Nikitumia jina la mama yangu Kama ubini je ni kosa kisheria?

Samawia

JF-Expert Member
Dec 6, 2017
594
458
Namjua baba yangu,ila kutokana sababu ambazo siwezi kuzisema hapa baba yangu akaachana na mama na akanikana mimi milele. Tangu hapo nikaacha kutumia majina ya baba nikawa natumia majina ya mjomba.

Sasa kwenye kitambulisho cha taifa nataka nitumie jina la mama yangu tu.

Samawia Nasm,je inakubalika kisheria?
 
Kama walikupata ndani ya ndoa...usibadili...tumia jina la baba...lakini kama ni nje ya ndoa tumia jina la mama ako...una haki zote kabisa...
 
Kama walikupata ndani ya ndoa...usibadili...tumia jina la baba...lakini kama ni nje ya ndoa tumia jina la mama ako...una haki zote kabisa...
Nje ya ndoa katika mahusiano ya kudumu ila yasiyo rasmi,baba alijitambulisha kwa akina mama nikiwa na miaka mitano
 
Namjua baba yangu,ila kutokana sababu ambazo siwezi kuzisema hapa baba yangu akaachana na mama,na akanikana mimi milele,tangu hapo nikaacha kutumia majina ya baba nikawa natumia majina ya mjomba,Sasa kwenye kitambulisho vya taifa nataka nitumie jina la mama yangu tu.
Samawia Nasm,je inakubalika kisheria?
Jina lolote sio baya ili mradi wewe umekubaliana nalo. Unaweza pia tumia majina yako yote. Mfano, Samawia Nasma Samawia.
 
Tumia jina uliloandikiwa kwenye cheti cha kuzaliwa, ukibadilisha uende na kiapo cha hakimu au mwanasheria ili lionekane kuwa ndio jina lako, ila km unaitwa Hashim Athumani Sele ukasema Sele silitaki nataka niweke Juma lisomeke Hashim A Juma na kwenye cheti hujaandikwa hivyo wala huna cheti cha kiapo itakukosti utaonekana umefoji
 
Kubadili jina inaruhusiwa unaweza hata ukatunga lakwako mwenyewe ila lazima uwe na cheti cha kiapo (affidavit) km jina hilo linatofautiana na jina ulilopewa kwenye cheti cha kuzaliwa, ndio maana unaambiwa uende na cheti cha kuzaliwa
 
Hakuna shida bro. Ilimradi hayagongani na majina yaliyo kwenye document nyingine muhimu kwani utapata tabu sana yakiwa tofauti.
 
Jina lako la Baba na la Babu au ukoo.
Unaweza kufuata family tree ya babu mzaa mama, Lakini family tree ya Baba yako ndio ukoo wako!! (DNA) Blood streem ya ukoo unapata family name!!
 
Baba alipandikiza mbegu mkuu,baba ni baba na mama ni mama;kutokuitwa jina lake hakukuondolei kutokushea mbegu zake;kuhusu majina ni mbwembwe tu...unaweza kutumia lolote kutokana na nafsi yako.
 
Back
Top Bottom