Nikitafakari ya Nelson Mandela napata picha maumivu ya usaliti yanavyouma.

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,014
Alipofungwa miaka 27, alikuwa tayari na akawasamehe waliomfunga miaka yote. Mke wake, winne/winnie alihangaika kwa kuendesha harakati za kisiasa kumnasua mumewe gerezani na kupigania uhuru wa mtu mweusi. Ikapelekea hata winne kukamatwa na kufungwa zaidi ya mara 23.

Lakini alipotoka gerezani, Mandela aliwasamehe waliomfungwa miaka 27 ila alishindwa kumsamehe mkewe aliyehangaika miaka yote, kwa kosa moja tu, USALITI WA NDOA!

Huwa inanipa wakati mgumu sana kufikiria changamoto za maisha ya ndoa.
 
Waafrika wanafiki sana eti ameweza kusamehe wazungu waliotoa uhai wa mamia ya watu akashindwa kumsamehe mke wake kwa kukazwa tu ndio maana wazungu wanatuona mabwege
Vipo vya ku share lkn cio mapenzi
 
Ndoa ni shida, inahitaji uvumilivu uliotukuka.
Mandela alikaa jela miaka 27, akatoka akakaa ktk ndoa yake na Winnie chini ya mwaka, ikamshinda!
27 ya jela kwa miezi kadhaa ya ndoani tu.
 
Kitendo cha kuwasamehe naona kina ugumu kukipima kwa sababu je asingewasamehe angewafanya nini, ambacho kinatufanya sasa tuseme kweli kawasamehe? Angesema awafukuze au aanze kuwafunga hovyo... No, Mandela hakuwa finyu kiasi hicho. Ukisema awabague No, yeye ndio kioo cha kupinga ubaguzi. Yaani utakuta inabaki kuwa kisiasa zaidi lakini moyo wake ndio unaujua ukweli kama kawasamehe. Kumbuka wamemharibia maisha yake yote. Kufungwa Miaka 27 ya ujana wako ni kama tu kusema Mandela hakuishi /hakufurahia kuishi. Ndio maana hakupenda hata kukaa madarakani muda mrefu maana ukiwa Rais pia huishi maisha yako.
 
Kosa la winnie kwa mandela halikuwa la kumsaliti kwa kutembea na mwanaume mwengne, mrs ex mandela alikua na kosa la mauwaji alimuuwa kijana mdogo sana kwa hyo kutokana na wadhifa alokua nao mandela wakati ule sheria ilimbana lazima amuache na winnie Mandela alienda jela mwaka 1 kwa kosa la mauwaji, kwa hyo Mandela hakutaka amuache ila ilimlazimu amuache
 
sio hoja ya msingi sana, na ukipata bahati soma hata hukumu ya kesi yake, au tafuta kisa cha mauaji hayo ktk gazeti la raiamwema, sikumbuki toleo gani. Ila ni la 2014. Haikuwa kweli. Msingi mkuu na sababu hasa, mzee alimwacha winnie kwa usaliti, winne alikuwa anadate na mpigania uhuru wa ANC, Kijana mdogo, Dali Mpofu.
 
wanaume wenyewe ni wasaliti sana tunawavumilia mengi lkn huwa hawanaga uvumilivu wala moyo wa kusamehe wenyewe wakisalitiwa.
 
mkuu acha masihara na kusalitiwa... kinachotuumiza zaidi ni ule ufundi na mitindo tunayopewa kitandani. kila nikiwaza hata mwenzangu amepewa kama ninavyopewa.Huwa inauma
 
mkuu acha masihara na kusalitiwa... kinachotuumiza zaidi ni ule ufundi na mitindo tunayopewa kitandani. kila nikiwaza hata mwenzangu amepewa kama ninavyopewa.Huwa inauma
Hahahahahahahaha kizuri kula na mwenzio.
 
Back
Top Bottom