Niko tayari kufukuzwa ccm kwa sababu ya kusema ukweli-januaryyy makambaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko tayari kufukuzwa ccm kwa sababu ya kusema ukweli-januaryyy makambaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 5, 2012.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,230
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  BIG UP MKUU KAMA ILITOKA MOYONI
  Katibu wa Mambo ya Nje ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Januari Makamba, amesema haogopi kufukuzwa kutoka katika chama hicho, ikiwa hatua hiyo inalenga kukidhi maslahi ya wanasiasa wasiokuwa wakweli.

  Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), anasema ukweli ni moja ya misingi iliyo nguzo ya kukikifanya chama hicho kukubalika kwa umma na kuendelea kushika hatamu za uongozi.

  Hivi karibuni, Makamba alitajwa kuwa mmoja wa wabunge ‘waliosulubiwa’ wakati wa kikao cha wabunge wa CCM cha hivi karibuni kutokana na kile kinachodaiwa kupingana na misimamo ya chama hicho.

  Mbunge huyo amekuwa miongoni mwa 'makamanda' wanaopinga ongezeko la posho za vikao kutoka Sh. 70,000/- hadi 200,000/- kwa kila mbunge kwa siku, kwamba haliendani na hali ya uchumi wa nchi ama hali duni ya wananchi walio wengi.

  Wabunge kadhaa wakiwemo wenye nyadhifa za uwaziri, wametajwa kuwa nyuma ya hoja hiyo, lakini Makamba anasema kila jambo analolifanya, linalenga kuinufaisha CCM na serikali.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki, Makamba alisema wabunge na mawaziri wanaoamini kuwa anastahili kufukuzwa uanachama wa CCM, wanapotoka na kwamba wameshindwa kupima matakwa ya jamii.

  “Wenye kutoa hoja hiyo wamepotoka, wanapaswa kuipima jamii tunayoingoza, ina matakwa gani,” alisema.

  Makamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema CCM inakabiliwa na changamoto ya kutambua msukumo uliopo kwa wapiga kura na mtazamo wa wanasiasa wa kizazi cha sasa kinachohitaji suluhu ya matatizo badala ya maelezo.

  Naye Mbunge wa Simanjro (CCM), Christopher Ole Sendeka alisema wana CCM wanaowaona wabunge wanaotoa maoni yanayotofautiana na maslahi yao kuwa ni wahalifu, hawajui misingi ya haki inayoanishwa kwenye Katiba ya nchi na ile ya chama hicho.

  Alisema kuna baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaoshindwa kuutambua ukweli, badala yake kusimamia hoja inayolenga kuhujumiana miongoni mwao.

  Kuhusu tabia ya wabunge wa CCM kupinga hoja za mawaziri, Ole Sendeka aliionya serikali ili ijiepushe na mazoea ya kukurupuka wakati wa kuwasilisha hoja na miswada bungeni.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos Makalla katika mazungumzo nami alisema katika masuala yenye maslahi kwa umma hususani ndani ya mipaka ya majimbo, hakuna sababu ya kuionea aibu serikali hasa pale inaposhindwa kutekeleza wajibu wake.

  Anabainisha moja ya maeneo yasiyostahili chembe ya aibu dhidi ya serikali ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho 17 ikiwamo Bodi ya Mikopo iliyobainika kuwa na ishara za ubaguzi hasa kwa raia walio masikini.

  Mapema wiki hii, wabunge wengi wao wakiwa kupitia CCM, walishinikiza kuondolewa kwa hoja mbili za serikali zilizotolewa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema.

  Hoja ya Mkulo ilihusu kuliomba Bunge liidhinishe punguzo la ushuru wa maji ya kunywa kutoka Shilingi 69 hadi Shilingi 12, wakati Werema aliwasilisha hoja ya mabadiliko ya sheria 17 ikiwemo ya Bodi ya Mikopo. Hoja hizi sasa zitaletwa tena kwenye mkutano ujao mwezi Aprili mwaka huu.
   
 2. K

  KWA MSISI Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source please!
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  haachi!!
   
 4. nyamemba

  nyamemba JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 689
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  hivui mnamwamini sana huyu j makamba?si yeye aliyemwandikia baba riz hotuba ile ya wazee wa dsm eti atakaye andamana apigwe virungu afu ati sihitaji hivo vikura vyenu 350000?
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,230
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  Tungekuwa tunakumbuka kila kitu kama wewe tusingekuwa na wake zetu wengine
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,115
  Trophy Points: 280
  " popularity automatic search"
   
 7. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  [FONT=&amp] Wakitaka kukufukuza wakumbushe ahadi za mwanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hasa ahadi #2, 3, 6, 8

  AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI[/FONT]


  [FONT=&amp](1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja[/FONT]
  [FONT=&amp](2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.[/FONT]
  [FONT=&amp](3) Nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.[/FONT]
  [FONT=&amp](4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.[/FONT]
  [FONT=&amp](5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.[/FONT]
  [FONT=&amp](6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.[/FONT]
  [FONT=&amp](7) Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.[/FONT]
  [FONT=&amp](8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.[/FONT]
  [FONT=&amp](9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika

  Ni wazi kuwa wanaounga mkono posho hawalengi kuondoa umaskini wa nchi na dhuluma kwa watanzania wengine. Pia hawatumii uwezo na nafasi zao kwa faida ya watu wote, na hawatumii rasrimali za nchi kwa manufaa ya waru wote.
  [/FONT]
   
 8. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo anatuthibitishia kuwa huko ccm kazi ni unafiki tuu na kufichana ukweli? Ya nini kushirikiana na wanafiki?
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,230
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280

  umsehau ile nyingine shindanaa/pigana mpaka kufa
   
 10. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hahahahahaaaa, wewe uko dunia gani wewe? Hizo ahadi siku hizi hazitumiki kama zinavyoosomeka, bali zinatumika kinyume chake!
   
 11. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko
   
 12. W

  We know next JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wasingoje kufukuzwa, kama wanaona chama kimepoteza muelekeo, wajitoe mapema wenyewe, wataheshimika zaidi.
   
 13. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hafukuzwi mtu hapo. Hao jamaa wanataka kuleta hoja itakaowahamisha watanzania kutoka kwenye machungu ya mgomo wa madr na posho za wabunge,ili badala yake tuanze kushikana mashati kwa hili jambo la kipuuzi kabisa. Hamna kitu hapo, jamaa wanajua wanachofanya. Jamani mpaka hapo humjajua janja ya hawa watu?
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Nadhani umefika wakati muafaka CCM wafanye Mtaguso na kuifuta ahadi namba 8 kwa kuwa haina maana tena
   
Loading...