Nikubali au nikatae Ushauri wako muhimu sana

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
954
1,035
Mambo vip? wakubwa zangu shikamooni wadogo zangu mambo?
Ipo hivi jamani nina mwanamke muongo saana yaani alishanidanganya mpaka nimekua shazoea yaani mpaka akiniambia kitu now simuamini kabisaa yaani ata akijaribu kuniaminisha simuamini hata chembee yaani simuamini kwa sababu ya uwaongo wake aisee.

sasa kilichonifanya nije hapa yule mwanamke nilikuaga nae mkoani baada ya kuona uwongo umezidi sana nikaona bora nimuache tuu ila yeye hakukubali matokeo. mwaka 2017 mwezi wa 3 nikaona simu kupokea ni yeye nikamuambia unasemaje? eti akaniuliza hivi mara ya mwisho mimi na wewe kukutana kimwili ni lini?
nikamuambia sikumbuki akanambia sawa. nikamuambia kuwa usinitafute tena now nina mdada mwingine na soon nitamuoa akanambia Hongera.

Nimekaa siku moja kuna broh wake akanipigia simu akanambia kuwa demu wako ana mimba kubwa tuu nikamuambia kasema ni ya nani akasema hajui bado? mwanamke akajifungua mtoto mtoto amekua mpka kafikisha miezi 9 sijatafutwa ikabidi nimtafute nikamuambia nasika una mtoto akanmbia ndio nikamuuliza ni wa nani aksema Ni wa (john) factious name ambae alikuwaga ni ex wake niakmumbia sawa.

Nikaaa akanza kunitafuta ooh mtoto ni wako siku niliamua kukujibu vile kutona na siku ile nilivokupigia simu nikakuuliza ukanijibu dharau ndo mana na mimi nikaamua kukujibu vile ila mtoto ni wako nikamkataa nikamuambia mtoto sio wangu kama ni wangu ungenambiaa akanmbia sikutaka kukuambia kwasababu ulishanambia una Mchumba na unaenda kumtambulisha kwenu.

wakuu samahani kwa maelezo marefu ila kwa maelezo hayo naomba ushauri mtoto atakua ni wangu au anatka kunibambikiziaa mimi binafsi sijakubaliana ila kuna nafsi mbili zinapingana moja inasema ni wangu nyingine sio wangu naombeni ushauri wenu tafadhali.
 
Kama hukumbuki Mara ya mwisho kukutana nae kingono ni Lini mtoto anaanzaje kuwa wako? Jiongeze kumbuka demu muongo huyo
 
Nimeishia hapo umesema una mwanamke muongo sijaendelea mi nakushauri achana nae najua nikiendelea kusoma nitakuta visa vyake tu wakati we unampenda, huyo muache.
 
em kamuangalie mtoto bro kafanana na ww au wapeleke ndg jamaa na marafk wakamuangalie kama ni copy yako au lah
 
Mkazie ila usimkatae huenda ni wako. Ila mkazie, mwanamke ukimkazia anasema yote.

Kuna mengi hapo.
1. huenda alitaka mtoto nawe ila akaona akikuambia utaitoa.

2. Sio yako ameamua kukuzingua tu..Sababu anaijua mwenyewe.

Ila toka siku nyingi unaonekana unacheza naye ndiyo maana hakuheshimu...nadhani umri(wa akili) nao ni kikwazo.
 
Aisee kuna watu waongo hadi akikusalimia habari za asubuhi inabidi uangalie saa kwanza kama kweli ni asubuhi alafu ndo unamjibu, .... Kampime DNA huyo mtoto usikate bia visibitisho.
 
Mkuu ,tatzo umelitafuta mwenyewe ,

Kulikua na haja gani kuntafuta na kumuuliza kwamba ana mtoto wakat yy mwenyewe kakausha tu
 
Nimeishia hapo umesema una mwanamke muongo sijaendelea mi nakushauri achana nae najua nikiendelea kusoma nitakuta visa vyake tu wakati we unampenda, huyo muache.
naunga mkono hoja.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom