Nikirudi nyumbani nisipokuta chakula tayari inanikera sana

Huaga siamini haya niyaskiayo, yaan mtu ameshnda home tangu kumekucha na haumw lkn hapiki mpka unaporudi!? Inashangaza mnooo, sjawah kuliamini hili swala. Na pesa ya chakula umetoa na bado mtu hapiki............mnawapataga wap hao wake zenu 🤔🤔🤔🤔​
Sisi tunapenda wanawake warembo haswaa. Na sasa hao ndio wako namna hiyo. Na kama si mrembo, binafsi hata sina hamu ya penzi.. na sitaki kuoa mke ambaye sina hamu na penzi lake.
 
Hilo si la kudumu maisha yote ya ndoa mwanamke anayejielewa atarekebisha ratiba. Hakuna mwanamke anayependa mwanaume asile chakula anachoandaa.
Sio kweli. Tena siku izi ni house girls ndio wanaofanya kazi zote pamoja na kupika na kulea watoto
 
Zamani wazee wetu waliweka sheria na ndoa zikadumu lakini saivi tunaenda kienyeji ukija hujui baba nani mama nani wote wamevaa mibano na kuvaa hereni heshima itatoka wapi?
Siku izi ukiweka sheria, wanasema unawaonea. Wanasema haki za wanawake..
 
Sio kweli. Tena siku izi ni house girls ndio wanaofanya kazi zote pamoja na kupika na kulea watoto
Na sio kweli kwamba kwenye ndoa zote wanaoandaa chakula ni dada wa kazi. Wapo wanawake ambao licha ya udhaifu wao kama binadamu hawapendi dada wa kazi aandae chakula cha waume zao
 
Ndio umuhimu wa makungwi na manyakanga unapokuja. Zamani kulikua na "semina elekezi" za kiasili kabda ya ndoa ili kuwapa wanandoa watarajiwa shule kuhusu maadili, majukumu, haki na wajibu wao katika ndoa

Siku hizi watu wamekua wajuaji sana. Zile taratibu za wazee wetu zinaonekana zimepitwa na wakati! Mume anaweza kurudi kutoka kazini anaingia ndani mkewe utakuta kakaa anaendelea na kazi zingine au anapiga soga tu

Toka mdogo nakua nikiona baba akirudi home bi mkubwa hata kama alikua na shughuli gani lazima ataacha na kumfuata mshua ndani

Huko kuchelewa kupika nako ni kero nyingine kubwa. Na bahati mbaya pamoja na stlye ya maisha (wakati mwingine utakuta labda both ni wafanyakazi wanarudi late wich is understandable) vinavyowachelewesha ni uvivu au tamthilia za kina Kurfi, Artuglu na nini sijui! Tena wanajua kabisa kua unakereka😀😀😀
Na ndio maana ndoa hazidumu kabisa. Yani watu waliooa ni ma-stress kila siku. Ni wa kuhurumia kweli kweli.
 
Na sio kweli kwamba kwenye ndoa zote wanaoandaa chakula ni dada wa kazi. Wapo wanawake ambao licha ya udhaifu wao kama binadamu hawapendi dada wa kazi aandae chakula cha waume zao
Wachache sana wako hivyo siku izi. Hiki kizazi cha facebook, insta, tiktok na youtube.. watashinda huko mitandaoni zaidi
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unataman ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakin ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawil mbele dah!
Mnyang'anye smartiphoni atastaarabika
 
Hongera. Lakini ukweli ni huu,kuna wanawake ni afdhali uishi na kuku. Maana kuku hujali sana ratiba ya kuingia na kutoka bandani au juu ya mti.

Muda wa mwanaume kutoka kazini, yeye atakuwa saloon kwa rafiki yake wanagonga story. Ndo kwanza anamsaidia rafikiye kuchagua mchele ampikie mumewe wakati kwake kumenuna.

Wanawake wa aina hii wako wengi sana. Nj siri za wanaume ndizo huwafanya waonekane wanawake.
Hujakosea. WAKO WENGI SANA SIKU HIZI. NA NDIO MAANA WATU TUMEGOMA KUOA..
 
Sisi tunapenda wanawake warembo haswaa. Na sasa hao ndio wako namna hiyo. Na kama si mrembo, binafsi hata sina hamu ya penzi.. na sitaki kuoa mke ambaye sina hamu na penzi lake.
Bas muwe wavumilivu msje kutulilia huku, na kutujumuisha "oooh wanawake wamefanya haya oooh wamefanya yale". Hahahahahahah! Kweli ukiyastaajabu ya Musa utayaona ya Farao, baadae "ooh wanaume tunakufa mapema, wanawake wanabaki" mnavumilia mshumaa uishie kiganjani​
 
bora hivyo anaanza kupika
Wangu ndo kwanza anakuuliza tupike nini MUMEWANGU

Amna swali linaloniudhi kama hilo Tupike nini mumewangu

huwa sijibu natoka zangu nje tu kupunga upepo na anifati tena 7bu anajua kashanivuruga
lakini cha kushangaza baada siku 2 anarudia tena hvyohvyo
Nishasema weee nimechoka
Mbona haya mambo ni ya kuongea tu?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom