Nisaidieni mawazo, niko mpweke sana

Pole mpenzi, sote tunatendwa kwenye maisha...lakini tunassamehe na kuzidi kupenda na kutenda mema. Usiwaogope binadamu,yapaswa uwe karibu na watu walau wachache unaowaamini na kuwapenda. Inachosha akili na kuzeesha kuwa mpweke hivyo.ushauri wangu, tafuta marafiki wachache mnaoheshimiana na wanaompenda Mungu kama wewe,zungumza nao,shiriki kwenye activities kama lunch,dinner,movie au hata shopping na wao.Utajifunza mengi,utajiona mwenye thamani zaidi na wao pia wataona u rafiki mzuri. Mungu akutunze na akupe ushindi na akuondolee hofu zozote zile na zaidi akupe mwenza anayestahili mdada wa thamani yako.AMEN!


upo dadake na nanihii????????
 
pole sana dada, sijui hata nikushauri nini wakati huu, ila kila mtu na kipawa chake, sijui unashindwa nini kujichanganya na wenzio, upweke wa kazi gani? kama ulisoma vizuri, unao ma-class mates, una kazi na unahudhuria ibada kanisanai. mi naona matatizo yako makubwa ni mawili.

1. ulianza ngono kabla ya ndoa na ukakutana na wababaishaji wakakujerui saikolojia yako kiasi kwamba hadi umri huo hujapona
2. unataka mtu wa kwnu mchaga tu ndiye mwenye nafasi moyoni mwako

hofu yangu ni kuwa siku ukikutana na mchaga naye aakujeruhi, hali yako yaweza kuwa mbaya zaidi ya hii uliyopo kwani kumbuka wachaga nao ni wanadamu na si malaika

ushauri wangu ni kuwa wewe kubali matokeo na tubu uzinzi uliofanya kabla ya ndoa, mrudie Mungu wako kwa moyo wako wotw, wapende majirani zako na rafiki zako, shirikiana nao shughuli mbalimbali za kijamii kila upatapo nafasi, ukialikwa unaweza kwenda na ukakadiria muda mzuri wa kurudi nk.

pia usiwachukie wala kuwakimbia wanaume wanaokutaka mapenzi. ni kawaida wanaume kutongoza, kwa hiyo kazi ni kwako mwenyewe ku-manage the whole affair hadi ufikie lengo la kuolewa kama una lengo hilo maishani mwako. hapo ndipo pannapohitaji hekima kubwa, vinginevyo utadanganyika kuwa ili aendelee kuwa nawe ni lazima umvulie nguo na si wote hu-appreciate hatua hiyo na kuji-commit kufikia hatua ya ndoa, sasa the situation will be dictating the terms and Jesus guiding you all the way, if you trust the Lord, He will surround you and give you a sweet home in the time he has appointed since the beginning of the ages!

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!

stay blessed my dear
 
thanks miss Judy,sikuanza nikiwa mdogo ila ni kwli nilianguka dhambini naamini Mungu keshanisamehe,that is why i now get feared of them nisije tena kuanguka.asante kwa ushauri
 
wewe ni binti miaka 34??acha utani!!wewe ni mwanamke acha mambo ya ajabuuu

Binti ni mtoto wa kike, it doesn't matter her age. Kwa mfano an 80 years woman is still "binti" with only one exception: Anaemwita "binti" lazima awe na umri wa kutosha kuwa mzazi wa huyo 80-years old. Otherwise, ubinti hauna uhusiano na umri.

Back to the topic:

Sweetbaby, relationship inajengwa na watu wawili. Inawezekana wale watu uliokutana nao walikuwa kweli matapeli, ulianza nao uhusiano muda mrefu kiasi gani baada ya kufahamiana nao? Ulijaribu kiasi gani kuhakikisha uhusiano wenu unadumu? Nafurahi kusikia kuwa unakwenda kanisani, huna sababu ya kuwa mpweke. Mshirikishe Mungu katika mahusiano yako na utaona mabadiliko.
 
ya that is what i have decided ndo mana muda mwingi nimeopt kuwa peke yangu ingawa watu wengi wamenikosoa kwa hilo,asante kwa ushauri be bless
 
dada yangu hata kama hutaki mahusiano na wanaume kwa sasa,ni vizuri uwe na mahusiano ya kawaida na binadamu wengine,sio vizur kabisa kuwa mpweke,jichanganye na watu mnaoendana kitabia,social interaction ni muhimu kwa afya mwili na akili.
Mungu atakuongoza.
 
dada yangu hata kama hutaki mahusiano na wanaume kwa sasa,ni vizuri uwe na mahusiano ya kawaida na binadamu wengine,sio vizur kabisa kuwa mpweke,jichanganye na watu mnaoendana kitabia,social interaction ni muhimu kwa afya mwili na akili.
Mungu atakuongoza.

Hata hii ni nzuri!
 
Hivi mkristo mzuri ni yupi na kipimo kinachoweza nijulisha kama na mimi ni VERY au NOT attractive ni kipi???!Just wondering!!
 
To be honest, dada una social problems. Yaani baada ya wanaume 2 kukuumiza, umeamua kujifungia ndani na unataka mchaga kwakuwa waliopita hawakuwa wachaga!? Kesho utataka uwe na mnene kwakuwa waliopita walikuwa wembamba! Lazima ukubali kwamba hata ww una tatizo maana uhusiano wa watu 2 unapovunjika, kila mtu anakuwa amechangia kuvunjika kwa huo uhusiano, japo kwa kiwango tofauti. Ukishakubali kwamba una tatizo, huo ndio utakuwa mwanzo wa kuponywa maumivu uliyopata ktk mahusiano.

Ni kawaida ya binadamu kupenda kulaumu wengine mambo yake yanapoenda kombo (mfano wazazi, waalimu, marafiki n.k), lakini pia ni muhimu kujiangalia wenyewe mienendo yetu ili kujua kama inaathiri mahusiano na walio karibu yetu. Hebu kumbuka mambo mazuri uliyofanya ukiwa na hao ma-ex, usiangalie mabaya tu. "Every cloud has a silver lining".
 
:mod:

Pole sana binti/mwanamke kwa yote.Nahisi kuna makosa uliyofanya katika kuingia or uendeshaji wa mahusiano yote uliyoyataja hivyo kusababisha matokeo usiyoyatarajia.
Kwa maelezo yako inaonekana ni binti/mwanamke mwenye maadili mazuri hivyo ikakufanya uamini hukutakiwa kutendwa uliyotendwa,lakini nadhani mwanamume anachofuata kwa mwanamke si hayo tu,kuna mambo mengine ya ndani ambayo hayahitaji vigezo ulivyovitaja(sifa ulizoziainisha kuwa unazo).Mambo hayo yanataka uweke sala, mavazi,elimu,kazi/cheo n.k pembeni!Je,u mtundu chumbani?Shikamoo/nguo za kanisani/nguo za ofisini bedroom za nini? Je,u mbunifu chumbani?(simaanishi ubunifu wa mavazi).Mfano:Unga wa ngano unaweza leo ukapika maandazi,kesho chapati,kesho kutwa visheti,au mkate,pan cake,cake,kalmati and so forth.

Ushauri wangu;
1.Turn your WOUNDS into WISDOM
2.Rem,Change is NATURE of life...,but Challenge is AIM of life so you have to Challenge the Changes,and not to Change the Challenges...be blessed!
 
Nimejaribu kusoma posts zako zote, kama kweli wewe ni mdada na unayoyasema ni ya kweli, then you have a very serious problem. Unahitaji kuchukuwa maamuzi ya haraka sana kudeal na hili tatizo. Otherwise, uta-suffer depression kama bado. Halafu nani kakwambia wachaga sio matapeli? Kwa staili hii hata ukikutana na mchaga halafu akakutapleke, hali itakuwa even worse. Ushauri hapo unaposali kutakuwa na wapo wanaoweza kukusaidia kama padri or mchungaji kwa kukupa mwongozo mzuri au kuku-link na watu wengine wanaoweza kukusaidia. Una tatizo kubwa and you need to act now.
 
:mod:

EMT umenena vema,nakubaliana.Kwa nyongeza tu,nakushauri pia ondoa dhana kwamba you are perfect.Kila binadamu ana mapungufu yake nawe ukiwa miongoni mwa hao binadamu.I dont mean to make u inferior ila kubali mapugufu yako ili uweze kubadilika pale inapobidi.

Ulimwengu tunaoishi sasa hauna matabaka ya kikabila, kutokana na utandawazi,tabia hazina kabila ila ni personality ya mtu mmoja mmoja na kuna zile common habits zinazosababishwa na huo utandawazi ambazo hata huyo mchaga unayemtamani atakuwa nazo.

Hujachelewa sana,just be yourself,changanyika na watu,be confident with what you are doing,jenga marafiki wake kwa waume BUT with limitations.The right man is there and you will be surprised how you managed that.Naomba kujua interests/hobbies zako.
 
Pole sana binti kwa yote hayo,ila unaonekana una tatizo linakusumbua@1 ni kuchagua ainaflan ya watu hata kama ni mkwel kwako hukubalian nae kwan una kind yako unayoitaka.2 humchunguz mwanaume kabla ya kukubaliana nae.ushaul wangu ni kwamba ondoa dhana ya kuitaj aina flan ya mtu kwan mchagua nazi huishi kuchagua korona,pia usiefate ukabira na mwisho muombe mungu akupe mme bora.good day.
 
wee naniii bint ni yule mwenye bikira miaka 15-20,wewee hapo ni kibibi

Mtorii wacha kuzidi kumuumiza mwenzio, ameshakwambia ni mpweke sana, nadhani labda hajawai kuzaa, hana mume kwa hiyo bado anajihesabu ni binti, ninavyoona mimi wanawake wengi wakiwa hawajazaa au kuolewa huwa ni ngumu kujiita mwanamke au mama. Naona ulitaka aji-address kama mimi ni mwanamke au mimi ni mama mwenye umri wa miaka 34, sasa hayupo kwenye umama kwa sababu hajazaa na hayupo kwenye uanamke kwa sababu hajaolewa.

Nikiludi kwenye mada: Mpenzi jaribu tu kujichanganya hiyo ndo itakusaidia, maana hata ukisema ukae karibu na nyumbani bado ni bure, mwanzoni unaweza ukaona kwamba hapa sasa sawa, lakini kadri muda utakavyokuwa unazidi kwenda upweke utakuludia tu, kwa sababu umri huo kwa wanawake kama hajaolewa na hana mtoto anaona maisha yote ni bure, hata kama una pesa, gari, kazi nzuri, nyumba na unaweza kufanya chochote kile ukipendacho kama kutoka out na marafiki unajikuta tu hujisikii, maana huko utakuta wanawake/wasichana wenzie wapo na wapenzi wao wewe mmhhhhhhhhh!!!! utajihisi kumiss kitu flani na kitu flani ni mume au mtoto. Inauma kwa kweli ndo maana naona labda hutaki hata kutoka, ila mi nakushauri jichanganye na jipende zaidi wewe, jipe kipaumbele wewe mwenyewe hakuna mtu anayeweza kukupa raha katika dunia hii zaidi ya kujipa raha mwenyewe. Unaweza kufungasha vilago uludi kwenu ndo ukapata kisirani zaidi, maana utakuwa unaulizwa kila siku wewe mbona hutaki kuolewa au wewe mbona hauolewi, wakati wa kukuoa ndo hajajitokeza, hapo sasa ndo utatamani hata vile ulivyokuwa unaishi mpweke, maana hayo maswali yatakuwa yanakuchanganya zaidi. Pole mpenzi.
 
Mie siyo mchaga,ni mwiraq.nahisi walau kidogo tunaendana,ninaelimu ya kutosha,nina kazi nzuri yenye kunipa mshiko unaonitosheleza,usafir mzur na gari,nina miaka 34.thus why can't we join together and enjoy a life?why can't we make a family which can make us enjoy!welcom
 
mh! Stail hyo ya maisha dada na muda unazid kukupiga changa la macho na huna hata mtoto wa kusingiziwa mh? Kazi ipo unaweza ukawa umetupiwa jini mana hvyo tena mtoto wa kike bora mara mia angekuwa wakiume lakn wewe mh? Kaz pole we
 
sweety baby unaonekana ulikua umeji commity na ulitamani sana kuishi maisha matakatifa hasa kuwa na mahusiano masafi yaani ngono baada ya ndoa ya kanisani ila ukaanguka na unahisi kumess up kila kitu..kama ni hivyo upweke wako wa sasa hauna tatizo kwani Mungu anakuponya moyo wako na kukufundisha tena jinsi ya kuona ulimwengu..kwa sasa mfanye Mungu kuwa company yako ya karibu till u will be full equiped...the problem ni kwamba hukosubiri the right time kupokea mchumba ako kutoka juu..lakini I believe bado yupo na haujachelewa bado.all this are going to pass quickly very soon and yuo will be happy once again...shimboni!
 
The purpose of life is not crystal clear, especially when the path is sometimes paved with fear. Keep the faith, and trust God’s guidance. Pray for strength and courage to help cope with the struggles. BUT REMEMBER a beautiful future is waiting for you.
walk with aims.
Run with confidence.
Fly with your achievements.
You will have a lovely and bright future.Nice wkend
 
Back
Top Bottom