Nikitoka nchini kwa njia za panya, nakuwa nimefanya kosa kwa nchi yangu au ile ninayoenda?

Habari wandugu. Hivi eti nikitoka hapa na kwenda labda Zambia. Sina cha passport wala cha Visa, nakuwa nimetenda kosa kwa nchi gani, Tanzania au Zambia?
Zambia unaweza kwenda kwa passport ya karatasi kwa nini uitafute jela kizembe hivyo Mkuu nenda uhamiaji wakupe mchelemchele huo Zambia ni wakali kuhusu vibali kuliko maelezo...
 
Zambia unaweza kwenda kwa passport ya karatasi kwa nini uitafute jela kizembe hivyo Mkuu nenda uhamiaji wakupe mchelemchele huo Zambia ni wakali kuhusu vibali kuliko maelezo...
Hiyo passport si ndiyo nasikia ina bonge la mlolongo kuipata?
 
Kwa uelewa wangu na uzoefu, nchi uliyoingia kinyemela inatakiwa ikufanyie deportation ili ukashtakiwe kwenye home country.

Nchi yetu haijazingatia hili ndio maana mahabusu wa kiethiopia wamejazana Segerea bila kurudishwa kwao ilhali nchi kama S.A huwa zina wa deport wabongo na huwa wanafikia Kisutu.

Kulingana na utaratibu wa nchi yetu, ni wazi kabisa kuwa justice system haiwatendei haki mahabusu wa kihabeshi.
 
Unakua umefanya makosa kwenye nchi zote.

Kwenye nchi wanazotumia akili zaidi watakurudisha nchini kwako ukashtakiwe huko ili wasipate gharama ya kukulisha bure. (kwa kesi yako ni kwamba ukikamatwa zambia watakurudisha Tz)

Kwa nchi wanazotumia mabavu zaidi watakufunga kwanza kisha ukimaliza kifungo chako wanakurudisha nchini kwako. Sijui kama ukirudishwa baada ya kutumikia kifungo ugenini utashtakiwa upya kwa kutoroka au vipi.
 
Habari wandugu. Hivi eti nikitoka hapa na kwenda labda Zambia. Sina cha passport wala cha Visa, nakuwa nimetenda kosa kwa nchi gani, Tanzania au Zambia?
Kama umejianda kwa kujilipua sidhani unashida kwa upande unaotoka au unakikwenda.
Kwani kwa walijipanga kujilipua huwa wanaimbaga wakamatwe ili asitumie garama kubwa njiani kwani kama uko vizuri serikali ya huko itakugaramia mambo mengi kwa hiyo ni ww tu umejipangaje
 
Sina ujuzi sana na hili, ila chukulia mifano hai ya wale wakamatwao let say south africa, hukamatwa kule wakawekwa lupango na baadae husafirishwa na wafikapo hapa hupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kwa utoro.
Wengi wanaorudishwa huwakujipanga kwani utaishi ktk Nchi za watu ueleweki mpango wako
 
Kwa uelewa wangu na uzoefu, nchi uliyoingia kinyemela inatakiwa ikufanyie deportation ili ukashtakiwe kwenye home country. Nchi yetu haijazingatia hili ndio maana mahabusu wa kiethiopia wamejazana Segerea bila kurudishwa kwao ilhali nchi kama S.A huwa zina wa deport wabongo na huwa wanafikia Kisutu. Kulingana na utaratibu wa nchi yetu, ni wazi kabisa kuwa justice system haiwatendei haki mahabusu wa kihabeshi.
Kinachowakamatisha hawa Waethipia ni kwamba wao waenda South wakati Documents zao hazipo kamili

Wataka hilo lisiwatokee waseme wamekimbia Nchini mwao kama Wakimbizi kwa hiyo wanatakiwa waombe Ukimbizi hapa kwanza then watapelekwa ktk kambi za ukimbizi baada ya hapo wataangalia namna ya kuondoka kwenda huko South.

Kwa wale Watz waliosafiri zamani wanajua hii stail mfano Watz wengi waliopo Nchi yoyote duniani wengi wao waishi kama Wakimbizi na hawaishi kama Wakimbizi wa Nchi zenye migogoro kama Kongo na Nchi nyingine zenye migogoro.

Kwani cha muhimu ni kujua vizuri complain ya Nchi unayoiplenia yaani mipaka yake Miji yake ikiwezekana hata Lugha pia.

Kuna Jamaa mmoja South alikuwaga na complain ya Angola lakini ni mtz wa Ilala na Kireno anakijua na miji anaijua alikamatwa akarudishwa Angola na walimpokea kama raia ambaye sio Mwangola
 
Back
Top Bottom