Nikiwa kama Mwanayanga ambaye naichukia sana Simba SC naomba kunzia sasa Kikosi cha Taifa kiwe kinapangwa hivi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,534
Iwe ni katika Michezo ya Wachezaji wa ndani pekee (CHAN) au hata ile mingine Kocha awe anapanga hivi:

Juma Kaseja

Haruna Shamte

Gadiel Michael

Kelvin Yondan

Erasto Nyoni

Jonas Mkude

Miraji Athumani

Muzamir Yassin

Mbwana Samatta

Hassan Dilunga

Mohamed Hussein

Halafu Kipindi cha Pili awe anampumzisha Kelvin Yondan ( Mchezaji wetu Yanga SC ) kwakuwa si mzuri Kivile huku Kocha ajitajidi sana Kuwabakisha Wachezaji wote Nane wa Simba SC ( ambayo Siipendi ) waendelee Kucheza kwani japo nawachukia pamoja na Timu yao ila Kocha Etienne Ndayiragije, Juma Mgunda na Seleman Matola wakiwapanga wao Taifa Stars kila mara itakuwa inafanya vyema.

Na Kocha nae awe anapunguza au asiwe anapoteza muda wake kila mara Kuwaita Wachezaji wetu Yanga SC kwani Uwezo wao ni mdogo ukilinganisha na Uwezo wa Wachezaji Nane wa Simba SC walioitwa Taifa Stars ukilinganisha na Wetu Watano tu wa Yanga SC ambao wameitwa nahisi kwenda tu Kujaza nafasi na Kula Posho za bure za TFF.

Wenu mwana Yanga SC Mtiifu An Eagle.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom