Nikiwa ninatokea Kariakoo/Ubalozi wa Marekani nishuke kituo gani?

Kama unatokea Kariakoo panda gari za KAWE.. Shuka kituo kinaitwa kwa MWALIMU!
Kutoka kwa mwalimu unaweza kutembea au unachukua boda boda elfu moja mpaka mlangoni kwa Ridhwani Kikwete

Njia nyingine ni uchukue gari za kwenda MAKUMBUSHO.. Unaenda mpaka mwisho wa gari stendi kabisa! Ukishuka unachukua boda boda unamuambia akulete kwa Ridhwani Kikwete gharama huwa ni Elfu 2 maximum.

Njia nyingine panda gari za MAKUMBUSHO kupitia Kinondoni shuka Kituo cha MOROCCO AIRTEL. Ukishuka tu kituoni request BOLT ikulete SENGA ROAD 23. Gharama yake huwa haizidi 2000 maximum.
 
Kwa mguu ukishuka morocco ni rahis zaid hata hapo namanga pia panafikika kirahis sanaa...Almost 3 to 5 minutes
Hapana aisee.. Kutoka Morocco mpaka kwa Ridhwani kwa mguu ni ishu mzee.. Njia rahisi ya kufika kwa mguu ni kushuka kituo cha Mwalimu kule kisha anakuja na Road ya Rose Garden mpaka mtaa wa SENGA ROAD hapo anakuwa amefika tayari
 
Hapana aisee.. Kutoka Morocco mpaka kwa Ridhwani kwa mguu ni ishu mzee.. Njia rahisi ya kufika kwa mguu ni kushuka kituo cha Mwalimu kule kisha anakuja na Road ya Rose Garden mpaka mtaa wa SENGA ROAD hapo anakuwa amefika tayari
Uko right pia mkuu.
Mi nimezoea hiyo zaid dats y
 
Nimeambiwa niende Mikocheni kwa Rizwan (Senga Road) near St Florence School. Nikiwa ninatokea kariakoo/ubalozi wa Marekani nishukie kituo gani? Mimi nimeishi saaana Iringa na Tabora hivyo ni mgeni/mshamba wa jiji. Wenyeji wa Dar ninaomba msaada wenu.
Kama huna wazo si usome ya wengine badala ya kupoteza muda?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom