Niko katika mgogoro mkali sana na mpenzi wangu kutokana na message aliyonitumia

Mjibu kila kitu hapana... Angalia atakavyo react... Halafu ni PM nikufahamishe nini cha kufanya after that...
 
Jamani hivi watu wengine wameumbwaje? mbona mambo madogo unacomplicate kiasi hicho!?kitu kidogo unakikuza kosa lake ni lipi?Kwani ungemjibu hayo maswali ungepungukiwa nini? Mwanaume hawi hivyo bana khaaaa!:flypig:
 
Siamini kama umekosa jibu kwa hayo maswali rahisi kama kweli unampenda.

Maskini binti wawatu kauliza maswali vizuri bila kukosea.

Ninge kuwa wewe na ninampenda huyo binti kama ulivyo sema kwa kila swali ninge jibu YES kwa lugha ya kigeni na NDIO kwa lugha yetu

Nina wasiwasi na upendo wako kwa huyo binti.
 
Sasa tatizo liko wapi hapo?? Mbona una complicate mambo madogo tuu hayo.. Kinachokufanya uchukie muda wote huo ni nini? Huwezi kusema majibu anayo..Wewe ndie mwenye majibu yote hayo.. Mjibu mpenzi wako hayo maswali maana najua hakukurupuka kukuuliza hayo..! Wanawake tunapenda kuhakikishiwa kila siku kama tunapendwa na tutaolewa.. Upo hapo???
"Mh!"
wanawake huwa mnakua tayari mna alternative,hivyo unataka uhakikishiwe ili uchague<wakati kwa mwanaume huwa anahitaji muda zaidi wa kuwa na uhakika na mtu atakemuoa.sasa huo mvutano ndio huwa unaleta shida.lakini nyie wanawake ni wakorofi kwasababu huwa mnalazimisha sana majibu hata kwa muda ambao sio muafaka.
 
"Mh!"
wanawake huwa mnakua tayari mna alternative,hivyo unataka uhakikishiwe ili uchague<wakati kwa mwanaume huwa anahitaji muda zaidi wa kuwa na uhakika na mtu atakemuoa.sasa huo mvutano ndio huwa unaleta shida.lakini nyie wanawake ni wakorofi kwasababu huwa mnalazimisha sana majibu hata kwa muda ambao sio muafaka.

Muda muafaka ni upi huo? Miezi 3. 6. mwaka1, maika 5 au? Sasa kama nimeshakaa na wewe mwaka mmoja unataka uhakika zaidi wa nini? Ambacho hatupendi ni kukaa na mtuu miaka inapita kumbe hana mpango na wewe.. Ndio maana tunauliza ili tupate uhakika.. Ili kama unasua sua nitafute ustaarabu mwingine before its too late.. !
 
Jamani hivi watu wengine wameumbwaje? mbona mambo madogo unacomplicate kiasi hicho!?kitu kidogo unakikuza kosa lake ni lipi?Kwani ungemjibu hayo maswali ungepungukiwa nini? Mwanaume hawi hivyo bana khaaaa!:flypig:

Na mimi naona kayakuza bila sababu ya msingi..just say YES man!!
 
Ongea na moyo wako kama kweli unampenda na unataka kumuoa mjibu tuu kuwa upo tayari kama huna mpango wa kumuoa ni vizuri umwambie mapema ili kama anabaki kuwa na wewe ajue kuwa hamtooana.
 
Ameamua kukueleza hata udhaifu alikuwa nayo huenda wewe hujui muulize vzr mwambie nashindwa kukujibu b'se cjajua umekusudia nn but take care.
 
Dada ameona muda unaenda na huna plan yeyote nae. Ukisema majibu yote yes, haitoshi kama umeamua kuwa ni mkeo umefanya mikakati gani mpaka sasa kuonyesha uko kwenye muelekeo wa huko. Mambo kama hayo lazima ufix date au atleast utoe approximation of time, hayaendi hivi hivi.

Maana kuna wanaume wengine usipowaweka on hot seat watakumega, kukuzalisha na wewe unasubiri tu commitment from him.

Rudi kaombe msamaha msonge mbele.
 
hayo maswali ni ya kawaida sana kati ya watu wapendanao! je, asipokuuliza hayo maswali hata siku moja utaona ni kawaida? Nakuomba umpigie simu ama umuite umjibu hayo maswali yake ana kwa ana na tena kwa hisia kali za upendo na mahaba (Onyo: hii uifanye kama kweli unampenda) nausichoke kumjibu hata kama alishawahi kukuuliza mara nyingi kipindi cha nyuma, usichoke hayo ni mapenzi kaka! je, kwani una umri gani? unampenda kweli? Be serious with her kama hupendi kuyajibu maswali haya mana yake huna malengo mazuri naye basi achana naye mara moja! If u do love her and intending to marry her, TELL HER THE ANSWERS SHE DESERVE!
 
Alikupigia simu kukuuliza hayo maswali, bahati nzuri ulikua umelela hujapokea. Ndo kaamua kukutumia msg juu ya yaleyale maswali ambayo angekuuliza kama ungepokea simu. So jibu maswali acha hofu. Wakati unamjibu wewe ndo ueleze hukupokea simu kwa sababu gani....
 
Three school of thoughts:

1. Anataka tu assurance ambacho ni kitu cha kawaida kabisa of which wewe inatakiwa umpe hityo assurance na kumwomba radhi huku ukimweleza hukupokea simu kwa kuwa umelala. Zungumza naye kama ana hisia ana mapungufu yeyote na hakikisha umeclear doubts zake zote.

2. Ameona unampiga dana dana kwa siku nyingi kuhusu maswali aliyokuuliza na sasa anataka assurance ili kama huna mpango naye asipote muda zaidi.

3. Kuna mtu amempata na anampenda kwa dhati, more likely kamkubali katika maeneo yote aliyokuuliza maswali. bado anakupa nafasi of which kama majibu yako ni negative anakutosa na kuanzisha mahusiano mapya possibly na ndo juu.
 
nimeona niombe ushauri wenu wa dhati kuhusu hili;
nina mpenzi wangu ambaye anajua nampenda sana nami vilevile nampenda sana.
kisa ni hiki kifuatacho:-
siku moja ndani ya mwezi wa june, mpenzi wangu alinipigia simu usiku na kwa bahati mbaya sikupokea simu yake kwa sababu nilikuwa nimelala hivyo baada ya muda mfupi akatuma sms iliyokuwa na maswali kibao na magumu ambayo sikuweza kupata majibu ya haraka haraka kama alivyotaka nimjibu na hili ndo limenipelekea kuomba ushauri toka kwenu. Message hiyo ilisomeka kama ifuatavyo:-
naomba unijibu kwa ufasaha kutoka moyoni mwako
  1. je uko tayari na umeridhika kuwa nami kama mkeo mtarajiwa?
  2. unanipenda kweli?
  3. uko tayari kunioa?
  4. haunidanganyi?
  5. umenipenda jinsi nilivyo pamoja na udhaifu nilio nao? Please naomba majibu
meseji hii ilileta shida na mpaka sasa tuko katika mgogoro mkali sana maana mimi nilireact kwa nini asiniulize nini kimesababisha nisipokee simu yake yeye akaniuliza maswali ambayo majibu yake anayo???
Nawaombeni mnisaidie ili tuondoe kutokuelewana tulikonako.

she is insecure
 
Usifanye inshu kuwa simple kiasi hicho kaka. Kama ndivyo kwa nini aniulize baada ya kunipigia sikupokea????

Using'ang'anie suala la kupigiwa bila kupokea! Naye anajua kuwa ilikuwa usiku kwa hiyo kutopokea sio ishu kwake kwa hiyo akaamua kutuma ujumbe wa maandishi. Labda kama kuna mambo mengine kati yenu tusiyojua sisi.
Halafu tambua kuwa uchumba ni dynamic, hata kama ulishamhakikishia upendo wako na nia yako ya kumuoa, kudai assurance mara kwa mara ni sahihi na sio usumbufu kwako. Kwa hiyo jibu swali lolote analouliza bila kujali ni mara ya ngapi anauliza. Ukishindwa mtihani huu mdogo basi hauko tayari kwa ndoa.
 
Kama kawaida ya wanawake...huyo anachotafuta ni kudanganywa...kwani ukimjibu ndio wala si garantiii kuwa ni kweli utamuoa.

Nimekusifu sana kwa kusita unlike wanaume wengi wenye wepesi wa kuwapa wasichana wao matumaini yasiyokuwepo.

Hivi msichana yeyote akiwa na relationship lazima hiyo relashionship iishie kwenye ndoa? Tukiongea na fact..ni ngapi zinaishia kwenye ndoa? Kwa nini tunalazimisha hawa watu waseme uongo?

Mwanaume anaweza asiseme kuwa ana mpango wa kukuoa hasa katika kipindi cha mwanzo cha uhusiano wenu...lakini baadae akaona anahitaji kuwa na mke na wewe ndie chaguo lake. Haina maana kuwa hakupendi ila hana mpango wa kuoa in the near future; au kwa maneno mengine hajafikiria kuoa. Na by the time anataka kuoa who knows kama bado mtakuwa wapenzi?
 
Kwani mkuu hapo kuna swali lisilojibika au unampotezea muda huyo
binti usilete maneno mengi toa majibu mambo yaishe.
 
Back
Top Bottom