Nikiwa kwenye gear namba 5 au 4 nitaweza kusimama?

Benevento

JF-Expert Member
Jan 3, 2019
4,982
29,535
Naomba mnifahamishe nikiwa kwenye gear namba 5 au 4 alafu natakiwa nisimame umbali ambao sitaweza kupangua gear hadi kufika namba moja je nitafanyaje?

Msaada wenu tafadhali
 
Maana yangu je hakuna madhara yeyote ya kutoka gia kubwa na kurudi moja kwa moja kwenye gia namba moja

Madhara yapo, piston inaweza kuchomokea mbavuni kama utaruka kutoka namba 5 hadi namba 1.

Kama mdau wa mwanzo alivyokwambia, kama kuna Emergency mbele, kanyaga Clutch kisha brake, hapo gari itasimama bila kuzimika vile vile Kama utakanyaga brake tupu bila clutch gari pia itasimama lakini engine itazimika hakutakuwa na madhara yoyote utapiga stata na kuendelea tena, nji hii ni kwa magari madogo.

Umeuliza kuhusu tuta. Inategeme na nguvu ya engine ya gari yako. Gari yangu mimi mfano niko namba 5 na nakaribia tuta, huwa natoka 5>4>3 napanda tuta na namba 3, kisha narudi 4>5 na kuendelea. Gari zingine zinapanda na namba 2 kama engine inaanza kuchoka.

Magari makubwa system yake ya kusimama kwenye emergence ni tofauti kidogo.
 
Naelekea kupata muafaka

Kilichokuwa kinanitatiza ni kwamba niko kwenye namba 5 then nikakanyaga clutch na brake nikasimama alafu nikaweka free nikarudi namba 1 je kuna madhara yeyote?

Na je nikitaka kupaki gari nikiwa kwenye gear 3 4 au 5 ni lazima nianze kupangua gear nakurudi namba 1?
 
Unaanza kwa kukanyaga brake kidogo ili upunguze mwendo kwanza kama ulikuwa na mwendo kazi wa zaidi ya 50kph, then ikishapungua unakanyaga clutch. Gari haliwezi kuzima ukiwahi kukanyaga clutch.

Unashauriwa kupunguza mwendo kwanza gari likiwa kwenye mwendo, hata kama ni gia ndogo kama 4, 5 au 6. Maana ukikanyaga clutch unaondoa kitu wanaita engine braking. So mzigo wote unabaki kwenye brakes pekee. Kama ni gari kubwa kusimama inaweza ikawa ishu.
 
Naelekea kupata muafaka

Kilichokuwa kinanitatiza ni kwamba niko kwenye namba 5 then nikakanyaga clutch na brake nikasimama alafu nikaweka free nikarudi namba 1 je kuna madhara yeyote?

Na je nikitaka kupaki gari nikiwa kwenye gear 3 4 au 5 ni lazima nianze kupangua gear nakurudi namba 1?

Huna haja ya kuweka free, ukishasimama toa 5 weka 1, japokuwa wanashauri utoke 5 uende 3 kisha 1.

Kupangua gia ni vizuri kwa sababu inasaidia kupunguza mzunguko wa Engine yaani Revolution.

Unapokuwa namba 5 engine huwa ipo kwenye mzunguko mkubwa, sasa ukitoka tano na kuruka kwenda 1 ni kama ule mzunguko unakuwa umeisimamisha ghafla, ndio maana nikakwambia piston inaweza kutokea mbavuni.
 
Hapa ndo nahitaji maelezo asee
Gari kubwa ukikanyaga brake na clutch haisimami hapo hapo. Labda iwe tupu. Wanashauri ukanyage brake ikiwa kwenye gia ili ile gia ikusaidie kama brake pia.

Kifupi gari kubwa ni ya kwenda mwendo mdogo mdogo tu hususan mijini. Hainaga brake ya papo kwa papo labda iwe mpya, lakink hizi za kubeba cement ni shida.
 
Ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom