Niko kwenye wakati mgumu sana lkn NAMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko kwenye wakati mgumu sana lkn NAMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lonely heart, Jan 18, 2012.

 1. L

  Lonely heart Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habarini wapendwa, ndugu zng ninawakati mgumu sn, naumia sn moyoni ila yote namwachia MUNGU. Nina miaka 30 nimeolewa na nina mtoto 1, namshukuru MUNGU kwani toka tuoane MUNGU amekua akitupa rizk na mimi nilikua nafanya biashara na kwa mwezi napata faida laki 3-5 na mume wangu anapata mil. 5-4, km miaka 3 iliyopita nilipatwa na matatizo ya ujauzito kuharibika mara 3 mfululizo madaktari hawakujua chanzo ni nini wakanipa dawa na kunishauri nipunzike km mwaka 1 ndio nibebe mimba.

  Ilibi nimweleze mama mkwe wangu akaniambia hk kwao ni lazma itokee hvy, kweli nilikaa mwaka mzima na mwaka uliofuata nikajaribu kubeba mimba lkn ikashindikna, mama mkwe,mawifi + mumewng wakawa wananinyanyasa sn kw sizai, niliumia sn lkn nilzidisha maombi kwa MUNGU na mwaka jana nilipata ujauzito, kumweleza mume wng hakubu chcht nikaenda hos.

  Wakanipa bedrest na huu ni mwezi wa 4 mume wangu kaniambia waz kw hatatoa ht shiling ya hosp. Kila k2 nijihangaikie mwnyw,KWANIni ANISUSIE MIMBA NA NIFANYAJE mana imefika mahali natamani kurudi kwetu.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmh pole sana nitarudi baadae mi kiukweli ushauri wa wanandoa mimi huwa naona mgumu ila muombe tu mungu
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kwenu umefukuzwa?
  kwa nini uishi kwa mateso wakati umepewa bedrest?
  mwanaume mwenyewe hakujali usipojali afya yako na mwanao nani atakuhangaikia?
  hebu rudi kwenu ukapate uangalizi.

  mwisho pole sana kwa kuwa na mume wa aina hiyo, huyo mwanaume ni looser lisokua na huruma wala upendo
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hawa viumbe walizaliwa na baba mmoja!!! pole mpendwa
   
 5. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  pole dada, embu rudi home upumzike kwa muda, maana hapo waweza fanyiwa visa na io ikatoka.
  pia muweke huyo mumeo kwenye maombi.
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pole dada,kwenye maisha kunakua na mitihani ya kila aina hasa kwa wenye ndoa nadhani kwa sasa unahitaji mtu wa kukufariji na mtu wako wa karibu kwa sasa atakua mzazi wako sio mume tena,usijitie BP kwa kufikiri kwani unakiumbe tumboni na afya yake na yako ndio muhimu kwa sasa, najua kua inauma sana kwani huu ndio ulikua wakati muafaka kwa wewe kudeka kwa mumeo lakini usife moyo mwenyezi mungu yuko pamoja nawe..
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Aisee pole sana kwa hayo yote. Je kulikuwa na ugomvi wowote hapo kabla? Maana si hali ya kawaida mume kukataa/kususia mimba bila sababu yeyote ya Msingi. Yumkini anaweza kuwa kasikia fununu labda hiyo mimba si yake nk ndiyo maana kageuka kuwa hivyo.

  Nakushauri mkae kama familia kulizungumza hili na kulipatia ufumbuzi hususani ktk kipindi hiki ambacho umepewa bedrest which means hufanyi tena biashara na hauna kipato chochote zaidi ya kumtegemea mumeo.
  Pia muombe Mungu kwa kadiri uptavyo nafasi, ili shetani mbaya asiivuruge ndoa yenu.

  Pole na nakutakia mema, matatizo yako yaishe mapema.
   
 8. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Pole sana my dia ila kwa sasa mi nadhani ungezingatia zaidi hali yako na mtoto aliyetumboni maana kosa dogo laweza kukughalimu sana.

  Kama kunamahali unaweza kwenda kwa usalama wako na mtoto ni bora ukaenda maana huyo mumeo na ndugu zake hawakutakii mema na inawezekana wameshangaa kwa nini umeshika mimba wakati wao walitarajia vinginevyo.

  Nakuombea Mungu akulinde na mtoto wako na siku moja waje kukuomba msamaha kwa mabaya waliyokutendea.
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Huu mtiririko unanilazimisha kufikiri na wewe una matatizo.
  Kwa nini hutafuti masuluhisho ya haya?
  Utakuwa unamwendekeza
  Tizama sredi zako za zamani   
 10. isamilo1982

  isamilo1982 Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo ulipo una ujauzito tena umewekwa bed rest ukiongeza nahayo mastress kha!rudi kwenu haraka au mpaka mauti yakukutie hapo?
   
 11. M

  MUMY A JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 234
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua ukifanya mchezo utakua muuaji,kwasababu kama uko bed rest means huitaji kufanya shughuli ya aina yeyote wala hutakiwi kupata stress kabisaa....sasa wewe unaendelea kukaa hapo ili ukiondoe hicho kiumbe??????rudi kwenu utafia hapo oooohoo!!!
   
 12. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Mimi leo sikuonei huruma ng'oooo........
  Kila siku tunapoteza muda tu kutoa ushauri lakini mtu mwenyewe hata hueleweki. Subiri uumie zaidi ndo akili itajiseti!!
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  si vizuri Kipipi ujue....mshauri bwana.....
   
 14. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0

  I love her very much, ndo maana nikaamua kumwambia directly kabisaa....... pengine nikimuonea huruma saana nitamlemaza!!!
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nadhani hili jambo ni la kifamilia zaidi......................jitahidi pande mbili za familia zikutane.
   
 16. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nenda pale Ubungo tafuta basi linaloenda nyumbani kwenu kwa baba na mama yako panda basi hilo uende kwenu!
   
 17. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Ungemshirikisha kabla ya kubeba ujauzito,mtoto si wenu wote?? Muombe msamaha kama ndo kilichomkasirisha,mwambie imeshatokea unamuomba sasa akusaidie kwa hali na mali katika kumtunza huyo mtoto...Huko kwenu utarudi kimoja? wanawake hatu-give up kirahisi hivyo....ukiona huwezi ita washenga na watu wake wanaokupenda na kumheshimu yeye.
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha umegonga nyundo ya kichwa
   
 19. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  ili nini, mwanaume kama hakutaki rudi kwenu. Kujipendekeza kwa familia yake ni kujidhalilisha na zaidi ni mara chache sana ndugu wa mwanaume kuside na wewe, hasa pale mwanaume anapokuwa na pesa.

  Ndugu mleta mada, tafuta ndugu zako wakusaidie, kila mchuma janga hula na wa kwako.
   
 20. R

  Rubuye123 JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,443
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180

  dah bonge moja la quote,nilikuja elewa baadae sana nilipokua.mwanamke haikimbii ndoa yake kirahisi rahisi hivyo.umejaribu kila njia kweli na imeshindikana??
   
Loading...