Nikiwaambia msioe muwe mnasikia; kwa miezi 4 mwamba kaishi maisha magumu bila mshahara kumbe mkewe ana laki 8 ndani, na usaliti juu kaambulia

SI Bora hiyo ... Nikiwa form three babaangu alipatia ajali na wakaiba mzigo wote ilikuwa ni magodoro, tajiri akamalizana na bima, mzee akafukuzwa kazi akarud maskan... Dingi alikuwa anakabalance kidgo hashindwi kuacha 5000 kwa siku unga upo mchele tunachota tu, akaanza kuishiwa Zaid anashinda road Mara madereva wenzie wanamtunza Mara deiwaka, Mara Kodi maskan, kadiri muda ulivoenda nlimuona baba akichoka Zaid , akaacha kwenda road tukawa tun
Storee nzuri ila mwandiko wa kingese asee
 
Eeeh bwana ehh ni Mimi Mr. Liverpool Tena.

Weekend hii tumempiga Manure na nyundo Kali sanaa mpaka kapoteana.!!
Sasa jiulize ile ilikua Old Traford, je wakija Anfield..!!!
Vijana mnashida sana, kwa hiyo matatizo ya John una Generalize kuwa ndoa ni mbaya ahaaa come on, huu ni ujinga uliopitiliza, Kwa hiyo umesikiliza upande mmoja ukajanna story zako za kimbea hapa.

Kwa maelezo yako ingawa yamekaa kipaahukuna sana sana, John naye ni Tatizo, hivi kwa akili yako Ukinunua gari then ukakuta hiyo gari ni mbovu utailaumu gari au wewe uchaguzi wako?
 
Tunapaswa tumsikilize nani kati ya MUNGU na wewe mleta mada Liverpool VPN ???

Mwasisi wa taasisi ya ndoa ni MUNGU. Ikiwa wanadamu wote wake kwa waume tukidumu katika UTIIFU wa Amri za MUNGU hayo matatizo ya kwenye ndoa hayatakuwepo.

Sasa wewe unapowaambia watu wasioe maana yake unawashawishi watu wavunje Amri za MUNGU kwa kushiriki zinaa.

Yeyote anayezivunja Amri za MUNGU atakutana na adhabu kali sana. Itakufaidia nini kuishi maisha ya zinaa halafu baada ya maisha haya ukaishia kwenye adhabu kali na mateso?????

Mwenye masikio na asikie!!!!!
 
Tatizo wanawake ni watu wachoyo sana, walafi mno, wana tamaa sana, roho mbaya, wana chuki, wabinafsi, watu wenye mashindano, wasiotulia, wachawi, wasiowafikiria wengine Na ndoa ni biashara kwao
Salute,wanawake wapumbavu sana halafu wanajihisi wanapower sana pale wanaume tunapowaambia sorry.

#No woman No cry.
 
Naona Mr. Livapuli anazidi kujipatia tu wafuasi yaan anasepa na kijiji cha JF kila day
 
Vijana mnashida sana, kwa hiyo matatizo ya John una Generalize kuwa ndoa ni mbaya ahaaa come on,
Braza kwamba ndoa zenye matatizo ndio hii ya kwanza kwako kuisikia?

huu ni ujinga uliopitiliza, Kwa hiyo umesikiliza upande mmoja ukajanna story zako za kimbea hapa.
Ngoja nikushauri jambo.

Siku zotee unapo toa hoja usiwe una "attack" mtoa mada, hebu jaribu kutoa hoja bila aina yoyote ya abuse "Kwani ungeandika bila kutumia neno umbea" UNADHANI USINGEELEWEKA?
Kwa maelezo yako ingawa yamekaa kipaahukuna sana sana,
By referring nilicho andika hapo juu; kama unahisi huna cha kuongea/kuandika na hoja ukubaliani nazo basi JUST AGREE TO DISAGREE basi.

Ila kutoa maneno ya abuse na kum attack mtoa mada SIO ISHU.

Just toa hoja yako ipingwe na hoja ila sio abuse.

John naye ni Tatizo, hivi kwa akili yako Ukinunua gari then ukakuta hiyo gari ni mbovu utailaumu gari au wewe uchaguzi wako?
Binadamu wanakawaida ya kuficha makucha yao ili wasijulikane tabia zao.

#YNWA
 
Braza kwamba ndoa zenye matatizo ndio hii ya kwanza kwako kuisikia?


Ngoja nikushauri jambo.

Siku zotee unapo toa hoja usiwe una "attack" mtoa mada, hebu jaribu kutoa hoja bila aina yoyote ya abuse "Kwani ungeandika bila kutumia neno umbea" UNADHANI USINGEELEWEKA?

By referring nilicho andika hapo juu; kama unahisi huna cha kuongea/kuandika na hoja ukubaliani nazo basi JUST AGREE TO DISAGREE basi.

Ila kutoa maneno ya abuse na kum attack mtoa mada SIO ISHU.

Just toa hoja yako ipingwe na hoja ila sio abuse.


Binadamu wanakawaida ya kuficha makucha yao ili wasijulikane tabia zao.

#YNWA
Nimekuelewa asante kwa kunishairi kiungwana, nitalifanyia kazi sorry kwa kukukwaza ndugu.
 
Shetani ana watu wangi sana wa kukampenia ili watu wazidi kumwasi MUNGU. Siku zote shetani hapendi watu waishi kufuata mapezi ya MUNGU, kwani ndoa ni mpango wa MUNGU ili watu waache zinaa,kwani imemebeba laana.

Kwa kuwa shetani sio Omni-Present amefanikiwa kupata wafuasi wengi katika kufanya na kukampenia dhambi kwa wengine ndo mana dhambi inaonenaka kama fahari na sifa hasa kwa sisi vijana,watu wapo tayari kujisifia uzinzi na ulevi lakini si ustaarabu na hekima.

Pia usikute hizo ndoa au mahusiano mnayoyaleta humu si tu kwa mapenzi ya MUNGU bali kwa show-off, kutimiza mitazamo ya ndugu na marafiki na umri.

ONYO: Usishabikie usichokijua, na usiwe mwana kampeni wa shetani acha mipango na mapenzi ya MUNGU yawe kwa wamchao.NDOA na iheshimiwe na watu wote.

Kila kazi itapimwa kwa moto kwa sababu MUNGU wetu ni moto ulao.. (Ebrania12:29)
MKE NI ADUI UNAYEMMUDU ukioa usiyemmudu hilo ni TATIZO LINGINE.
 
Eeeh bwana ehh ni Mimi Mr. Liverpool Tena.

Weekend hii tumempiga Manure na nyundo Kali sanaa mpaka kapoteana.!!
Sasa jiulize ile ilikua Old Traford, je wakija Anfield..!!!

Turudi kwenye mada ....

HIVI KWANINI HAMSIKII NIKIWAAMBIA MSIOE ??

Sasa Kuna mwenzenu yamemkuta huku ......

Nimemsikitikia sanaaa "Hiii BAGOSHAAAA" (in jiwe's voice)

Mr. Liverpool ni mfanyakazi na mkuu wa idara fulani katika moja ya Halmashauri nchini.

Ana rafiki yake nae ni mkuu wa Idara (kaimu) nyengine (tumuite John).

John kuna jambo alizingua mwezi wa 2 akapigwa SP (Due to Absentees - alisepa kazini wiki bila ruhusa Wala taarifa na aliondoka kiboya hasaa).

John aliishia miezi 4 bila mshahara (akipambana na nisamehe na kumbembeleza HR mpaka wakafungua mshahara, waliufungua mwezi wa 6).

Jana nikaona nipige na John story; "Alitoboa vipi maisha miezi 4 bila MSHAHARA" Tuliongea mambo mengii ila Kuna jambo kanisikitisha sanaaa.

Anasema ........

Kipindi hana mshahara ndio aliijua rangi halisi ya mkewe..!!
Kaishi na mkewe miaka 5 ila hakujua huyu mkewe yuko hivi..!!

Mwezi wa 4 ndio ulikua mwezi mgumu. Hali ilikua ngumu japo kwa nje hakuonyesha.

Alivyoona mambo magumu hasa ilibidi amshirikishe mkewe. Alimueleza kila kitu mkewe japo mkewe ana duka la mahitaji ya nyumbani ambalo alifunguliwa na John ila alimjibu hana kitu.

(John alioa mama wa nyumbani ila aliamua kumfungulia duka ili asiwe wa nyumbani kabisa..!!!)

Ikabidi John anyamaze tu "mtu gani kwenye biashara miaka miwili apati faidi ye kila siku anatangaza hasara?"
John alijiuliza mengi akaona anyamaze alale.

Maisha yalikua taiti, John alikosa hela ya bia na ya manhood (kulinda wallet).
Ye alikua ana hakikisha tu mwanae mmoja wa ndoa anakula na kufurahi.

Kumbe bana John alikua anapitia mengi kwa siri sanaa na hata kula alikua anakula mgahawa wa mbali ili tusimuone yule mzoea makuku ana kula maharage..!!!

Aliogopa aibu na maneno ya walimwengu.

Kuna siku hali ya ugumu ndio ilizidi alirudi home empty (kazini hakupata dili wala kaposho cha kikao).
Kukopa hataki (atalipa nini na hana mshahara?).

Kufika home akamshirikisha mkewe, mkewe akatoa jibu lile lile SINA HELA..!!!

Asubuhi ya siku ifuatayo ilifika aliwazaa akaona leo haendi kazini. Alimwacha mkewe aende dukani, John aliamua kufanya searching nyumba nzima.

Alikuta vifuatavyo:-

1. Kwenye begi la nguo lilikua limechanwa chini.
Alijiuliza begi jipya kuchanika..!! akakuta mule kwenye mchano Kuna vidonge vya uzazi na laki 3 kamili..!!!

2. Akainua godoro, kwa mwisho kwenye kono ya godoro akakuta kuna laki 5.

Akafanya searching kubwaa sanaa kwenye chumba chao cha kulala. Anakwambia alivyovigundua vilimfanya apate hasira hasaa.

Alitoka kwa hasira mpaka dukani kwa mkewe. Akamkuta mkewe anahudumia mteja, kuangalia simu akakuta haijajifunga (mkewe alikua akiangalia kitu YouTube)

John alizuga pale dukani akaiba ile simu akaenda kujificha ili aifanyie upekuzi.

Alivyoviona ........

1. Kumbe mkewe ana bwana ambae alikuaga mwanafunzi mwenzake chuo.

2. Na kwa kusoma sms, inaonyesha huyo jamaa ni X wa mke, na jamaa kapata Kazi mkoa huu huu tuliopo.

3. Mke wa John alimlipia jamaa kodi ya kuanzia maisha kazini na godoro alimnunulia.

3. Mke wa John anavyosemaga anaenda mjini kujumua vitu vya dukani huwa anashukia kwa mwamba ambacho ni chumba cha mke wa John na X..!!

4. Kwenye chatting ya WhatsApp inaonyesha X alimshauri mke wa John waache kutumia P2 ila mke awe anakula vidonge vya majira..!!!

Yaani John Ali screenshot kila chatting akajitumia WhatsApp.
Kwa kuonyesha ukatili hakufuta zile picha ili mkewe ajue kwamba John amejua.

Sasa haya yametokea Kati ya mwezi wa 4 mpaka wa 6.
John anasema anahitaji kuvunja ndoa.

Mke kuona John haitaki tena ndoa kakimbilia kanisani.
Mchungaji alimuita John, John alijibu "Mumewe huyo ni Michael (X)"

Mke akakimbilia kwa wazazi aombewe msamaha.
Wazazi wa mume na mke wamekaa, ila John anasema aliomba ili aelewe cha mtu basi yafanyike mazungumzo mengine na kwenye hayo mazungumzo Michael (X) awepo.

Ila Michael aligoma kabisaa kutimba kwenye usuluhishi na kwa taarifa ya mke pale alipokua anaishi Michael kahama na hajui kahamia wapi na namba za simu hazipatikani tena...!!!

John aligoma kumsikiliza yoyotee kwahiyo wazazi walisepa bila maelewano.

Nilichoshangaa sasa, anasema... Hajawahi kuongea na mtu juu ya hili ila Mimi kumuuliza mambo ya ku survive bila mshahara ndio kumemfanya animwagie yotee kama kushusha mzigo wa fikra..!!!

John haitaki tena ndoa na mpaka tunavyoongea hapa kasha file kesi ya talaka.

Kwake hajafika tokea mwezi wa 6 na nyumba haitaki tena.

John huenda kumchukua mwanae shule akitoka siku za Ijumaa huenda nae gheto lake jipya huku akimtaarifu mkewe "mtoto yupo kwangu".

Mshahara ulivyofunguliwa John kumbe kapanga chumba karibu kabisa na kwangu..!!

Kanunua vitu vichache vya kuanzia maisha.
Kaamua kumuachia mkewe nyumba tu aishi na mwanae.

Ye kaondoka na Shamba la Eka 10 na kiwanja chenye pagala..!! Hati ya nyumba kaacha kwa mkewe ye kaondoka na documents za kiwanja cha pagala na Shamba.

Kabla mahakama haijaamua John kashagawa mali na maisha yanasonga...!!!

Nilichofanya nilienda kupajua kwake alikopanga maana sasa Mimi ndio nimekua jirani yake..!!

Kwenye pagala lake anataka ajitahidi amalizie hata vyumba viwili ahamie maana maisha ya kupanga alishayasahau kabisaa.

TURUDI KWENU WANAUME WABISHI ......!!!!

Na hizi ndio ndoa zenu mnazokimbilia.

Mwamba alijifanya kupenda akamfungulia mpaka biashara kumbe POLE YAKE.

NIKIWAAMBIA MSIOE MUWE MNASIKIA.

Nani kakwambia kuwa wanakupenda?

Braza They love your wallet..!!

Huyu alimpenda John au alipenda pesa za John za kufungulia biashara??

Just hook with them halafu pita hivi kabla wallet haijaisha.

Ila man usisahau kuwezekeza kwenye Mali na akili (financial knowledge).

SECURE YOUR FINANCIAL FUTURE.

When You have ASSETS and FINANCIAL KNOWLEDGE, Then it's ENOUGH..!!!

PESA NDIO KILA KITU, Huoni ZILIVYOMUOKOA RAFIKI YANGU JOHN.

#YNWA
Visa kama hivi vinatokea hata kwa wazinifu wa kawaida ambao hawajaoana.napenda kusema ubaya hauna kwao.






Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Hawa watu inataka moyo sana kuishi nao! Yani kimsingi hamna haja ya kushangaa huyo mke jamaa alifosi yeye
Kuna Lecturer kasafiri majirani tunaona baada ya wiki mke kaleta mkenta ule sijui fuso kasomba kila kitu wamama wenzake wanamuuliza kulikoni ... Akawajibu tumehamishiwa singida Mme wangubkahamishiwa huko ...hahaahahaaaa siku ngapingapi kama tatu hivi Mme huyu hapa karudi kutoka alipoenda kumbe alienda workshop Uganda. Mke wake kasomba kila kitu na mifugo kauza kubabeki.
 
Kuna Lecturer kasafiri majirani tunaona baada ya wiki mke kaleta mkenta ule sijui fuso kasomba kila kitu wamama wenzake wanamuuliza kulikoni ... Akawajibu tumehamishiwa singida Mme wangubkahamishiwa huko ...hahaahahaaaa siku ngapingapi kama tatu hivi Mme huyu hapa karudi kutoka alipoenda kumbe alienda workshop Uganda. Mke wake kasomba kila kitu na mifugo kauza kubabeki.
Yani mke kasafisha mjengo mubasharaa
 
Back
Top Bottom