhula wa kwanza.

Hali hiyo ilinikatisha tamaa na kuamua kuchukua maamuzi magumu ya kuacha chuo, na kujiingiza kwenye ujasiriamali hela ya mwisho ya kujikimu tulipopewa ilinilazimu niondoke nalo na kuanza maisha mapya Jijini Dar. Nilitafuta sehemu mtaani nikalipa pango la miezi mitatu na kuanza biashara ya kuuza mtumba.

Hadi sasa nimepoteza mtaji na sijui nini la kufanya na hadi dakika hii, mama kjijini anajua niko chuoni nasoma nikamkomboe kwenye umasikini.

Kwa hiyo ninachoomba kweli wapendwa dada na kakazangu, kama kuna mtu yeyote anaweza kunipa kazi ya kufanya niko tayari maana hapa pango limeisha na sina hela ya kulipa tena pango. Nawaz nirudi kjijini ila sijui ntamweleza nini mama akanielewa.

Pia, kama kuna mfadhili yuko tayari kunisomesha tuandikiane mkataba nimlipe nikipata kazi kwa riba ile ile ya Bodi ya mikopo maana kule siwezi kukopesheka tena mpaka nilipe kiasi fulani nitashukuru.

Ahsante.
 
Kuna kizazi flani cha kielimu na stadi za kazi kilitengenezwa wakati wa JK ni janga kwa taifa.
Huu ni mfano wa mmoja katika maelfu ya hicho kizazi ambao wapo huku mitaani.
 
Halafu kitu kingine biashara sio vitu....biashara n muuzaji...muuzaji akiwa dhaifu bas lazma biashara lazma ianguke

Half kngne usikurupuke...fanya uchunguzi....!!

Mimi mwenyew nilipostpone masomo mwaka wa mwsho baada ya kuona ntamaliza boom bila ya kujiandaa na maisha...maana hali ya ajira niliiona

Lakini nilifanya research miezi mi3 kabla biashara gn ya kuweka na jinsi ya kuisimamia...mpk sasa mambo yanaenda vizuri tu
IMG_20190704_112830.jpeg
 
View attachment 1181065
Ulifanikisha vip mkuu naona story yako inanivutia hivi.....
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom