Nikiwatimua kwa kuniambia 'dhaifu' mtalalamika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikiwatimua kwa kuniambia 'dhaifu' mtalalamika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Jun 21, 2012.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nikiwatimua kwa kuniambia dhaifu mtalalamika?

  Mwandishi:Charles Misango

  alhamis, 21 juni 2012


  JUMANNE wiki hii, Watanzania waliokuwa wakifuatilia mkutano wa Bunge, walishuhudia Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) akitimuliwa bungeni kwa amri ya Naibu Spika, Job Ndugai.

  Kilichomponza Mnyika ni kukataa kwake kufuta kauli yake ya "kudai" kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu.
  Sitaki kujikomba kwa msomaji yeyote, kwa kuweka wazi kuwa binafsi, nakubaliana na maamuzi ya naibu spika kwa sababu mbili; mosi, ni kwamba alichofanya ni kutekeleza kanuni za Bunge.

  Mnyika alikataa kufuta kauli hiyo na kanuni zinasema kwa tendo hilo apaswa kupewa adhabu ya kutolewa bungeni.

  Pili, Ndugai pamoja na kushambuliwa kwa madai ya kutumia vibaya kiti chake, bado hakutoa adhabu ninayoamini ni nzito kabisa ya kumzuia Mnyika asihudhurie vikao vitatu vya Bunge, badala yake akatumia kifungu cha pili kinachomzuia mbunge aliyekataa kufuta kauli yake ya ‘kuudhi' kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa muda wote wa kikao cha siku hiyo hadi kesho yake.

  Pamoja na adhabu hiyo, Ndugai pia ameniudhi! Tena namtafutia nafasi naye nimpe adhabu yake. Ndugai anajua kuwa, ni mwiko kabisa kwa mtu hata kama ana hadhi kiasi gani kutudhalilisha sisi viongozi tuliopewa dhamana kubwa na mamilioni ya Watanzania wanaotupenda na kukipenda chama chake cha dole juu, hadharani na mchana kweupe.

  Unashangaa nini na wewe msomaji? Ujasiri wa kutudhalilisha wenye nchi yetu nani kawapa? Hakuna heshima? Hamjui kuwa anayevaa khanga ya mama ndiye baba hata kama humpendi kwa sura iliyopondeka kama kitako cha sufuria?

  Kama huyo huwezi kumtolea maneno ya kumuudhi, ukijua kwa kufanya hivyo, utamchefua mama, sembuse sisi viongozi wa nchi tuliyopewa ridhaa ya uongozi kwa ushindi wa kishindo?
  Hivi nani kawaambia sisi tu wadhaifu? Katika lipi? Maana kuna watu wamediriki kuinua midomo yao na kutushambulia kuwa eti tumeshindwa kuwaletea maendeleo. Wanadai tumeruhusu wawekezaji waje kupora rasilimali zetu. Maudhi hayo!

  Ngoja niwaleze tu namna gani tulivyojitahidi kuinua jina la Tanzania katika sekta ya madini, ingawa mnatuudhi kwa kutuambia kuwa tumeshindwa kuwadhibiti wachimbaji wa madini, ambao mnadai ni waporaji. Tena mshindwe na mlegee! Nani kawapa weredi wa kujali mambo haya mazito, wakati kwa hulka zenu watanzania ni watu msiojali? Mnaoshabikia mambo ya Simba na Yanga, na kubobea tu katika kuchangishana michango ya viharusi badala ya harusi, "siendi kwa hofu', na ‘twisheni pati" (potelea mbali hata kama nakosea majina yake).

  Ngoja niwapake wote mnaotusakama; ninyi wavivu wa kufanya kazi na mabingwa wa maneno ya kuuudhi! Nani kawaleta wawekezaji bora katika sekta ya madini? Ninyi ama sisi viongozi wenu?
  "Mnasema eti sekta ya madini imeshindwa kunufaisha nchi hii. Nani kasema? Hivi hamjui kuwa kutokana na uhodari wetu, tumeuwezesha mgodi wa Geita gold mine kuwa mkubwa kuliko yote hapa nchini, na wa tatu Afrika."

  Hivi nani hajui kuwa tangu mwaka 1998, nchi yetu imekuwa mzalishaji mkubwa wa soko la dhahabu dunia na namba tatu kwa Afrika tukitanguliwa na Afrika Kusini na Ghana? Hamuoni kama tumelitangaza jina la Tanzania duniani na kujulikana? Hamjui kujulikana ni sifa? Halafu mnasema uongozi wetu ni dhaifu; Mnaudhi! Chama chetu oyeee!

  Mnalalamika kuwa kampuni hizi zinamiliki ardhi kubwa ya machimbo ya madini, na zimekuwa zikitumia leseni za utafiti vibaya kwa kuchimba madini kwa miaka kadhaa na kisha kubadilisha majina, ama kuziuza kampuni hizi kwa makampuni mengine, hatua ambayo mnadai eti inatumika kukwepa kodi. Hayo nayo ni maneno ya kuudhi!

  Kama mtu kashindwa biashara kwa nini asimuuzie mwingine? Na alipe kodi gani wakati kwa miaka mitano alikuwa anafanya utafiti?

  Eti nimesikia watu wakitoa mfano wa jinsi Kampuni ya Ashanti Goldfields Company Ltd ilipoinunua Kampuni Samax Gold Inc mwaka 1998 hivyo na kupata faida katika mradi wa Golden Pride.
  Eti Kampuni ya Barrick ndiyo inayoongoza kwa kupewa leseni nyingi za utafiti wa madini pamoja na uchimbaji hapa Tanzania.

  Sasa ulitaka apewe mjomba wenu ambaye ni miongoni mwa waliofilisi mashirika ya umma miaka ileee? Si bora tumpe mzungu kuliko Mswahili wa kibaingwa? Acheni kudhihaki wenzenu. Mnacheza na wazungu ninyi!

  Unadhani sisi viongozi ni wajinga kwa kuipa Barick leseni nyingi za utafiti na uchimbaji? Tunajua uwezo wake. Ona inaendesha moja kwa moja migodi ya madini ya Bulyanhulu ulioko Kakola wilayani Kahama, Mgodi wa North Mara wenye leseni mbili za SML 18/96 kwa eneo la Nyabirama na SML 17/96 eneo la Nyabigena wilayani Tarime mkoani Mara na ule wa Tulawaka SML 157/03 ulioko wilayani Bihalamuro mkoani Kagera.

  Kwa hatua hizi pia mtatuita sisi dhaifu kisa tu, mnaona kwa akili zenu hawajatoa kodi kadri mnavyotaka? Tukiwapeni ninyi mtaweza kama hamtaishia kutambiana kwa mikogo ya wingi wa magari ya kifahari na kushindana kubadilisha ‘totozi' kila siku?

  Mwandishi:Charles Misango
  Mytake:
  Mbona kama simwelewi huyu mwandishi vizuri,wewe umemuelewaje?

   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumwelewa mwandishi wa kutumia fasihi ni ngumu sana
   
 3. N

  Nsomba Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alichoandika ni bora alichosema Mnyika, maana angalau Mnyika alitumia lugha nyepesi. Huyu mwandishi katwanga kavu kavu, ila kwa wenye akili kama za mtu wa Bagamoyo anaweza asiupate ujumbe uliokusudiwa.
   
 4. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Alalaye usimuamshe ukimuamsha utalala wewe
   
 5. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama mtu alitaka kukupiga ngumi ya uso ukachelewa
  kukwepa likatinga kwenye uso jumla basi hii ndio ngumi
  ya uso aliyochapwa Rais badala ya ngumi aliyomchapa
  JJ Mnyika bungeni.Hili ni konde maridadi

  Kuna waandishi wachache sana nawaamini uandishi wao.
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tupa kule linafaa kwenda kwenye bin for other use
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naona mwandishi ameamua kuthibitisha udhaifu wa Kikwete ambao Mnyika aliusema. Lakini amesahau madhaifu mengine kama ya ndege ya kijeshi ya nchi nyingine kutua nchini na kubeba wanyama na kuondoka pasipo Rais kujua. Hicho kibali cha ndege ya kijeshi ya nchi nyingine kuingia nchi nyingine kilitoka wapi? Huu ni udhaifu uliopindukia ambao kwa hakika kama watanzania wangekuwa ni watu wenye akili timamu basi rais alitakiwa awe ameshajiuzulu. Sasa bunge lenyewe ndiyo hilo la akina Mwigulu, upinzani nao wapo busy na kukusanya wanachama, wakati hili lilikuwa liwe ni bingo kwa upinzani kumlazimisha Rais ajiuzulu. Ni vile tu sina pa kusemea, na sina pesa ya kutosha, otherwise, ningevichochea vyombo vya habari viikomalie hii ishu hadi kieleweke.
   
 8. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,143
  Likes Received: 10,498
  Trophy Points: 280
  Ritz na wenzake wakifungua hii thread mimate itawadindoka wakidhani kunamfuasi wa Nape kaongezeka.. kumbe.

  Mwandishi naona kaongeza Petroli kwenye blazing fire ya Mnyika.
   
 9. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukiona hawachangii huu uzi basi ujue wameelewa mwandishi alimaanisha adhabu aliyompa naibu spika ndugai
   
 10. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yes,kelele zimeanza,wameshaanza kuelewa kilichoandikwa!!
  taratibu tutaeleweshana.
   
 11. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwandishi anamuunga Mkono Mnyika kwa 100% . Hamjampinaga hata kidogo! Anabeza CCM vilivyo!!Simply ni Mwoga!! You don't need to do all the meanders in the bush, to Confront a Person or his party!!
   
 12. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  inabidi tuanzishe mkakati maalum wakuoji ujio wa ndege hii huu ni uvamizi kunasiku tutatumiwa kombora.
   
 13. MANI

  MANI Platinum Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu fasihi ni ngumu kuilewa inabidi utulie ndio utailewa na kuchangia.
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu asiyeelewa hapa anajua kuwa jamaa kamponda Mhe Mnyika ila kwa wanafasihi wanajua kuwa ujumbe umefika
   
 15. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  JAPO UDHAIFU SI TUSI ila "USIMSEME VIBAYA KIONGOZI WA WATU WAKO MBELE YA ANAOWAONGOZA" ailwahi kusema sulemani katika mithali ya BIBLIA TAKATIFU
   
 16. B

  Bob G JF Bronze Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi JJ Mnyika ulijua kuwa ukisema JK ni dhaifu utakuwa umetoa changamoto kubwa kwa watanzania kujadili uwezo mdogo alionao rais na chama chake, Hivi ulijua kuwa ndo unakimaliza ccm, Ulijua utaamsha watu na kuijadili ccm na Udhaifu wake?
  Hivi ulijua kwamba watu wengi wanajua udhaifu wa rais na kwamba waliogopa kusema hadharani, Hivi ulijua kuwa unaivua unguo zinazo nuka serikali ya ccm?, JJ Mnyika Umewaamusha wengi Big Up
   
 17. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni kweli JJ alifanya kosa kikanuni,lakini ukweli kuwa JK ni dhaifu ni ukweli mchungu,na naona mwandishi amepulizia machungwa kwenye pua ya mpiga chafya!!
   
 18. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280

  Mimi binafsi nimemuelewa vizuri sana mwandishi. Huyu ni bingwa wa uandika Fasihi na misemo yake.

  Ni dhahiri hapa kuonyesha Kikwete na Serikali yake ni Dhaifu hakuna kubisha.

  Mambo yote wanayoringia kuyafanya hayana manufaa kwa Mtanzania bali kwa wawekezaji na viongozi mafisadi.

  Hongera sana mwandishi.  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...