Nikiwa naitazama kinachoendelea Tanzania kwa sasa kwa wapinzani natabasamu

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Nikiwa naitazama kinachoendelea Tanzania kwa sasa kwa wapinzani natabasamu tu maana najua tunapaswa kukipitia ili kuweza kuifikia Tanzania ile tuitamaniyo, Tanzania ya usawa kidemkorasia na kiuchumi. Yanayompata Lissu mimi huwa siumii na wala huwa sinung'uniki, yanayowapata CUF na CHADEMA wala hata hayatishi wala kuogopesha bali yanatia chachu ya kupigania haki zaidi na zaidi bila kukata tamaa. Tulipaswa tuyapitie haya mapema sana baada ya 1992 au kabla ya 1992 sema wengi wa wanasiasa wetu walikosa ufahamu na wananchi wengi hawakuwa na elimu hivyo ndio maana tumecheewa kuyapitia haya.

Kule nchini Kenya mambo haya ya kunyanyasana, kuwekana rumande, hata kuuliwa wapinzani yamefanywa sana miaka ya 70 na 80 kwa sababu wengi wa Wakenya waliwahi kuuona mwanga wa elimu na kuutumiaa haswa.

Ngoja niwape hadithi kidogo, mwaka 1978 Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta alivyofariki madaraka yalichukuliwa na Daniel Arap Moi, mzee Moi alikuwa zaidi ya dikteta, hakutaka kupingwa wala kusikia sauti mbadala, alikuwa mbinafsi na aiyejaa chuki kwa wapinzani wake, na ukumbuke ipindi hicho nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa na mfumo wa chama kimoja cha siasa, kule Kenya kilikuwa KANU ndio kinaongoza.

Wakaibuka vijana machachari sana kwenye bunge la Kenya , vijana hawa wakaitikisa sana serikali kwa michango yao bungeni na nje ya bunge, walikuwa machachari kweli kweli. Ila kwa umahiri wao walifanikiwa kuteka umma wa Wakenya haswa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za kisomi na hata wananchi wa mashinani walizielewa hoja zao. Walipingana sana na jinsi serikali ilivyokuwa ikiendeshwa kiupendeleo na kikandamizi, walipinga mfumo wa uchumi wa Moi. Vijana hawa walifahamiana bungeni tu baada ya kuwa na hoja zinazoendana kila kwenye debate ya bunge.

Wengi wa vijana hawa walilazwa sero na wengine kukimbia nchi na kwenda kuishi uhamishoni ili kuyakimbia madhira ya serikali ya Moi, lakini hawakukoma. Walipambana nje ya bunge wakitaka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi Kenya ili kutoa fursa sawa ya mawazo na sauti. Kile walichokipigania sasa kinatoa matunda , nchini Kenya kwa sasa sauti inasikika kutoka kwa yeyote na serikali inaheshimu.

Vijana hawa maarufu walipewa jina maarufu la THE SEVEN BEARDED SISTERS (WADADA SABA WENYE NDEVU), lilikuwa jina la kebehi tu kwao kwamba , wao walifananishwa na wanawake tu wenye ndevu japo kwenye kundi hilo hakuwepo mwanamke hata mmoja. Jina hilo walipewa na serikali ya dikteta Moi. Hawakujali. Walichokitaka ni utawala wa kisheria unaojali haki za binadamu na usawa.

Vijana wa The Seven Bearded Sisters walikuwa

1. James Orengo
2. Abuya Abuya
3. Onyango Midika
4.Mwashengu wa Mwachofi
5. Lawrence Sifuna
6. Chibule wa Tsuma
7. Koigi wa Wamwere

Vijana hawa walikuwa na miaka kati ya 25-35 tu kwa muda ule ila walionyesha ukomavu uliopindukia. Juhudi zao zilizaa matunda hatimae 1992 wakiungana na wanasiasa na watu mbalimbali walilazimika kuilazimisha serikali kufanya mabadiliko katika katiba yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini humo. Waliopo hadi sasa kati ya hao saba ni James Orengo, Sifuna, Wamwere , wengine walikwisha tangulia mbele za haki ila wanakumbukwa na kwa misimam yao na matunda ya wao kulala cello yanaonekana hadi kesho. Kati ya hao saba hakuna aliyelala cello pungufu ya miaka minne, na hata kuishi uhamishoni kwa miaka kadhaa.

Kwa kushirikiana na wanasiasa wakongwe na wazoefu pamoja na wanaharakati akina Michael Kijana Wamalwa, Kiraitu Murungi, Raila Odinga, Paul Muite Jaramogi Oginga Odinga, Masinde Muliro na Martin Shikuku walifanikiwwa kuitikisa serikali katika uchaguzi wa 1992 kiasi cha kushindwa kwa uchache sana wa kura. Mbegu ile waliyoipanda haikupita miaka mingi serikali ya Moi ilianguka kifo cha tembo.

Kinachosababisha haya tunayoyaona nchini kwa sasa yatokee ni kwa

1. Hakukuwa na maandalizi yaliyofanywa na wananchi wenyewe katika kuingia katika mfumo wa siasa za vyama vingi, wananchi hawakuwa na uelewa juu ya mfumo huu. Wengi wa wananchi walikosa uelewa na elimu, ndio maana hata jaji Nyalali alipokuwa anakusanya maoni ni asilimia 20 tu walionyesha kuuukubali mfumo wa vyama vingi, ikiwa na maana ya kwamba 80 walikataa.

2. Hakukuwa na msukumo wa kisiasa wa katika kuingia kwenye mfumo huu, wanasiasa wetu tokea ktambo wamekuwa, ni wasisiasa wepesi sana katika uga wa kuhoji, kuchambua na kuchanganua mambo hivyo hawakuwa na uelewa wa kiundani kuhusu mfumo mbadala wa kisiasa uliotaka kuletwa nchini, hawakujiandaa kumpokea mtoto ambae hawajamdungia mimba. Tofauti na Kenya ambapo tayari kulikuwa kunafurukuta tangu 1967 wanasiasa walikuwa tayari.

3. Kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi kwa msukumo wa mashirika ya kifedha ya nje kama WB, IMF na mataifa ya Magharibi kwa sababu ya kuogopa kukosa mikopo na misaada. Nchi nyingi haswa Tanzania ikiwa miongoni mwao walilazimishwa kuingia kwenye mfumo huu wa vyama vingi kwa sababu waliambiwa bila kufanya hivyo wangekosa misaada ya kifedha na kiuchumi na haswa ukizingatia ndio tulikuwa tumetoka kulishuhudia anguko la USSR ambao walikuwa washirika wetu hivyo kukawa hakuna budi ni lazima kutii matakwa ya magharibi.

Tunapoelekea sasa, ni kule ambako wakenya walikupita miaka 40 iliyopita, manyanyaso waliyoyapitia akina Odinga ndio lazima yawapate akina Lissu ili tuje tuijenge Tanzania ya kweli, usidanganyike hakuna mtawala anaependa kuhojiwa kuhusu utumbo anaoufanya, atakuwa tayari kukulza gerezani miaka hata kumi ili mradi tu usimhoji. Hatuna haja ya kumuonea Tundu Lissu huruma juu ya anachokipitia, wanapaswa kukipitia hiki ili kujenga roho ya upambanaji. Msishangae hata akafungwa jela kabisa hapo baadae. Ni lazima tupite huko ili kuijenga free society yenye fikra huru na pevu.
 
Mbona NCCR Mageuzi, ATC WAZALENDO na vingine vingi tu mnaviacha?
Dhambi hii ya ubaguzi haita waacha salama.
Eti Sisi ni bora kuliko wale

Bado Tanzania hatujapata upinzani wa Kweli. Wengi ya hawa wanaojiita wapinzani ni wachumia tumbo tu.

Kumbuka Chagadema walivyobadili gia angani kisa Mpunga wa Mzee Lowassa

Walisema miaka zaidi ya saba kwamba dingi ni fisadi.
Dhambi hii Lazima iwabomoe kama jinsi walivyombomoa Mzee Lowassa mpaka CCM kumuengua.
Sishangai upinzani huu uchwara kujifia kifo cha mende, na hizi ndo dalili.
Wasitafute mchawi. Eti serikali ya CCM .
wachawi ni wenyewe kwa tamaa zao badala ya kutanguliza maslahi ya waliowachagua. Kama anavyofanya RAIS MAGUFULI, wanajali matumbo yao familia zao na jamaa zao wa karibu.

Magufulication oyeeeeeeeeeee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Chama cha ACT ni upinzani? Tawi la CCM haliwezi kuwa upinzani
 
Wengi wana elimu ila wachace sana walioelimika
 
Bavicha bana!upinzani wa kenya huwezi kulinganisha na wachumia tumbo wetu.Mbowe kauza chama kwa bilioni 5,na mpaka sasa siasa mnaongoza kwa matukio na mihemko tu
 
Mkuu,kwenye hii hadithi yako uliyotusimulia hapa inaonyesha wazi hao wanasiasa wa kenya walichokua wanakipigania ni nini.
Sasa unaweza kunisaidia kuniambia Tundu lissu,lowasa et al wanachokipigania ni nin mpaka sasa?
 
Nikiwa naitazama kinachoendelea Tanzania kwa sasa kwa wapinzani natabasamu tu maana najua tunapaswa kukipitia ili kuweza kuifikia Tanzania ile tuitamaniyo, Tanzania ya usawa kidemkorasia na kiuchumi. Yanayompata Lissu mimi huwa siumii na wala huwa sinung'uniki, yanayowapata CUF na CHADEMA wala hata hayatishi wala kuogopesha bali yanatia chachu ya kupigania haki zaidi na zaidi bila kukata tamaa. Tulipaswa tuyapitie haya mapema sana baada ya 1992 au kabla ya 1992 sema wengi wa wanasiasa wetu walikosa ufahamu na wananchi wengi hawakuwa na elimu hivyo ndio maana tumecheewa kuyapitia haya.

Kule nchini Kenya mambo haya ya kunyanyasana, kuwekana rumande, hata kuuliwa wapinzani yamefanywa sana miaka ya 70 na 80 kwa sababu wengi wa Wakenya waliwahi kuuona mwanga wa elimu na kuutumiaa haswa.

Ngoja niwape hadithi kidogo, mwaka 1978 Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta alivyofariki madaraka yalichukuliwa na Daniel Arap Moi, mzee Moi alikuwa zaidi ya dikteta, hakutaka kupingwa wala kusikia sauti mbadala, alikuwa mbinafsi na aiyejaa chuki kwa wapinzani wake, na ukumbuke ipindi hicho nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa na mfumo wa chama kimoja cha siasa, kule Kenya kilikuwa KANU ndio kinaongoza.

Wakaibuka vijana machachari sana kwenye bunge la Kenya , vijana hawa wakaitikisa sana serikali kwa michango yao bungeni na nje ya bunge, walikuwa machachari kweli kweli. Ila kwa umahiri wao walifanikiwa kuteka umma wa Wakenya haswa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za kisomi na hata wananchi wa mashinani walizielewa hoja zao. Walipingana sana na jinsi serikali ilivyokuwa ikiendeshwa kiupendeleo na kikandamizi, walipinga mfumo wa uchumi wa Moi. Vijana hawa walifahamiana bungeni tu baada ya kuwa na hoja zinazoendana kila kwenye debate ya bunge.

Wengi wa vijana hawa walilazwa sero na wengine kukimbia nchi na kwenda kuishi uhamishoni ili kuyakimbia madhira ya serikali ya Moi, lakini hawakukoma. Walipambana nje ya bunge wakitaka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi Kenya ili kutoa fursa sawa ya mawazo na sauti. Kile walichokipigania sasa kinatoa matunda , nchini Kenya kwa sasa sauti inasikika kutoka kwa yeyote na serikali inaheshimu.

Vijana hawa maarufu walipewa jina maarufu la THE SEVEN BEARDED SISTERS (WADADA SABA WENYE NDEVU), lilikuwa jina la kebehi tu kwao kwamba , wao walifananishwa na wanawake tu wenye ndevu japo kwenye kundi hilo hakuwepo mwanamke hata mmoja. Jina hilo walipewa na serikali ya dikteta Moi. Hawakujali. Walichokitaka ni utawala wa kisheria unaojali haki za binadamu na usawa.

Vijana wa The Seven Bearded Sisters walikuwa

1. James Orengo
2. Abuya Abuya
3. Onyango Midika
4.Mwashengu wa Mwachofi
5. Lawrence Sifuna
6. Chibule wa Tsuma
7. Koigi wa Wamwere

Vijana hawa walikuwa na miaka kati ya 25-35 tu kwa muda ule ila walionyesha ukomavu uliopindukia. Juhudi zao zilizaa matunda hatimae 1992 wakiungana na wanasiasa na watu mbalimbali walilazimika kuilazimisha serikali kufanya mabadiliko katika katiba yake na kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini humo. Waliopo hadi sasa kati ya hao saba ni James Orengo, Sifuna, Wamwere , wengine walikwisha tangulia mbele za haki ila wanakumbukwa na kwa misimam yao na matunda ya wao kulala cello yanaonekana hadi kesho. Kati ya hao saba hakuna aliyelala cello pungufu ya miaka minne, na hata kuishi uhamishoni kwa miaka kadhaa.

Kwa kushirikiana na wanasiasa wakongwe na wazoefu pamoja na wanaharakati akina Michael Kijana Wamalwa, Kiraitu Murungi, Raila Odinga, Paul Muite Jaramogi Oginga Odinga, Masinde Muliro na Martin Shikuku walifanikiwwa kuitikisa serikali katika uchaguzi wa 1992 kiasi cha kushindwa kwa uchache sana wa kura. Mbegu ile waliyoipanda haikupita miaka mingi serikali ya Moi ilianguka kifo cha tembo.

Kinachosababisha haya tunayoyaona nchini kwa sasa yatokee ni kwa

1. Hakukuwa na maandalizi yaliyofanywa na wananchi wenyewe katika kuingia katika mfumo wa siasa za vyama vingi, wananchi hawakuwa na uelewa juu ya mfumo huu. Wengi wa wananchi walikosa uelewa na elimu, ndio maana hata jaji Nyalali alipokuwa anakusanya maoni ni asilimia 20 tu walionyesha kuuukubali mfumo wa vyama vingi, ikiwa na maana ya kwamba 80 walikataa.

2. Hakukuwa na msukumo wa kisiasa wa katika kuingia kwenye mfumo huu, wanasiasa wetu tokea ktambo wamekuwa, ni wasisiasa wepesi sana katika uga wa kuhoji, kuchambua na kuchanganua mambo hivyo hawakuwa na uelewa wa kiundani kuhusu mfumo mbadala wa kisiasa uliotaka kuletwa nchini, hawakujiandaa kumpokea mtoto ambae hawajamdungia mimba. Tofauti na Kenya ambapo tayari kulikuwa kunafurukuta tangu 1967 wanasiasa walikuwa tayari.

3. Kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi kwa msukumo wa mashirika ya kifedha ya nje kama WB, IMF na mataifa ya Magharibi kwa sababu ya kuogopa kukosa mikopo na misaada. Nchi nyingi haswa Tanzania ikiwa miongoni mwao walilazimishwa kuingia kwenye mfumo huu wa vyama vingi kwa sababu waliambiwa bila kufanya hivyo wangekosa misaada ya kifedha na kiuchumi na haswa ukizingatia ndio tulikuwa tumetoka kulishuhudia anguko la USSR ambao walikuwa washirika wetu hivyo kukawa hakuna budi ni lazima kutii matakwa ya magharibi.

Tunapoelekea sasa, ni kule ambako wakenya walikupita miaka 40 iliyopita, manyanyaso waliyoyapitia akina Odinga ndio lazima yawapate akina Lissu ili tuje tuijenge Tanzania ya kweli, usidanganyike hakuna mtawala anaependa kuhojiwa kuhusu utumbo anaoufanya, atakuwa tayari kukulza gerezani miaka hata kumi ili mradi tu usimhoji. Hatuna haja ya kumuonea Tundu Lissu huruma juu ya anachokipitia, wanapaswa kukipitia hiki ili kujenga roho ya upambanaji. Msishangae hata akafungwa jela kabisa hapo baadae. Ni lazima tupite huko ili kuijenga free society yenye fikra huru na pevu.

Umesema vema kabisa. tunahitaji watu wa kujitoa mhanga ili mapambano yaendelee. angalau kuwaunga mkono tu wale wanaothubutu kufanya hivyo. inasikitisha kwamba hata wale ambao hawataki kabisa hata kugusa tu kwa ncha ya kidole, lakini bado wanawakatisha tamaa wale wanaothubutu. Maisha yanahitaji sadaka. ukombozi unahitaji sadaka kubwa zaidi
 
Bavicha bana!upinzani wa kenya huwezi kulinganisha na wachumia tumbo wetu.Mbowe kauza chama kwa bilioni 5,na mpaka sasa siasa mnaongoza kwa matukio na mihemko tu
Wakati haya yanafanyika Kenya madikteta wa sasa wa Tanzania hawakuwa hata wamemaliza shule ! Kaazi kweli kweli !
 
Umeandika barabara!
Natamaani kuona harakati zaidi awamu hii kuliko awamu nyingine zote, actually natamaani kushiriki katika harakati zaidi ndani ya awamu hii.

Tunahitaji wapinzani jasiri na wajenzi wa hoja zaidi kujitokeza mstari wa mbele.
Tufanye siasa kwenye mabasi, tuongee kwenye mikutano ya kidini, tuongee kwenye misiba, tuongee masokoni na kila mwanachama wa upinzani acheze nafasi yake bila kusubiri uongozi wa juu wa chama!

Ukiona facts zinapotoshwa ili kumsifia mfalme somewhere na unajua ukweli, then ongea usisubiri mwaliko.

Tukiwa hai tuongee
Tunyamaze tukiwa wafu.
 
Hakuna marefu yasiyo na ncha. Hata hii Amani tunayoringia hii ni dalili kiwa soon itapotea.
Wakenya wanyarwanda wasiera leoni waliberia nao pia Walikuwa wanamuomba Mungu huyu huyu. So msijidai sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom