Niko njia panda: Mimi ni masikini na ninayempenda kwao ni masikini zaidi

Haswa...

Jamaa anajiita masikini ilihali kaweza kujiunga Jeiefu na kuweka posts! bila shaka anamiliki simu au tarakilishi...na kaweza nunua bundle

Hii ina maana somehow anaweza pambana na kanunua vitu luxurious kwa masikini wa kweli...
Kwa hiyo nitembee kifua mbele huku nikiwa na matumaini kuwa siku moja nitakuwa "mtu fulani" sio!!
 
Kila famili inachangamoto zake. Kua alietoka familia ya kawaida au yenye pesa haikugarantee maisha ya furaha
 
Kaka oa kama mnaendana, usiangalie, mwilini , utadanganyika, angalia uzuri wa ndani , je anamcha MUNGU,? Ana hofu ya MUNGU? Moyoni mwake kimejaa vitu gani? Je ni msafi?
Unajua umasikini ni kujitakia. Lakini duniani MUNGU ametuumba sawa kwamba tuna akili na utashi.
Sasa kila mtu amepewa nafasi ya kuchagua aina ya maisha anayoyataka , kwahiyo unachochagua ndicho unachopewa( unachokiona ndicho unachopewa- Mwanzo 13:14-15).
Hali ya mwonekano wa mtu kwa nje usikudanganye hata kidogo kaka.
Mwanamke anayefaa kuwa mke utamuona tu, kuongea kwake, kuvaa kwake, kutembea kwake, kwa uchaji wake kwa MUNGU na jinsi anavyoishi ni kiuharisia siyo kwa kuigiza.
MUNGU akupe hekima tu ya namna ya kuishi naye umuongoze mjenge maendeleo yenu na familia bora yenye kumcha MUNGU.

Jitambue kuwa nyie ni matajiri kupitia NGUVU zenu wenyewe kila kitu kinatafutwa. Maisha ya kuanza pamoja ni mazuri sana. Hasa wote mkijitambua na kujua lengo lenu ni nini.
Maisha ni kupanga , na kupanga ni kuchagua, muwe akina nani.
Nakutakia kila la heri.

Sent from my KIW-L24 using JamiiForums mobile app
 
Soma hapa wewe boya, umenikera sana! Dogo ukiwaona maskini utasemaje? Uko mkoa gani ili nikisafiri nikichukue nikakuonyeshe maskini??
961f167106055ea72649375d5042c092.jpeg
 
ukweli nampenda huyu mwanamke na naamini nae ananipenda, natamani tuje kuishi pamoja(mke na mume), mimi natoka familia masikini(naweza sema sana) ila mwenzangu amezidi. nimejitoa kua kwa lolote nijitahidi kwa kadri nitakavyoweza, ila kuna muda kuna kasauti kananijia kua haya majukumuni makubwa sana hovyo kama kananishawishi ni stop. silelewi. ingawa kwa asilimia kubwa moyo unanituma kukomaa nae as long personally tuna match.
Kama unaamini wewe ni maskini basi huna sababu ya kuhangaika na hayo mambo kwa sasa. Kajitupe huko mjini utafute pesa. Ukiishika shekeli utampata yeyote unayemfikiria. Hata wale ambao ukiwaona tu unajikatia tamaa hapohapo kuwa hutawaweza.
 
Hakuna swali gumu ukweni kama kuulizwa kijana unafanya kazi gani hasahasa binti akiwa anatoka familia bora...
 
We dogo Maleven,
dogo kuzaliwa maskini si tatizo na wala si zambi, zambi ukifa maskinI. ........ kama vipi nikupe namba za tajiri gani akupe mwanaye
 
Sikuhizi Ukimpenda mwanamke inabidi uangalie na hali ya uchumi ya nyumbani kwao?
Ili uufanyie nn huo uchumi wa nyumban kwao, kwamba unaweza ukapata share hapo?

Kikubwa ni kupambana tu watafute za kwao, umaskini si kilema, maskin wa Leo ndo tajiri wa kesho juhud na maarifa ndo chanzo cha utajiri. Nyie oaneni tu as long as mnapendana.
 
Kabla hujaweka proposal ya kuowa embu tafuta pesa naye awe na kitu cha kujiingizia kipato iwe biashara ndogondogo au ata kazi ya viwandani ambazo nyingi haziitaji elimu kubwa iyoo itawasaidia kujikimu na kusaidia familia zenu usiowe kwaajili ya nyege kijana au mhemko wa kihisia utajiona umekosea sana maishani jipeni muda tafuteni pesa ndoa ata iwe miaka 29 au 30+
 
Kuwa na masikini yataka moyo wa chuma, ukiwa na choka mbaya utaombwaombwa mpaka basi, alafu ndugu zako wakijua kama mtu wako masikini wanakuzarau kweli.
 
Back
Top Bottom