Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
Tafadhali naomba ukiwa kama mwana Wenge BCBG yake JB Mpiana uniambie ni kwanini Nyimbo hizi Nne zifuatazo haziishi Utamu na wala hazichuji miaka nenda rudi?

1. Champion Kapangala ( Sebene )
2. Omba ( Rhumba )
3. Wallah Danico ( Sebene )
4. Sans te Toucher ( Rhumba )

Kama una 'updates' zozote za kuihusu Bendi hii yetu pendwa ya Wenge BCBG yake JB Mpiana tafadhali karibu utupatie kwani hii Bendi ambayo Mbinguni kwa Mungu Baba inapendwa na imebarikiwa kabisa.

Wenge BCBG ni Mashine ya Muziki hasa!
 
1. Masuwa
2. I love you
3. Ndombolo
4. Cavalier Solitaire

Hizi nyimbo kusema na ukweli hata kama sina fedha hua nahisi nina pesa,pindi ninapoanza kuzisikia!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Katika hizo Nyimbo za Masuwa na Ndombolo ndipo Watu waliujua Uwezo mkubwa wa Kughani au Kurapu ( Wakongo wanaita Atalaku ) aliokuwa kuwa nao Mwalimu wa Marepa ( Atalaku ) wa Kizazi cha Pili aitwae Tutu Calugi ( jina Kamili Yombo Lumbu ) kwani alizinogesha vilivyo hizi Nyimbo.

Najivunia Kuipenda Wenge BCBG Mkuu.
 
BCBG for life, taja nyimbo zote lakini Kama hakuna Kalayi Boeing hiyo siyo Wenge ni Mawenge.
Mpaka leo bado sijaona Wimbo wa Kuupiku uitwao Kine Bouger ( yaani Kinshasa inatingishika ) ambapo Mghani au Rapa ( Atalaku ) Mwandamizi aitwae Roberto Wunda Enkokota aliutendea vyema kabla ya kumuachia Jukumu la 'Kurapu' Mwalimu Tutu Calugi na Yeye ( Roberto ) kwenda Ufaransa kutibiwa Koo lake ambalo ndiyo lilizima kabisa Safari yake ya kuwa Rapa ( Atalaku ) wa Wenge BCBG yetu hii Mkuu.
 
Tafadhali naomba ukiwa kama mwana Wenge BCBG yake JB Mpiana uniambie ni kwanini Nyimbo hizi Nne zifuatazo haziishi Utamu na wala hazichuji miaka nenda rudi?

1. Champion Kapangala ( Sebene )
2. Omba ( Rhumba )
3. Wallah Danico ( Sebene )
4. Sans te Toucher ( Rhumba )

Kama una 'updates' zozote za kuihusu Bendi hii yetu pendwa ya Wenge BCBG yake JB Mpiana tafadhali karibu utupatie kwani hii Bendi ambayo Mbinguni kwa Mungu Baba inapendwa na imebarikiwa kabisa.

Wenge BCBG ni Mashine ya Muziki hasa!
Nipe tofauti ya Wenge Musica na Wenge BCBG
 
Mimi sijui ata kwa nini nikiusikia ule wimbo uitwao OMBA nasuuzika mno moyo mkuu
Ndiyo Wimbo bora wa Rhumba ( Mziki wa taratibu ) ambao umemfanya JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG Kupendwa, Kukubalika na kuwa Tishio Congo DR nzima na huku Kwingineko.

Na huo Wimbo JB Mpiana aliuimba kwa 'Hisia' hizo za juu kwakuwa alikuwa akimuimbia aliyekuwa Mkewe ( Mpenziwe ) wa muda mrefu na aliyempenda sana Amida Shatur ambaye baadae alimsaliti kwa Tajiri ( Pedeshee ) Didi Kinuani ( kama sijakosea ) na baadae kutoka na aliyekuwa Rais wa Congo DR Joseph Kabila.

Ila kwa sasa inasemekana Wawili hawa wamesharudiana kwani walishazaa Watoto wao akina Junior Mpiana ( wa Kiume ) na Suraiya ( wa Kike ) ambao katika Album zote za JB Mpiana huwa anawataja ( anawafagilia ) kama ambavyo hata Koffi Olomide nae hupenda 'Kumfagilia' Mwanae katika Nyimbo zake aitwae Didistone.
 
Mpaka leo bado sijaona Wimbo wa Kuupiku uitwao Kine Bouger ( yaani Kinshasa inatingishika ) ambapo Mghani au Rapa ( Atalaku ) Mwandamizi aitwae Roberto Wunda Enkokota aliutendea vyema kabla ya kumuachia Jukumu la 'Kurapu' Mwalimu Tutu Calugi na Yeye ( Roberto ) kwenda Ufaransa kutibiwa Koo lake ambalo ndiyo lilizima kabisa Safari yake ya kuwa Rapa ( Atalaku ) wa Wenge BCBG yetu hii Mkuu.
Japo kuna kina Suzuki 4×4, Bill clinton n.k Huyo Roberto Ekokota sijui kama kuna rapa yeyote anagusa hapo
 
Hivi rapa Wa Kallai Boeing ile OG ni nani!? Huwa natamani ningekuwa studio nimuone wakati anaghani
Alikuwa akiitwa Roberto Wunda Enkokota ila sasa anaumwa Saratani ( Cancer ) ya Koo na yuko nchini Ufaransa.

Baada ya tatizo lake hilo nafasi yake ndiyo ilikuja Kuzibwa vyema na Tutu Calugi ( Yombo Lumbu ) ambaye ndiyo Mwalimu wa Marapa ( Atalakus ) wengi wa Bendi za Congo DR kama vile Theo Mbala ( aliyerapu kwa Aurlus Mabele, Madilu System na Bozi Boziana ), Celeo Mozami Muviu ( aliyerapu na Werrason katika Bendi yake ya Wenge Maison Mere ) na Fusee De Gaire ambaye sasa anarapu na JB Mpiana katika Bendi yake ya Wenge BCBG akichukua nafasi ya Rapa ( Atalaku ) Marehemu Cellulaire ( Faustin Nzinga Yankobo ) akisaidiana na Atalaku ( Rapa ) Mkuu wa Wenge BCBG aitwae GENTAMYCINE ( Pitshou Lisimo ) pamoja na akina Pajo na Bin Laden.
 
Japo kuna kina Suzuki 4×4, Bill clinton n.k Huyo Roberto Ekokota sijui kama kuna rapa yeyote anagusa hapo
Rapa aliye Tishio kwa sasa ni GENTAMYCINE ( Pitshou Lisimo ) wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana japo hata akina Bill Clinton ( Mukeba Kalondji ) pamoja na Gesac aliyekuwa akirapu kwa Felix Wazekwa kabla hajahamia kwa Koffi Olomide na Bendi yake ya Quarter Latin ambapo alifanya Kazi kubwa katika Album ya Monde Arabe hasa ule Wimbo mtamu wa Respect.
 
Back
Top Bottom