KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 30,263
- 69,504
Hii imekuwa ni moja kati ya dhana ambayo sijaielewa vizuri,iko hivi imekuwa ikisemekana kwamba mtu akiweza kusafiri kama speed ya mwanga unavyosafiri basi ataweza kudhoofisha/kusimamisha umri wake! means kama atasafiri kwa spidi ya mwanga akiwa na miaka 20 hata akirudi hapa duniani ikiwa imepita miaka 100 toka aondoke atarudi vilevile na miaka 20 bila kuzeeka!
sasa nachotaka mimi kujua ni nini kinaathiri mwili mpk umri usisonge..?
au ukisafiri kwa spidi ya mwanga nini kinatokea kwenye mwili mpk kusababisha umri usisonge..?
ni hicho ndicho nachokitakia ufumbuzi kwa anaejua anijuze ili nielewe,mengine tutaendelea kujuzana kadri mjadala utakavyokuwa
karibuni