Niko njia panda naombeni msaada

yani kwa kweli mi naona ni chenga tu, na kigezo cha kua mke wangu hana ata kimoja zaidi ya ile portability yake tu, ila sifa zingine hana
Unadhani muda wakuoa vigezo vitatimia kama unavotaka,kua uyaone,utamkumbuka huyo dada nakwambia
 
Sikiliza moyo wako kubali mapungufu yako za mchecheto changanya na za multitalented123
 
Hukumpenda wewe sida yako ilikuwa ngono tu vinginevyo maneno hayo anayakwambia sio ya kumuacha mtu chaguo la moyo wako, au umeamua kufanyia kazi ushauri wa rafiki zako ama kujishaua.
 
mwaka jana mwishoni kuna msichana nilianza nae uhusiano wa kimapenzi japo kua rafiki zangu karibu wote hawakuniunga mkono mimi kua na yule dada. nami nilichukulia kawaida tu ni maoni tu ambayo watu wanweza wakazungumza.

mwanzoni mwa mwaka tukiwa katika penzi zito kuna maneno aliyokua anaongeaga nami nilikua siyapendi japo sio mara zote nilikua nikimkaripia kuhusu kauli zake,
mara utamsikia akisema umenikuta kwetu nikiwa nakula,navaa na chochote ninachotaka kutoka kwetu nakipata,
mara pamoja na kwamba natongozwa na watu wenye hela na magari ninawakataa nimeamua kukupenda wewe kwa sababu unamapenzi ya kweli japo hauna pesa bado, mara saa ingine nikisafiri ananiambia ulienda kwa wadada wengine.

imepita kipindi hivi kama mwezi hatujawasiliana vizuri na juzi nikakaza sitaki mawasiliano nae tena leo mama yake mzazi kanipigia simu ananieleza kwamba yule dada hataki kula wala kusikia chochote hivyo anaomba nimsamehe mwanae!!!
na mimi sipo tayari kabisa kua nae tena kulingana na sababu hizo na zingine nyingi. sasa wakuu nifanyeje???
na dada anataka kuolewa lakini mi ndo kwanza nishabadilisha maamuzi
msaada samahani....
Wewe ni mwanaume buana. Mimi niliwahi kuwa natoka na binti mmoja wa Country code +254.. Sasa nikaona analazimisha nikamtambulishe home huko mwisho wa reli.

Baada ya kuwaza na kuwazua pamoja na ubabe wake nikaamua kumpiga chini. Sasa nilikuwa napigiwa simu mpaka na wanaume wanasema ni kaka zake wakisema aisee Victoria amelazwa yupo hoi kwa kuwa umemuacha.

Likanipigia janaume limoja linasema ni li baba yake, ooh mtoto wangu akifa ujue wewe na mimi, nikasema nyoo, na afe tu kama ameamua na ujue tu mimi ni mtanzania dume la mbegu hamniwezi.

Akaja kupiga mama yake eti anamuombea msamaha kama alinikosea nimsamehe turudiane. Nikasema hajanikosea, ni vile tu hatuendan na hatuwezi kuoana. Nilichofanya baada ya kuona jam limezid nikaamua kutopokea namba yoyote inayoanzia +254.. na baadae maisha yalienda, memory zikafutika.

It is the matter of time and every thing will be at the bottom of the sea. Vaa roho ya chuma.
 
Duh kama umeweza kumtoa Moyoni kabisa..Duh! Hapo hapana Mapenzi kabisa. Mwambie huyo Dada ukweli.. Utamuweka huru hatakama ni mchngu vipi ataumia kwa kitambo kdgo tu but baadae atazoea na atapona. "Hurt Me with a Truth but never Comfort Me with a Lie"
 
We nae multitalented umtuficha vitu vingi ndio maana watu wanashindwa kukushauri inavyotakiwa.
Kwanz jiulize kwanoni anakwambia kuwa yeye kawao anaueezo huo so isimuone kama kafanya vitu kwako?? Je ni kweli kwao wanauwezo mkubwa wa kujitapa hivyo au na wewe hiwa unamnyanyasa kupitia mali zako??

Kwa nini anadao kuwa anatonhozwa na wanaume wenye pesa na magari lkn anakupenda wewe tu?? Je kama akimkubali kati ya hao wenye magari unadhani atakwambia?? Siku zote mwanamke anakwambia kama kakutana na mbulula lkn akikutana na mkali thubutu hawezi kukwambia.

Je mbali na hizo tabia ulizotwambia kuna zingine mbaya zaidi? Je kwa nini marafiki zako toka mwanzoni hawakukuunga mkono ktk uhusiano huo kulikuwa na tatizo gani ambalo wewe uliziba masikio na.kufunika vibanzi machoni kujifanta huoni??
I guess huyo femu alikuwa kimeo, na ndio maana haya washikaji wako walikudis sana wewe.ukajiganya kichwa ngumu.

Si kila wakati watu wako wanapokuonya kuhusu uhusiano wako ukadhani wanakuonea wivu huwa wanajua mengi sana mtaani usiyoyajua.
mtu kukupenda sio kigezo cha kumwoa wala kufunga ndoa swala ni kwamba huo upendo uko kwenye nini?? kama upo kwenye mali siku mali zikiisha basi hakuna upendo, na kama anasema napenda tu bila masharti wakati mi naona sio hivo ya nini kuendelea kua nae??
 
experiance inasema hapo chapa lapa, hao zamadamu hawanaga akili, we ulikuwa second choice au substitute wa mtu
Kama ukweli vile, huyu jamaa alikuwa second choice au hata third hand hapo. Ni baada ya mambo kumwendea ndivyo sivyo akaona aibuke na huyu jamaa hivyohivyo.
 
midomo ya hawa watu,sema kama ndo maamuzi yako hayo yakoleze na kupigia mstari,kuomba ushauri ni sawa na kukosa msimamo au kujiingiza kwenye njia panda.
 
Mkuu inabidi tu uusikilize moyo wako unavyokuambia. Kitu muhimu tu ni kwamba inabidi uwe na msimamo. Sio kwenda mbele na kurudi nyuma. Halafu bro, ulisema kuna sababu nyingine nyingi ambazo pia zinakufanya uachane naye, basi sio vibaya ukiwaeleza wadau ili wakupe a more well-informed ushauri
 
Mama gani anapigia viboyfriend simu?

Real african mama would never do that shit,
Tena akisikia huli coz of a boy, damn she gonna beat the shit out of you

Piga chini husimpotezee muda kwa huruma zisizo na msingi
 
Back
Top Bottom