Nikiwa Tz nitumie mtandao gani wa mawasiliano?

cha ajabu watanzania wananunua...nyumbani TV.., kwenye gari TV.., baa TV.., simu TV....ha haaaa kazi kweli kweli...wachina wao wanauza tu
Ni vzuri...kwa kua inawapa taarifa mbali mbali pia burudani.
Oh!
 
lakini ukizingati line ni chini ya 1000/= kwanini asiwe nazo zote?
kwa sababu bei ya sim card sio gharama pekee iliyopo katika kumiliki line nyingi. Itabidi ubebe misimu mingi mifukoni, au uwe na simu moja yenye line nyingi, ambazo nyingi ni magumashi ya kichina.
 
Njoo na desktop na inverter umemem wa tabu... 12hrs outage.. :roll:

Wewe kweli unaona mbali umekumbuka jambo ambalo, wengi tumesahau kwa sababu ya mazoea,issue (inshu)ya umeme ni balaa karibe tz bwana ndevu, ila usobebe jacket yoyote njo singlet tu kuna joto la kufa mtu
 
karibu Tz. Siku hizi kunz usafiri wa Boda boda(motorcycle) foleni haifai balaa.
Ila kuna mpango wa kujengewa bara bara za juu kwa juu(fly over). Kama litatimizwa. Watoto/mabinti 2nababaikia wageni maana wa humu humu wanatunyanyapaa.
Nami napatwa na dharuba hiyo.
 
pia usitarajie kulipwa kwa usumbufu utaopata kwenye hizi celular network co!
Unaweza kukatwa pesa yako bila ridhaa kwenye hizi kampuni za simu.tunachangishwa michango bila kupenda!
Yaani ndio hivyo tena Ndevu Mbili.
 
cha ajabu watanzania wananunua...nyumbani TV.., kwenye gari TV.., baa TV.., simu TV....ha haaaa kazi kweli kweli...wachina wao wanauza tu
cha ajabu ni nini? ina maana ukiwa na TV nyumbani usiwe na ya kwenye gari au ofisini au ya kwenye simu? kama una mawe (hela) unaweka TV popote unapotaka hata chooni au stoo unaweza kuweka hela yako tu mbona nje watu wana TV kwenye kila chumba na kwenye gari na kila sehemu hatusemi
 
Kweli kila mtu na mawazo yake humu!
Maisha haya ni magumu.
Kuwa na mawe(pesa) haikatazwi lakini imekua gape kati yenu wenye nazo na wasio kua nazo...wenye nazo ndio wanaowachukulia wasio nazo!
Hizo Tv kila sehem za nini? Wanachuo wanaumia huko na migomo hawasikizwi...wewe unasema kuna ubaya gani wakati unayo mawe(peso)!
Jamani mtuonee huruma!
 
ila topiki zako Ndevu mbili zimekaa kihaya kihaya, anyway kaibu sana Bongo maana unaonekana fikra zako kuhusu Bongo ni kama unaenda jehanamu lol.
 
Kweli kila mtu na mawazo yake humu!
Maisha haya ni magumu.
Kuwa na mawe(pesa) haikatazwi lakini imekua gape kati yenu wenye nazo na wasio kua nazo...wenye nazo ndio wanaowachukulia wasio nazo!
Hizo Tv kila sehem za nini? Wanachuo wanaumia huko na migomo hawasikizwi...wewe unasema kuna ubaya gani wakati unayo mawe(peso)!
Jamani mtuonee huruma!
sijasema hivyo kwa ubaya lakini kama una pesa kwa nn usifanye kitu roho inapenda? kama mtu anagoma ili haongezewe BOOM ni tatizo litakalosababisha mimi nisiweke TV kila chumba kwenye nyumba yangu? siku zote MUNGU ameumba watu tofauti kimapato na kimaisha shida za jirani yangu haziwezi kuninyima usingizi hata usiku mmoja kama akaunti yangu inasoma salio la kutosha na deal zangu zinaingiza hela
 
Usinielewe vibaya haya ni mazoea yangu tangu huko Bongo. Hata wazazi na marafiki,walimu na ww...wanajua nlipenda kuomba ushauri wa kila jambo!
Mke atabakia huku...kwani nkiwa huko huduma ya massage hakuna?
Itansaidia kwa muda wote nkiwa huko. Pia nina hilo tatizo nasikia dawa za nyumbani zinasaidia zaidi hii shida /kaugonjwa.(nataka viagr*).
Hapa umenichanganya kidogo, nini mahusiano kati ya mke kubakia huko,massage bongo,dawa za nyumbani na viagra....please fafanua ili tukupe msaada unaotakiwa......
All in all karibu kwenye Joto, Mgawo wa umeme, vumbi,wadudu,majungu,mafisadi,wezi,RA,JK,Richmond aka Dowans nk
 
Habari zenu wana JF!
Poleni na matatizo ya hapo nyumbani!
Tutaijenga nji yetu japo itatuchukua miaka mingi...naamini itatukuka!
Hivi huku nimezoeea mawasiliano bila kero...
Je nkiwa huko Tz nitumie mawasiliano kupitia kampyni gani ya simu?
Nawaombeni waungwana mniwasilishie.
Mniju.....

Naomba usijiunge na VODACOM kwa kuwa umtamtajirisha mtu anaye tuibia ROST HAM
 
Hapa umenichanganya kidogo, nini mahusiano kati ya mke kubakia huko,massage bongo,dawa za nyumbani na viagra....please fafanua ili tukupe msaada unaotakiwa......
All in all karibu kwenye Joto, Mgawo wa umeme, vumbi,wadudu,majungu,mafisadi,wezi,RA,JK,Richmond aka Dowans nk
Mwenzangu bado atabaki huku huku Canada. Japo ninalo hilo tatizo....mbali na tendo lenyewe ntapenda kua na mtu wa karibu zaidi kubadilisha mawazo n.k
Waweza nipa msaada wako pia kwa hili.
Ahsante.
 
Simu ya kichina ikoje yenye Line 3,4?

wewe njoo bongo nenda kariakoo mtaa wa green uliza hyo cmu yan zipo hata line 6 wewe unashangaa 3 na 4 wewe njoo alafu ulizia utapata hii ndo tanzania kilaki2 kipo baba yake wewe 2
 
Mimi nakushauri utumie simu na namba yako kama kawaida ila ukiwa tanzania tumia huduma ya roaming. Hiyo itakuwezesha ku hook kwenye network yoyote huko Bongo na kuendelea na mawasiliano kama kawaida.
Hiyo itakusaidia sana huko canada watakupata kwa simu na Bongo utawapigia simu watu kama kawaida.
tatizo jamaa wa Bongo watashindwa kukupigia sababu ya gharama ila wewe hakuna shida bei ile ile ya bongo.
 
Mkuu Roaming acha kabisa utakuwa charged hata kupokea simu., yaani jamaa zake wa Canada wakimpigie hata kupokea tu yeye mwenyewe ndio analipa, solution ni very simple hata kama anayo handset moja anaweza akawa na Sim cards zote atakuwa anaswap pale anapopigia watu..., Hivyo ndio bongo tunavyoishi
 
Back
Top Bottom