Nikupe siri kidogo ya Kudumisha Maisha ya AC ya gari yako na Maisha yako Binafsi

Samatime Magari

Senior Member
Feb 10, 2017
103
387
Kwenye mfumo wa AC kuna kitu kinaitwa Cabin Air Filter, Hichi kifaa kinasaidia upate hewa safi kwa kuchuja vumbi, uchafu na chochote kisichotakiwa kufika ndani ya gari[harmful pollutants].
.
Sasa watu wengi hatukijui so huwa kinakaa kinajaa uchafu kinaziba au kinafanya upenyo wa hewa kuwa wa shid, Utaona unaanza kusikia harufu mbaya ambazo huzielewi..
.
Uchafu unajaa mpaka unaanza kupenya kwa nguvu na hii inasababisha Ufanisi wa ac [cooling defrosting defogging] unakua affected.
.
1655128723370.png
1655128798652.png

.
Baadhi ya Watu huwa vinawapa mpaka mafua/vifua na vikohozi visivyoisha sababu ya kuvuta hewa chafu bila kujua, Hapa Pua, Koromea, Trachea na Mapafu yako wanaguswa kwa namna moja ama nyingine na Unajikuta unakohoa na hujui chanzo nini unaweza hisi umepigwa kipapai kama we bado ni wa imani, upendo na miujiza
.
Anyway tuendelee, Hii Filter Ikiziba inafanya ac kufanya kazi nguvu ili hewa ipite [hapa unaitesa motor ya blower], Blower ni kileta upepo ndani na hapa itabidi kitumie nguvu nyingi sana [energy consumption inakua kubwa]..
.
In short HVAC [Heating, Ventilation, and Air Conditioning] inabidi ifanye kazi ya ziada ili mambo yaende sawa, Sasa automatic inapunguza lifespan ya vifaa vinavyofanikisha unapata ubaridi ndani ya gari na Hapa tunawagusa [Blower, Evaporator, Compressor, Condenser ]..
.
1655128859230.png
1655128931885.png
1655129049103.png

.
Inashauriwa hii filter kubadilishwa kila baada ya km around 30,000, Ingawa hapa inategemea na mazingira unayoendeshea gari. Kibongo bongo kama unatumia Barabara za Kimara Bonyokwa Kisemvule Mpiji Magohe etc nakushauri ukiwa unafanya service nayo iangalie kama imejaa uchafu weka mpya tu na Bei zake ni nzuri inategemea na gari aiu ikishindikana piga upepo, il Kama imeshaanza kutoa nyuzi nyuzi nunua mpaya tu
.
Kuibadilisha ni rahisi hata mwenyewe unaweza, Maranyingi iko chini ya dashboard mbele upande wa abiria ukifungua ile cabin ya vimizigo vidogo dogo Utaikuta hapo ndani na Inapachuka kirahisi.. .
.
1655129578389.png
1655129596858.png

.
Natumaini umejifunza kitu basi unaweza share na wengine wajifunze pia na kama unahitaji kuagiza gari, kununua hapa nchini showroom au mkononi karibu, Tunafanya kazi na dealers wa Japan, UK, Singapore na hapa nchini, dealers wanaotupa gari nzuri kwa ajili yako..
.
Simpy bofya link [Samatime Cardealers] kwenye njoo whatsapp au ofisini Posta Phoenix House floor ya 4 mkabala na Mkapa tower tutaku assist, Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu pia..
.
Utatupa hitaji lako tutakupa ushauri then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice na utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo..
.
Asante
Samatime Car Dealers Co LTD
0714547598
 
Binafsi kukiwa na mvua kuna harufu furani nakisikia kwenye gari. Nimechunguza kila sehemu hakuna shida. Hiyo filter kuna zaidi ya miaka minne sijabadilisha wala kupulizwa na bara bara zangu ni bonyoko, mbezi makabe na mpiji magoye
 
Back
Top Bottom