Nikiwa Mkubwa nataka niwe Mwanasiasa. Ndani yake nitakuwa Doctor, Mwalimu,Injia, mungu,Mfalme n.k

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
katika nchi za Afrika kuna vyeo vinavyoenda sambamba na vyeo cha Mungu. Usibishe. Vipo. Nimeangalia na kusikiliza watoto wengi wakihojiwa husema nikiwa mkubwa nataka niwe pilot,mwalimu,injia,daktar,mwanajeshi,mwanasheria,mtaalam wa...

Mimi nikagundua kuna cheo hawakifaham. Nami nawaambia waache wao wawe nafasi hizo. Mimi nikiwa mkubwa nataka niwe mwanasiasa. Tena nataka niwe Rais Kabisa. Hapo kwa nchi za Afrika nitakuwa level moja na mungu. Watakaonikwaza au kunichefua nitawapa misuko suko sana. Ntawalaza jela au ntawapotea kabisa.

Nitawadhalilisha wanaonikwaza na wanaonipenda nitawapenda. Nitahikikisha hao wengine nawapatia sehemi ya ufalme wangu ili mradi wanisifu kwa nyimbo na mapambio. Hao watakula vya kwangu wataishi kwa raha mustarehe.

Nimeyaandika majina ya wote walionichefua utotoni mwangu. Labda waje kuhama nchi. Nitawaburuza hasa, nitawararua na kuwachana chana nikikumbuka waliyonitendea zaman.

Ukiwa mwanasisa wa ngazi ya Rais afrika wewe mungu kabisa katika nyama. Usibishe. Angalia mwenyewe akina mugabe akina nani...

Wanachoamua ndicho kinachokuwa. Ni afrika rais anaweza akaua ila asihukumiwe kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom