Nile Water Agreement (1929)

willy ze great

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
1,026
1,179
Huu mkataba uliosainiwa na serikali za kikoloni . Je kuna haja ya kuuvunja?

Nimekua nikijiuliza kwa muda mrefu kwanini hatutumii ziwa victoria kwa umwagiliaji lakini huko misri wanatumia kwa kila kitu na wanategemea 100% ya maisha mto nile ambayo chanzo chake ni ziwa victoria na kuzalisha umeme na kilimo cha umwalgiliaji.

Wakati sisi wanaafrica mashariki tunapata mvua za misimu ambazo hazitoshi kuwekeza kwenye kilimo na hivo tukiataabika na baa la njaa wakati mwingine na bei ya vyakula maradufu wakati mungu katupa hili ziwa victoria la bure kabisa tulitumie bila buguza? Kwann?

Baadhi ya masharti.

1.Misri imehakikishiwa kutumia mita za ujazo 55.5bn za maji, nje ya jumla ya mita za ujazo 84bn.

2. Hairusiwi nchi za africa mashariki kwenye chanzo yaani ziwa victoria kutumia maji haya kwa shughili za umwagiliaji, kusambaza maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.


3. Misrii itatumia maji hata kwa kufanyia jambo lolote lile mfano. Kujenga stigler gorge, uwekezaji wa mfumo ya umwagiliaji mashamba makubwa na madogo.

"These are people with no water," said the Tanzanian water minister, Edward Lowasa. "How can we do nothing when we have this lake just sitting there?" maneno ya lowasa hayo. 2004

The Ugandan commentator Charles Onyango: "Egypt can't enjoy the benefits of having access to the sea, while blocking a landlocked country like Uganda from profiting from the fact that it sits at the source of the Nile."

Aliekua Waziri wa maji wa Misri, Mahmoud Abu-Zeid, hivi karibuni alielezea nia ya Kenya ya kujiondoa mkataba kama "kitendo cha vita". Boutros Boutros-Ghali, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ametabiri kuwa vita inayofuata katika eneo hilo litakuwa juu ya maji.

Mkataba wa Nile, ambao Uingereza ulisign kwa niaba ya makoloni yake ya mashariki mwa Afrika, huzuia miradi yoyote ambayo inaweza kutishia kiasi cha maji kinachofikia Misri. Mkataba pia unatoa Cairo haki ya kukagua urefu wote wa Nile.

Wanasheria huu mkutaba wa kinyonyaji tunawezajaze kuukataa kama jumuiya ya Africa Mashariki?
images%20(1).jpeg
 
"Nile is Egypt and Egypt is Nile"....tulisomeshwa kwenye somo la Jiografia
 
Dah haya tuseme basi sisi Tanzania tuna neema kubwa ya rasilimali ,hivi Sudan unakokatiza huu mto hawautumii kweli na ukame wote ule ??
 
Nakumbuka Kuna Waziri Aliutengua Akapeleka Maji Ya Kunywa Hadi Kahama, Nadhani Kwasasa Amepumzika Siasa
 
Umoja wa Afrika wenyewe umezubalia mambo yasio na msingi wakati mambo kama haya yanaachwa.
 
Mapatano juu ya matumizi ya maji ya mto Nile yalifikiwa baina ya serikali za Misri na Ufalme wa Maungano (Uingereza) mwaka 1929 kwa njia ya kuba dilishana nyaraka za kidiplomasia.

Misri ilikubali kuongezeka kwa maji yaliyotumiwa kwa umwagiliaji nchini Sudan kama kiwango cha kutumiwa hakikuingilia na haki za Misri juu ya maji ya Nile.

Uingereza kama mlezi au mkoloni wa Sudan ilitambua haki za kihistoria za Misri juu ya maji ya mto Nile ikakubali ya kwamba matumizi ya maji ya Nile katika maeneo juu ya utawala wake yasihatarishe mahitaji ya Misri.

Haki za Misri katika mapatano Mapatano haya yaliipa Misri haki zifuatazo: ·

Misri ina haki ya kukataza kazi zozote zinaoweza kuwa hatari kwa mwendo wa maji ya mto Nile · Misri ina ahidiwa matumizi ya mita za ujazo bilioni 55.5 katika jumla ya billioni 84 m³ ya maji ya Nile. · Misri ina haki ya kutembelea na kuchungulia kila mahali
kwenye mwendo wa mto Nile na kuchungulia
miradi yote ya matumzi ya maji kando lake.

Sababu za kufanya mapatano
Sababu ya kufikia mapatano haya yalikuwa
mabadiliko ya kilimo katika nchi zote mbili.

Misri iliwahi kutumia maji ya Nile hasa kwa njia ya
mafuriko yake iliyofunika kila mwaka mashamba
kando la mto na kuacha matope yenye rutba juu ya
mashamba yale na pia kwa nia ya mifereji midogo iliyopeleka maji kwa kanda nyembamba ya
mashamba kando la mwendo wa mto.

Lakini tangu mwisho wa karne ya 19 kilimo cha pamba kilisambaa iliyohitaji kumwagiliaji wa kudumu pia mbali zaidi na mto. Kwa hiyo Wamisari walianza
kuangalia na kupima kiwango cha maji yali yopatikana .

Katika Sudan serikali ya kikoloni ililenga
kupanusha eneo la mashamba kwa njia ya
umwagiliaji. Pia ilitaka kupunguza upotevu wa maji
katika eneo la Sudd ambako vizuizi vinasababisha maji kukwama yakifunika eneo kubwa sana ya
maziwa na mabwawa matope kwa hiyo maji
mengi yapotea kwa njia ya uvukizaji kwa sababu ya joto kali ya sehemu zile.

Kwa hiyo Waingereza walipanga kuchimba mfereji wa Jonglei kwa kusudi la kupunguza kiasi cha maji kinachokwama kwenye Sudd na kuvukiza badala yake kuyapeleka kwa njia ya mfereji hadi Khartoum. Wakati huohuo mipango iliunda hofu ya kwamba maji yanaweza kutumiwa kumwagilia mashamba mapya kando la mfereji.

Mapatano baada ya ukoloni Tangu miaka ya 1950 na 1960 Uingereza haitawali tena maeneo ya Afrika na nchi za kujitawala zilianzishwa kando la mto Nile ambazo ni Sudan, Uganda, Kenya na Tanzania zilizokuwa zote chini ya Uingereza.

Waingereza waliwahi kufanya mapatano na serikali ya mfalme Menelik II. wa Ethiopia pia iliyoahidi pia kutojenga malambo au kuanzisha
miradi inayopunguza mwendo wa maji ya Nile ya buluu.

Misri inadai hadi leo ya kwamba nchi zilizojitokeza tangu uhuru ni wafuasi wa Uingereza katika mapatano.

Wanasiasa Wamisri waliwahi kudokeza ya kwamba Misri inatazama swali la maji kama jambo la usalama la taifa au kwa maneno mengine yalitisha ya kwamba matumizi ya maji katika nchi nyingine inaweza kusababisha vita. Serikali za nchi nyingine zilikataa kukubali.

Ila tu Sudan alikubali mwaka 1959 mapatano mapya inapotambua kipaumbele cha MIsri juu ya maji yale.

Hadi mwaka 2011 majadiliano juu ya mapatano
mapya yaaendelea kati ya nchi zote jirani wa Nile.

1910 Ethiopia, Uganda, Tanzania na Rwanda zilitia saini mapatano mapya kati yao juu ya matumizi ya
maji ya Nile lakini Misri ilikataa kukubali hatua hii.
 
Back
Top Bottom