Nikitaka kuelekeza mahali nitakapopenda msiba wangu na mazishi yangu nifanyeje?

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
342
Sina uelewa sana kuhusu mambo ya wosia. Ila niliona Rais Aboud Jumbe ilitarifiwa kwamba aliandika wosia kuelekeza namna gani angependa kuzikwa.

KWenye ukoo wetu kumekuwa na ubishi wa kugmbania msiba na hata mazishi. Mimi niataka nikomeshe huu ubishi kwa kuandika wosia unaoelekeza nikifa nizikwe wapi na msiba ufanyikie wapi na vipi.

Siyo kwamba ninakaribia kufa bali ni kutokana na ukweli kwamba siijui siku yangu ya kufa kama ni kesho, mwaka kesho au decade ijayo.

Sitaki ndugu wachukue nafasi ya kutokuwepo wosia ili kugombania kupata umaarufu wa msiba wangu wakati wengine tulishakosana miaka 20 iliyopita halafu eti nikifa waje warundikane na kugombania mazishi yawe wanapopata wao.

Kuna mahala na namna ambavyo ningependa msiba wangu na mazishi yangu viwe ninavyotaka mimi, tena kimaandishi.

Je, hilo linawezekana, na kama linawezekana nichukue taratibu zipi?

Je, na nikiishafanikiwa kuurasimisha huo wosia kisheria, je ninapaswa kuusambaza kwenye ukoo wangu kumaliza ubishi na kiburi cha wanaukoo?
 
Daaa mi mwenyewe napenda Man Nikifa nichomwe moto sitaki kufukiwa niliwe na funza nawaza sana sijui wosia ntauejaje ili ufike siku yenyewe mwenye uelewa wa haya mambo atueleweshe maana binadamu wa leo wabishi kweli unaweza ukazikwa ata na manispaa
 
inawezekana fuata taratibu za kisheria.lkn haya mambo ni ya kiimani zaidi ukifa ya dunia unayaacha ukuuku autajua kama wametimiza matakwa yako.
 
Tafuta Mwanasheria Andika Wosia Unataka Kuzikwa Vipi. Au Ita Kikao Na Ndugu Waambie Ikitokea La Kutokea Unatakaje
 
andika wosia na upeleke kwa mwanasheria upigwe mhuri.pia umuachie copy.

mkuu uko wapi nataka ukifa niwe wa kwanza kusema ulijitabiria
 
Back
Top Bottom