Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 19,408
- 25,926
Tanzania inahitaji wakina Magufuli wengine wengi zaidi.Habari!
Kwakuwa jf ni huru sidhani kama uzi huu uliojaa mawazo huru usio na kejeli wala matusi sitarajii kwamba utafutwa.
Nikiulizwa Magufuli ameacha nini kwa Watanzania, pasi kupapasa nitajibu kuwa "Magufuli ameacha hofu kwa Watanzania, itachukua miaka mingi sana kuipndoa".
Watanzania katika serikali za awamu ya 1, 2,3 na 4 kidogo walikuwa watu wanaozifahamu haki zao na wakati mwingine walithubutu kuzidai kwa nguvu walipoona zinacheleweshwa na wenye mamlaka.
Ila tangu Magufuli aingie madarakani ile style yake ya kuwaminya waliojaribu kuinunua shingo zao imeleta athari kubwa kwa Watanzania.
Sasa hakuna mtu tena wa kuweza kuipinga serikali kwa vitendo.
Watanzania wamepandikizwa woga.
Nakumbuka mkwara aliowapigia wanafunzi wa UDSM endapo wataandamana, naukumbuka mkwara aliopigwa Majaliwa endapo ndugu zake wataandamana. Na kumbuka pale alipokuwa akitumia neno fyokofyoko akimaanisha uchochezi.
Watumishi walikuwa wapole kwa miaka yote 6 huku wakisubiri Mungu aongee na Rais juu ya hatma yao.
Hii hofu haitafutika hivi karibuni. Si mmeona tozo zilivyoingizwa kikatili ila wananchi wakaishia kulia mitandaoni tu.