Niko katika mgogoro mkali sana na mpenzi wangu kutokana na message aliyonitumia

BUCHANAGANDE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,513
474
Nimeona niombe Ushauri wenu wa dhati kuhusu hili;
Nina Mpenzi wangu ambaye anajua nampenda sana nami vilevile nampenda sana.
Kisa ni Hiki kifuatacho:-
Siku moja ndani ya Mwezi wa June, Mpenzi wangu alinipigia simu usiku na kwa bahati mbaya sikupokea simu yake kwa sababu nilikuwa nimelala hivyo baada ya muda mfupi akatuma sms iliyokuwa na maswali kibao na magumu ambayo sikuweza kupata majibu ya haraka haraka kama alivyotaka nimjibu na hili ndo limenipelekea kuomba ushauri toka kwenu. Message hiyo ilisomeka kama ifuatavyo:-
Naomba unijibu kwa ufasaha kutoka moyoni mwako
  1. Je uko tayari na umeridhika kuwa nami kama mkeo Mtarajiwa?
  2. Unanipenda kweli?
  3. Uko tayari kunioa?
  4. Haunidanganyi?
  5. Umenipenda jinsi nilivyo pamoja na udhaifu nilio nao? Please naomba majibu
Meseji hii ilileta shida na mpaka sasa tuko katika mgogoro mkali sana maana mimi nilireact kwa Nini asiniulize nini kimesababisha nisipokee simu yake yeye akaniuliza maswali ambayo majibu yake anayo???
Nawaombeni mnisaidie ili tuondoe kutokuelewana tulikonako.
 
Sasa tatizo liko wapi hapo?? Mbona una complicate mambo madogo tuu hayo.. Kinachokufanya uchukie muda wote huo ni nini? Huwezi kusema majibu anayo..Wewe ndie mwenye majibu yote hayo.. Mjibu mpenzi wako hayo maswali maana najua hakukurupuka kukuuliza hayo..! Wanawake tunapenda kuhakikishiwa kila siku kama tunapendwa na tutaolewa.. Upo hapo???
 
wanawake tunapenda kusikia neno 'nakupenda' na sifa nyingi juu yetu. yanatufanya tujiamini, mjibu tu kaka mmalize ugomvi
 
sasa mpaka unakuja hapa jf

ulishindwa tu kusema
'nisamehe yaishe'
i am nothin without you
nimekosa yaishe'

halafu unge concentrate na vitu viingine by now

wewe umebaki kuja jf na kichwa chako still in a mess
 
kuna tatizo hapo?
Si umwambie tu.

Kuambia kutoka mdomoni mwa shetani ni zaidi huliko kuhisi.
 
mbona majibu yake yapo simple sana hayaitaji kudesa!!!
 
Usifanye inshu kuwa simple kiasi hicho kaka. Kama ndivyo kwa nini aniulize baada ya kunipigia sikupokea????
 
dah ndugu yangu sema ukweli, na kuwa wazi na ujiulize maswali haya.!! 1 furaha yako ni ipi...?? 2 pili nini unahitaji????

kama furaha yako ni huyo mpenzi wako nilazima uipiganie kwa nguvu zote.

na kama moyo wako unamuhita hayo maswali umjibu halaka muhim ujuwe unataka nini.
 
Jambo rahisi sana hilo kaka.

MAJIBU:
1. NDIO
2. NDIO
3. NDIO
4. NDIO
5. Inategemea na aina ya mapungufu, mapungufu mengine lazima ujirekebishe ili tuish kwa amani kila mmoja. kama hi meseji sijaipenda hivyo jirekebishe siku nyingne ukiona simu haipokelewi usikurupuke kulalamika ITAKUCOST

Simple & clear
 
Hakuamini, Wewe unareact nini sasa? Yani mie Wala nisingeijibu n tungekuwa Poa tu.

UOTE=BUCHANAGANDE;4281148]Nimeona niombe Ushauri wenu wa dhati kuhusu hili;
Nina Mpenzi wangu ambaye anajua nampenda sana nami vilevile nampenda sana.
Kisa ni Hiki kifuatacho:-
Siku moja ndani ya Mwezi wa June, Mpenzi wangu alinipigia simu usiku na kwa bahati mbaya sikupokea simu yake kwa sababu nilikuwa nimelala hivyo baada ya muda mfupi akatuma sms iliyokuwa na maswali kibao na magumu ambayo sikuweza kupata majibu ya haraka haraka kama alivyotaka nimjibu na hili ndo limenipelekea kuomba ushauri toka kwenu. Message hiyo ilisomeka kama ifuatavyo:-
Naomba unijibu kwa ufasaha kutoka moyoni mwako
  1. Je uko tayari na umeridhika kuwa nami kama mkeo Mtarajiwa?
  2. Unanipenda kweli?
  3. Uko tayari kunioa?
  4. Haunidanganyi?
  5. Umenipenda jinsi nilivyo pamoja na udhaifu nilio nao? Please naomba majibu
Meseji hii ilileta shida na mpaka sasa tuko katika mgogoro mkali sana maana mimi nilireact kwa Nini asiniulize nini kimesababisha nisipokee simu yake yeye akaniuliza maswali ambayo majibu yake anayo???
Nawaombeni mnisaidie ili tuondoe kutokuelewana tulikonako.[/QUOTE]
 
Moyo wako ni mwepesi sana,katatizo kadogo umeshakafungulia thread?Wewe kuna watu tunashida na wapenzi wetu tukibandika hapa "pole na like" zitaongozana.

Ukiyachekea mapenzi nayo yatakucheka pia.

Stuka!
 
Kwanza hakuna ugomvi hapo. Yaani huyo dada mstaraabu sana, anakupenda na anakuheshimu. Alipanga akupigie simu akuulize, bahati hukupokea akaamua atume messeji. Sijaona kama kuna mahali amekutuhumu kwa nini hujapokea simu. Ila mkioana huyo dada atapata shida, maana itakuwa ugomvi kidogo panga mkononi.
 
Message yake mbona imetulia tu. Mtoto anataka uhakika kama uko serious naye au unamega tu kisela kisha utasepa jumla.
Unajua mademu huwa wanaendelea kutokewa, hivyo anataka kujua kama haumpotezei muda kwani anawatosa wengine kwa ajili yako.
Jibu ukweli wako. Kama unampenda na unataka kumuoa basi jibu la kila swali ni NDIO.
Udhaifu wake ww ndio unaujua.
Hakuna mgogoro hapo jombaa...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom