Nikiwa kijijini nilidhani siwezi kumshinda alieko mjini kwenye mtihani!!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Hizi zilikua akili zangu nikiwa mdogo kule kijijini Ndolezi. Mawazo haya yalitokana na changamoto kubwa sana tuliyokua nayo pale kijijini kwetu katika uzungumzaji wa lugha ya kiswahili.

Mara zote niliwaonea shauku wanafunzi wa mijini nilidhani kwamba uwezo wao wa kukimudu vizuri kiswahili ungewasaidia kutushinda kwenye mitihani. Jambo la ajabu ni kwamba tulipoingia kwenye vyumba vya mitihani tuliwashinda wengi sana. Ndipo nikagundua kwamba kujua lugha hakuna uhusiano na uwezo wa mtu kiakili.

Tuache kupima uwezo wa mtu kwa kuangalia umahili wake kwenye lugha fulani, tumpime mtu kwa kuzingatia umadhubuti wake na uwezo wake wa kujenga hojaj
 
Ujifunze lugha kuanzia shule ya msingi,sekondari,chuo mpaka Phd na usiiimudu wewe ni kiazi aka kilaza tu
 
Ujifunze lugha kuanzia shule ya msingi,sekondari,chuo mpaka Phd na usiiimudu wewe ni kiazi aka kilaza tu
we unamuita mwenzi kiazi? unafikiri lugha ni kuongea tu? hata wingereza kuna watu wanajua kuongea kingereza lakini hawajui kusoma na kuandika.Mfano sikia sentence hii Baba yake juma alikwenda dukani akanunua baiskeli alivyorudi alisikitika sana na kushangaa kwanini mama hajapika chakula muda unaotakiwa akasema looh jamani nina njaa sana
Hebu nyambulisha hiyo sentence uweke vitenzi,vihisishi,fomimu,vielezi n.k
 
niliwahi soma shule ya msingi fulani kijijini nikiwa nimeeeeeeeeetokea mjini lakini nilikuwa nakimbizwa tu na wanafunzi wa kijijini hasa hesabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom