Nikiwa Rais wa nchi hii ndani ya miaka 5 nitabadili madhali ya miji yetu iwe hivi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
1540803020647.png

Moja ya mambo ambayo yananikera katika nchi yangu hii ya Tanzania ni ushaghalabara wa mandhari katika miji yetu, kinachonikera zaidi ni kuona mambo ambayo ni madogo kama ya kuweka madhari nzuri katika miji yetu hayafanyiki.

hivi kweli manispaa zetu zinashindwa kutenga fedha katika mapato yake kupanda bustani pembezoni mwa barabara zetu? hivi kweli tunashindwa hata kutumia wafungwa tunaowafungia ndani wawe wanafanya kazi kazi za kutengeneza mandhari ya miji yetu?

hivi kweli tunashindwa kubadili mfumo wa mafunzo ya vijana baada ya kumaliza kidato cha sita wawe wanatokea nyumbani, wanalipwa fedha kidogo kama elfu 5 kwa siku na wote wanafanya kazi za kijamii katika miji kuweka miji yetu katika mwonekano mpya na kuwajengea hulka za kuweka mazingira katika hali inayovutia?

hivi kweli tunashindwa kutunga sheria za makazi kuwalazimisha wananchi kila mmoja atengeneze mazingira yanayomzunguka kuweka mandhari nzuri?

Daima huwa nakuwa irritated ninapoona tunaendelea kukumbatia old fasheni strategies ambazo hazielekei kubadili living standard ya watu wetu kutoka kwenye uovyo kwenda kwenye umodern bali kupiga hatua katika uovyo.

1540804204564.png

Hii ndiyo miji ya kiafrika na ni miji ambayo haionekani kuwakera wanaotuongoza. Nilitegemea hapa tulipo tumejifunza mengi na tuanze kusema huku tuliko siko na kuanzia sasa tunabadili direction au uelekeo. ili kubadili uelekeo ni lazima utambue ni changamoto zipi zimetupelekea kuwa na makazi ya hivi? na kuyaadress katika new direction.

kinachosikitisha ni pale unakwenda katika mji na kukuta makazi yaliyojengwa miaka ya 70 yalikuwa katika mpangilio lakini makazi yanayojengwa leo tunatengeneza kinachoonekana kwenye picha ya pili. Kinachosikitisha zaidi ni pale wizara inayojihusisha na makazi inapoonekana kutokukerwa na miji yetu inavyojengeka na kuanza kuhalalisha makazi haya ilimradi tu yalipe kodi na tukiendelea kutengeneza makazi ya ajabu.

Tunahitaji regulator ambaye atachora mstari kwa makazi holela na kusema hapo ndio mwisho na kutoa dira mpya. Regulator huyu Anaweza kupanga mwenyewe au kutoa kanuni kwa wadau walioko kwenye sekita hii ili wao wajipange.

Nikiwa raisi recruitment yangu kwa waziri wa makazi itakuwa "hivi unaona miji yetu ilivyo ovyo? unafikiri tufanye nini ili miji yetu ifanane hivi kwa kumuonyesha mahali palipokaa vizuri? kama unadhani ama haiwezekani kubadili miji hii kwa maana wananchi walishajenga na kama tunataka kuibadili basi tukope fedha tuwalipe fidia alafu tupange upya, then you are bogus hautakaa upate hiyo fursa.

Tutazame mfano hivi haya makazi ni nani anagawa viwanja hivi? ni wananchi wenyewe na pengine kushirikiana na serikali za mitaa. Hawa wanaofanya kazi hizi wamepewa mwongozo gani na Hawa wanaolipwa kodi za watanzania washughulikie makazi? Ukiwauliza hawa tufanye nini wanakimbilia kupanga miradi ya kwenda kukopa benki ya dunia mabilioni.

Tunashindwa kutoa mwongozo kwa serikali za mitaa kwamba kila kiwanja katika miji ni lazima kiwe na ukubwa usiopungua huu na usiozidi huu, kila kiwanja katika mji ni lazima kiwe na access ya barabara na barabara hizi za mitaa ukubwa wake ni huu.

ili kuwadhibiti hawa wanaouza, ukiwa na kaeneo kako ukipima hakaja fikia kiwango kilichoruhusiwa hauwezi kukauza kama kiwanja tafuta njia nyingine ya mapato. mnaweza kukubaliana majirani kuchanganya eneo ili lifikie ukubwa unaokubalika kisheria na mapato mgawane kwa proportions za ukubwa wa eneo alilochangia kila mmoja.

wanunuzi waelezwe ukinunua kiwanja kilicho chini ya kiwango itakuwa hasara kwako, ukinunua kiwanja kisicho na barabara shauri yako lakini pia serikali za mitaa wapewe semina za kuwapa maarifa ya kuhandle mambo haya. kupanga barabara na kuseti preliminary arangements ambazo wanaweza kuwa wakiwasiliana na halmashauri husika katika mambo haya.

waliokwisha kuvuruga wapewe probashasheni period ya 10 yrs. ikiwezekana majirani wanunuliane ili kama umenunua 12m kwa 12m na jirani yako ana 15m kwa 18m na mkaambiwa miaka 10 ijayo mnatakiwa kuwa mmetafuta ufumbuzi kwa maana kiwanja cha chini kitakuwa 20m kwa 20m ni kutazama yupi amuuzie yupi ili mmoja atimize vigezo kwa gharama nafuu na huyu kurudisha fedha yake akaongeze fedha nyingine na kujenga pengine. au nyote uzeni kwa mtu mwingine.

Wakati mwingine tunahitaji sheria kubadili hulka zilizojengeka katika jamii. Unaweza kukuta mtu anamiriki simu tatu kwa ajili ya kujionyesha tu lakini akikupeleka kwenye nyumba anayoishi utashangaa, rangi ya nyumba haitambuliki tena. ukipiga mahesabu ya gharama ya ndoo moja ya rangi ya maji na kulimpa fundi kwa siku kubadili mandhari ya nyumba anayoishi ni nafuu kuliko simu za ziada anazomiriki.

Viongozi wanaotoka katika jamii zenye hulka hizi unakuta wanawatungia wananchi sheria za kutokutumia magari mitumba na kutaka wanunue mapya, kuwazuia kutumia simu zilizopitwa na wakati na kuwataka kutumia smartphones, kuwazuia kutumia tv za kizamani na kuwataka kutumia za kisasa. hii ni kwa sababu hawawezi kutazama jamii zao wakatambua shida zao na kuzipa kipaumbele bali wakisikia ulaya wanatoka kwenye technolojia fulani wanakimbia kusema na sisi bila kujua mambo ya msingi kama makazi kwa kule walishapiga hatua na kwa sasa wako kwenye mambo ya luxury na hivyo tuanzie kwenye mambo basic kama makazi tuwekeane utaratibu.

haiwezekani unaweka kibanda cha biashara manzese unaezeka kwa mfuko wa cementi tukuangalie tu. unakuta nyumba kariakoo kuelkea msimbazi ina wapangaji wa maduka wanalipa kodi kubwa lakini nyumba inafanana ghofu haina ukarabati. tufike sehemu tuwekeane sheria nyumba ikichafuka tupigane faini. Nyumba ndani ya Dar es salaam imeezekwa kwa kushikilia mabati kwa mawe??? ukitathmini gharama ya kununua kilo moja ya misumari na hata nyundo baba mwenye nyumba au kijana upande juu ugonge mwenyewe ni kiasi gani? unakuta ni hulka tu tulizojijengea kuona mambo ya kawaida tu.

Unaweza kupita barabara ya musoma mwanza kutokea nyanguge mpaka mwanza unaona majumba yenye biashara, mashine mbalimbali lakini utafikiri magofu na bado tunasema mwanza inaongoza kwa usafi.

ukiitazama kigali kwenye picha ki msingi wanajitahidi kutengeneza bustani za kando ya barabara lakini sisi tunaongozwa kwa old fasheni mind, funga biashara mpaka saa fulani lakini magofu ni yale yale. kwa nini tusiseme manispaa wabanwe kutengeneza bustani kwenye barabara zao na maeneo ya wazi, wananchi wabanwe kutengeneza mazingira kwenye makazi yao. na si swala la mwananchi anafanya mwenyewe kwa mikono yake au la bali kama unaweza kumuajiri mtu mwingine akuwekee mazingira kwa standard inayotakiwa ni vizuri zaidi maana umetoa ajira kwa mtu lakini kama huna uwezo fanya mwenye
 
Tatizo ni jiwe....Jiwe ni tatizo...yeye karuhisu machinga wafanye biashara sehemu yoyote ile wapendayo.....na machinga ndio wachafuzi wakubwa wa mazingira...

Jiwe ni tatizo
 
Nina uhakika asilimia 100 kipau mbele cha Taifa kwa sasa siyo hicho unachokiwaza.

Wananchi wanaishi kwenye dimbwi kubwa la umaskini, hata ukipanga huo.mji uwe kama miji ya ulaya watakula mawe.

Kipau mbele chetu kwa sasa kinatakiwa kuwa elimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimu....

Tukishakombolewa hapa hata haki zetu watu wataweza kudai kwa nguvu maana wanayo elimu na hawatapenda kudanganyika. Na hayo mengine yote yatakuwepo. elimu, elimu, elimu elimu elimu elimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimu....
 
Hizo ndo akili mbovu, unadhani kazi ya kujenga miji na majiji ni ya Rais...ndo maana na bwana yule aliyejitangaza kuwa yeye ni kichaa na huteua vichaa wenzake kuipora nchi naye anadhani kazi ya kujenga miji ni ya kwake, pumbavu kabisa!
 
Nina uhakika asilimia 100 kipau mbele cha Taifa kwa sasa siyo hicho unachokiwaza.

Wananchi wanaishi kwenye dimbwi kubwa la umaskini, hata ukipanga huo.mji uwe kama miji ya ulaya watakula mawe.

Kipau mbele chetu kwa sasa kinatakiwa kuwa elimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimu....

Tukishakombolewa hapa hata haki zetu watu wataweza kudai kwa nguvu maana wanayo elimu na hawatapenda kudanganyika. Na hayo mengine yote yatakuwepo. elimu, elimu, elimu elimu elimu elimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimuelimu, elimu, elimu elimu elimu....

tatizo ni sisi tuko kwenye ile "vicious cycle of poverty" na tunadhani tutakumbatia nadharia mpaka siku moja nadharia zitatuoa huko.

inabidi tutoke kwenye nadharai hizo za kusema elimu elimu elimu.

asilimia kubwa ya elimu ya mwanadamu ni mazingira yanayomzunguka. mpeleke mwanadamu darasani umfundishe mipango miji lakini awe anaishi kwenye mazingira shagala bagalabagala. ukimpa mtihani kwenye karatasi atakumbuka formula na kanuni zote lakini katika maisha yake halisi akili yake imejaa mambo aliyoyazoea kuyaona.

umasikini sio technolojia kusema inabidi watu wakasome nadharia darasani ili kuiielewa bali umasikini ni mfumo wa maisha.

kama mtaani mzima nyumba miaka nenda miaka rudi hawapaki rangi unategemea watapata wapi ajira vijana walioko katika mtaa huo kuondoa umasikini? kama mtaani hakuna anayepanda maua vijana wataotesha wapi vitalu vya maua kuuza kupata kipato cha kuondoa umasikini.

ni kutokuelewa dhana ya umasikini ndio maana mnagangania elimu elimu elimu.

ni lazima jamii itunge sheria za ku create ajira mpya katika jamii. Hatuwezi sote kuwa madaktari, kuwa walimu, kuwa wahandisi, kuwa wahasibu na hizi ndizo fursa tulizozizoea lakini kadiri mzunguko wa fedha unavyokua tunahitaji kuzalisha fursa mpya katika jamii.

mathalani ukishatunga kanuni mpya za mazingira katika jamii, ukawalazimisha wanajamii kutengeneza bustani, kuhakikisha nyumba zao zinakuwa katika mwonekano unaokubalika, ukawalazima kupanga makazi yao bila shaka unaweza ku create ajira zifuatazo
1. Interior/exterior designer
2. mafundi rangi
3. garderner
4. Land surveyors

n.k

unapokuwa na mtaa ukiwa na wakazi elfu kumi na wakazi hawa ukawabana wasitumie viato vyao katika mambo yasiyo ya msingi kama electronics ukazidervert fedha hizi kufanya mambo katika mtaa wao utapunguza umasikini katika mtaani huo kwa maana watu wengi wataajiriwa katika mtaa na kujipatia vipato. watu wengi wakijipatia vipato unachochea biashara zaidi kwa maana ya kutengeneza fursa zaidi.

kwa kifupi tunakalia kwenye ujinga na kukalili elimu elimu elimu kama njia za kuondoa umasikini badala ya kutazama fursa za kuwakwamua watu wetu.kadiri unavyotengeneza fursa ndivyo ziakwenda zikifungua fursa zaidi za elimu katika jamii.

huwezi kubadili jamii kwa kuwa na wataalamu bila kuwa na fursa husika katika jamii ukitegemea eti elimu elimu itawakomboa. unapeleka watu wanasoma nyukilia wanaishia kufanya kazi ambazo hazihusiani na nyukilia mpaka wanastaafu ukitegemea ukiongeza wataalamu zaidi ndio utatoka. huo ni umbumbu ambao unaendelea kutulimbikizia umasikini.
 
Umenena
 
Back
Top Bottom