Nikisema viongozi wa dini ni wanafkini ni kosa kwa hili?

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,220
368
Wana JF,

Kwanza natanguliza samahani kwa wale ntakao kuwa nimewakwaza ila inanibidi nisema hili kwani linanigusa sana,

Moja Kabla ya Uchaguzi kulizuka sana minong'ono kuwa kuna UDINi basi hapo viongozi wa madhehebu mengi wakapiga vita kuuhusu ilo swala la UDINI na Kuhubili AMANI na wakasahau kuhubiri HAKI kwa hali na mali sasa baaada ya Uchaguzi kuisha basi hakuna tena wa kumshauri Rais Aliye Apishwa JK Mrisho kuwa sasa anatakiwa kuchagua baraza lake la Mawaziri kwa kuzingatia uadilifu wa viongozi atakao wateuwa kuwa mawaziri wasio na kashfa au tuhuma zozote eg UFISADI.

Pili viongozi hawa wa dini hawajamwambia Rais asimamie HAKI na usawa na ita leta AMANI.

Matokeo yake baada ya Rais kuapishwa basi Viongozi wote wa DINI kimya sijasikia hata mmoja akitoa tamko lolote kumweleza Rais.

Je huu ulikuwa ni unafki tuu wa kujikosha au ulikuwa ni uoga wa kutokea machafuko???? Sasa hapo nini wanacho tetea kwa wananchi katika serikali yao??
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,317
10,298
Mkuu samahani: Hivi viongozi wa dini wana sauti juu ya maamuzi yeyote anayotaiwa kuyafanya mhishimiwa Rahisi?

Yaani kikatiba hilo suala linakubalika au?
 
Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,237
317
Mkuu samahani: Hivi viongozi wa dini wana sauti juu ya maamuzi yeyote anayotaiwa kuyafanya mhishimiwa Rahisi?

Yaani kikatiba hilo suala linakubalika au?

Hawana sauti kikatiba ila huwa wanatumiwa na wanasiasa kwa matashi ya kisiasa kwa ajili ya kujihalalishia madudu yao
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,959
3,292
Mkuu nakubaliana nawe viongozi wengi wa Dini Tanzania ni wanafiki, kwasababu zifuatazo:

  • Kabla ya uchaguzi walikuwa wakidai wanaombea nchi ifanye uchaguzi kwa AMANI,
  • Mara baada ya uchaguzi wenye mashaka, kasoro nyingi, wizi wa kura nk. wao walipaswa kutoa tamko kwa NEC kuitaka iharakishe kutoa matokeo ili kupunguza MUNKARI na hasira za wapiga KURA. Lakini hawakufanya hivyo!!
  • Matokeo yalipotoka walipaswa kwenda kuwaeleza ukweli TUME kuwa, wamefanya mchezo mchafu wao pamoja na CCM
  • Mwisho, viongozi hao hao wa DINI walipaswa kuwa wakwanza KUPINGA matokeo ya NEC na kuomba Serikali pamoja na Mamlaka husika kuunda TUME huru, ili kuchunguza mchakato mzima wa uchaguzi toka Daftari la Wapiga KURA, vituo vya kupigia KURA na hadi Zoezi la Kuhesabu na Kutangazwa kwa matokeo. Lakini wao wakawa/wako kimya hadi sasa.
Mkuu, kweli ni Wanafiki wametumiwa na CCM kama DELILA alivyotumiwa na WAFILISTI.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
wafuasi ndo wanafiki kuliko hata hao viongozi.

Mfuasi hakumbuki lini mara ya mwisho ameenda kanisani au msikitini wala hakumbuki mara ya mwisho alofungua bible au msahafu, lakini yupo tayari kuchagua kiongozi kwa dini yake tu.

Bora hata hao atheists wanaweka wazi hadharani kuwa hawaamini mungu kuliko ya wafuasi wanafiki.
 
Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
142
Naunga hoja mkono. Ni wanafiki na hawafai kuitwa au kuongoza wateule wa Mungu. Unafiki wao umezidi mipaka hasa kwa dini za kikristo. Ebu fikiria Baba Askofu wa Singinda anaenda kumwomba Tindu Lisu awazuie washabiki wake wasisherekee ushindi kwa sababu atawahumiza moyo walioshindwa..... ni wangapi katika majimbo yote wameshindwa na sherehe za walioshinda zilikubalika? Uozo huu umeanza kufanya hata maudhurio makanisani kupungua.
Kama wamo viongozi wa Dini hapa JF basi wajirekebishe!!
 
emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,743
3,033
Mi ni mmojawapo niliyepunguza maudhulio kanisani kwa kuwa they can no longer be trusted

Niliwahi kuwasilisha hapa JF kwamba mkazo wa viongozi wa dini upo kwenye amani na sio haki. Tha's absolutely ridiculous. Amani inayopatikana bila haki ni amani ya kinafiki.
 
Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,259
2,124
Wana JF,

Kwanza natanguliza samahani kwa wale ntakao kuwa nimewakwaza ila inanibidi nisema hili kwani linanigusa sana,

Moja Kabla ya Uchaguzi kulizuka sana minong'ono kuwa kuna UDINi basi hapo viongozi wa madhehebu mengi wakapiga vita kuuhusu ilo swala la UDINI na Kuhubili AMANI na wakasahau kuhubiri HAKI kwa hali na mali sasa baaada ya Uchaguzi kuisha basi hakuna tena wa kumshauri Rais Aliye Apishwa JK Mrisho kuwa sasa anatakiwa kuchagua baraza lake la Mawaziri kwa kuzingatia uadilifu wa viongozi atakao wateuwa kuwa mawaziri wasio na kashfa au tuhuma zozote eg UFISADI.

Pili viongozi hawa wa dini hawajamwambia Rais asimamie HAKI na usawa na ita leta AMANI.

Matokeo yake baada ya Rais kuapishwa basi Viongozi wote wa DINI kimya sijasikia hata mmoja akitoa tamko lolote kumweleza Rais.

Je huu ulikuwa ni unafki tuu wa kujikosha au ulikuwa ni uoga wa kutokea machafuko???? Sasa hapo nini wanacho tetea kwa wananchi katika serikali yao??

Viongozi wa dini wako katika hali ngumu kweli: wakifanya hivi wanaambiwa wanaingilia siasa au wanachanganya dini na siasa. Wasipofanya kitu, wanalaumiwa na kuambiwa ni wanafiki. Sasa wafanye nini? Inabidi wao wenyewe waone ni kipi wafanye au wasifanye kwani kwa lolote watakaloamua kufanya watalaumiwa tu!
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,622
Jethro,
Mkuu wewe ndio umewashitukia leo?...Dini na siasa huleta Udini hakuna jingine, sasa wamerudi kujipanga kutafuta tax excemption
 
Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
16
Kwani ni lini viongozi wa dini waliacha kuwa wanafiki - wamekuwa hivyo tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Wengi wao hutumia dini kwa masilahi yao na ni nadra kwao kupingana na anayetawala kwani kwa kufanya hivyo watahatarisha 'ulaji' wao. Hili halina ubishi!
 
sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
20
Mie nafikiri wapigwe marufuku kushiriki siasa katika namna yoyte ile,huu udini unaoonekana kupigiwa kelele wameuleta wao na ccm.2005 Kilaini alisema JK rais chaguo la Mungu watu wakakaa kimya,kipindi hiki kaja Slaa wakazua udini kisa kapata support kutoka kwa viongozi fulani wa dini.Sioni sababu ya yote haya,taasisi za dini zisijihusishe kwa vyovyote vile na mambo ya siasa.
 
In Focus

New Member
Nov 11, 2010
3
0
Mi ni mmojawapo niliyepunguza maudhulio kanisani kwa kuwa they can no longer be trusted

Niliwahi kuwasilisha hapa JF kwamba mkazo wa viongozi wa dini upo kwenye amani na sio haki. Tha's absolutely ridiculous. Amani inayopatikana bila haki ni amani ya kinafiki.

Huna tofauti na anaekataa shule kisa walimu ni wezi, mbumbumbu. Kama unadhani utaishi milele acha dini.
 
Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,220
368
Viongozi wa dini wako katika hali ngumu kweli: wakifanya hivi wanaambiwa wanaingilia siasa au wanachanganya dini na siasa. Wasipofanya kitu, wanalaumiwa na kuambiwa ni wanafiki. Sasa wafanye nini? Inabidi wao wenyewe waone ni kipi wafanye au wasifanye kwani kwa lolote watakaloamua kufanya watalaumiwa tu!

Ni Bora wawe Baridi au Moto Kuliko kuwa vuguvugu

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom