Nikumbukwe kwa mambo nane nikiondoka ikulu 2015 -jk | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikumbukwe kwa mambo nane nikiondoka ikulu 2015 -jk

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ICHONDI, Oct 1, 2010.

 1. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  brahim Bakari, Kaliua
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amesema anataka Watanzania wamkumbuke kwa mambo nane wakati atakapoondoka Ikulu 2015.

  Kikwete alisema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Jimbo la Urambo Magharibi alipokuwa akiomba ridhaa ya wananchi kumrejesha kuongoza serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.


  "Nimesema kuna mengi nayafanya, lakini nikimaliza kipindi changu nataka watu wanikumbuke kwa mambo nane... waseme Mungu amrehemu, yule bwana acha tu, amefanya kitu."

  Huku akishangiliwa na mashabiki, wanachama na wapenzi wa CCM, Kikwete aliyataja mambo hayo kuwa ni; kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kupitia mpango aliouasisi wa Kilimo Kwanza, matumizi bora ya mbolea, dawa za kilimo, kutoa wataalam na maofisa wengi wa kilimo.
  Pia kusaidia upatikanaji wa masoko kwa mazao ya wakulima, kusimamia uwepo wa bei bora za mazao, kuimarisha barabara ili wakulima waweze kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuachana na jembe la mkono na kutumia matrekta makubwa na madogo.


  Kikwete aliyekiri kutofikiwa malengo kwa maeneo mbalimbali katika sekta ya maji na barabara, alisema katika kipindi cha miaka mitano ijayo serikali imejipanga kikamilifu kutekeleza ahadi zake.
  Alisema kuna mengi yanahitaji misaada ya wahisani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya maji hivyo ni lazima tuwatafute wahisani.

  Akizungumzia safari zake za nje, Kikwete alisema: "Wapo wanaosema nasafiri sana, sasa ningekaa pale nyumbani kwangu nikamwangalia mke wangu Salma halafu nimwambie aisee ulivyopendeza, Watanzania wangekufa njaa na Wajapan wanaotaka kusaidia, leo hii wasingeijua Kaliua.

  "Sasa kuyapata yote haya, lazima nisafiri. Nilikuwa Marekani, nikakutana na wahisani mbalimbali; wenyewe wananiuliza wanataka wanisaidie wapi, mimi nasema hapa na hapa na pale... kuna watu wanapesa nyingi tu."
  Akizungumza katika mkutano huo, mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya alisema CCM wameshafundishana kucheza mpira wa uchaguzi.

  "Pasi ya kwanza anatoa diwani, diwani kwa mbunge na mbunge anatoa kwa rais anafunga goli... Kikwete ni (mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan) Mgosi wa CCM, ukimpa mpira anafunga," alisema Kapuya na kuamsha vicheko kwa wote waliofika kwenye mkutano huo.

  Naye Kikwete aliyekuwa pembeni, baada ya Kapuya kumaliza, alisema: "Aah! Mimi bwana na Kapuya kuna mengi tunakubaliana, lakini katika soka, tuko timu tofauti, mimi siko huko," alisema Kikwete ambaye anajulikana kama shabiki mkubwa wa Yanga wakati Kapuya ni shabiki asiyejificha wa Simba. Hata hivyo alimaliza kwa kusema: "Timu bora inajengwa na ngome imara, kiungo imara na safu yenye mtazamo mmoja na ndiyo inayoshinda kuliko kuchanganya."

  Naona JK sasa amechanganyikiwa moja kwa moja. Au la muandishi wa habari hakuandika mambo yote nane aliyosema JK. Kwa kuwa ameongelea sekta moja tu ya kilimo. Hata hicho kilimo kwanza ndio kwanza kinaanza, hatuna uhakika kuwa kitafanikiwa wakati wajanja wanakula fedha kila siku. Hata huo mradi wa kuagiza matrekta ulikuwa wa kifisadi sana!!!!
   
 2. G

  Gashle Senior Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huu ni upuuzi wa hali ya juu, kama mzee mzima ndio uchambuzi wake wa mambo ulivyo (kwamba hapo kuna mambo manane tayari), si ajabu hajui kwa nini tuko maskini. Inauma.
   
 3. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  JK jana, anasema, ....."Nimesema kuna mengi nayafanya, lakini nikimaliza kipindi changu nataka watu wanikumbuke kwa mambo nane... waseme Mungu amrehemu, yule bwana acha tu, amefanya kitu (sourrce Mwananchi, 1/10/2010).

  Swali langu kwa wana JF, huwa tunasema bwana amerehemu mtu akiwa hai au mfu. Kiswahili kimenipiga chenga.
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kiswahili hakijakupiga chenga Mkuu.
  Kikwete ana maana hata atakapokuwa amekwishakufa watu wamuombee kwa Mungu wakikumbuka mema ambayo yuko supposed kuwa ameyafanya.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nikumbukwe kwa mambo nane nikiondoka ikulu 2010.

  Hatutakuwa na haja ya kukumbuka wewe jiondokee tu!!!!!!!
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  huyu mzee vip ?
   
 7. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Baada ya kutoa Ahadi zooote, Sasa Ahaidi KUFA :A S 13:. Huyu jamaa kiboko:hand:
   
 8. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #8
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  "
  Nimesema kuna mengi nayafanya, lakini nikimaliza kipindi changu nataka watu wanikumbuke kwa mambo nane... waseme Mungu amrehemu, yule bwana acha tu, amefanya kitu."
  Jamaa Kaahidi KIFO chake. Mungu mrehemu Marehemu sio mtu akiwa hai.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tutamkumbuka kwa jinsi alivyotuingiza mkenge katika mikataba ya madini. Tutamkumbuka kwa jinsi alivyotuletea wawekezaji kuchukua ardhi yetu na wananchi kuhamishwa. Tutamkumbuka kwa jinsi alivyokumbatia mafisadi na kuacha ufisadi ushamiri chini ya uongozi wake. Tutamkumbuka kwa jinsi alivyosaidia kuua utawala wa kisheria nchini Tanzania. Tutamkumbuka kwa jinsi alivyoanza kutuletea utawala wa kifamilia.
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Duh! hiyo nayo ipo kwenye ILANI yao? am doomed kwa kweli lol
   
 11. Mubezi

  Mubezi Member

  #11
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu jamaa nashangaza,baada awaache wananchi wamsifu anajisifu mwenyewe,hooooo nimeahidi nimetimiliza,hooooo nitanikumbuka kwa mengi,mi nakuomba uwaache wananchi wakuulize,au waulize maisha bora wamepata uliowaaidi,sio ujisifu mwenyewe,au ndio unatuaga?,mana dk wako sher hayaha kasema kuna mgombea atakufa kabla ya uchaguzi,twambie mzee mana toka umeanza kampeni haujaenda kubadilisha dam,yawezekana wadudu wamezidi.
   
 12. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #12
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Mkuu pmwasyoke;1115501, asante sana kwa kunipamoyo kuwa kiswahili changu kiko fiti.

  Ila tatizo linakuja pale JK anapotoa ahadi alafua anamalizia watu wasema MUNGU AMREHEMU. Huoni hapa kuna tatizo? Je ni ahadi kuwa baada ya kutoka ikulu 2015 moja kwa moja atakufa au? Mimi bado ninaomba msaada wa kueleweshwa!
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  No matter how hard I can try to remmember anything Mkwere huyu kafanya miaka 5 iliyopita honestly sipati japo dogo tu la kujifariji nalo! CCM wanalijua hilo wamekimbia midahalo yote! Ninacho kumbuka kila nikiwaza Kikwete, mshikaji narenare,kaanzisha vita dhidi ya ufisadi katishiwa kafyata mkia, (can you imagine a sitting president), ujenzi wa barabara ulimalizika pale ben alipoondoka imagine hata km 10 za mandela road zimekushinda, rushwa bandari ya dar wananchi wameihama, usimamaizi na ukusanyaji mbovu wa mapato ya serikali, mzee wa ahadi, tayari keshaahidi underground train, nadhani mradi wa mabasi yaendayo kasi keshaumaliza (jamaa anaahidi mpaka anasahau) naweza simulia siku nzima failures za mswahil huyu!
  Kama lipo hata moja la kumkumbuka naomba mtu 1 atukumbushe!
   
 14. A

  Akiri JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Naona utabiri wa Shekhe unaanza kutimia taratibu du jamani niagieni du...
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nCHI MASIKINI ITAENDELEA KWA KUTEGEMEA MISAADA TOKA KWA WAHISADNI (jk)
  NDO MAANA NAMPENDA SANA HUYU JAMAA NIMKWELI KABISAA!!
   
 16. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hiyo ahadi ya mwisho ndiyo itakayotekelezwa ndani ya miaka mitano. mungu amlaze mahali pema.aaaaaamin
   
 17. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,483
  Likes Received: 1,215
  Trophy Points: 280
  akumbukwe kwa
  ufisadi
  kugawa vyeo kwa masela wake
  kuanguka anguka
  kucheka cheka
  kujaza mabango
  kuogopa midahalo
  kutojua kwanini nchi ni maskini
  kusafiri kama vasco da gama
  :smow:
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,853
  Likes Received: 11,974
  Trophy Points: 280
  Wahenga husema mtu akikaribia kufa huwa anaaga kwa aina yake, hata Baba wa Taifa alipokaribia siku zake alisema 'Najua watanzania mtalia lakini nitawaombea kwa Mungu'. Kama JK mwenyewe kasema hivyo basi nami nasema amrehemu marehemu mtarajiwa.
   
Loading...