Niko busy, msaada!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,636
Habarini, Nataka kujua neno hili linatamkwa vipi kwa kiswahili?
 
nina shughuli nyingi....

nimebanwa na shughuli.....

nimebanwa na mambo...

mambo yamenizonga...
 
Niko busy mpaka hapo umesema kiswahili, nenda kwenye kamusi ya kingereza - kiswahili halafu tafuta neno busy utapata maana yake kisha itangulize niko - maana ya busy. Umenipata aiseeee.
 
Habarini, Nataka kujua neno hili linatamkwa vipi kwa kiswahili?

Umeuliza "linatamkwaje", na sio lina maana gani.
Matamshi yake ("pronunciation") kama utalitamka kwa kiswahili japo litabaki limeandikwa kwa kiingereza litakuwa "bizi".

Ila: maana yake (translation) kwa kiswahili ni "kutingwa na shughuli".

Kwa hiyo:

I am busy=Nimetingwa na shughuli
I am very busy=Nimetingwa sana na shughuli.

Asante.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom