Nikirudi nyumbani nisipokuta chakula tayari inanikera sana

Hongera. Lakini ukweli ni huu,kuna wanawake ni afdhali uishi na kuku. Maana kuku hujali sana ratiba ya kuingia na kutoka bandani au juu ya mti.

Muda wa mwanaume kutoka kazini, yeye atakuwa saloon kwa rafiki yake wanagonga story. Ndo kwanza anamsaidia rafikiye kuchagua mchele ampikie mumewe wakati kwake kumenuna.

Wanawake wa aina hii wako wengi sana. Nj siri za wanaume ndizo huwafanya waonekane wanawake.
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unataman ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakin ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawil mbele dah!
kazini kwako wakufuruge kichwaa,hata bebi akufuruge ubongo BEER TAMUUU ,Nikupitia Bar tu ..........Ila Cha msingi tuwavumilieni hayo Ni madhaifu yap
 
Hapo ni kuweka sheria tu ukifika mda huu chai bado sinywi ikifika muda huu chakula bado sili tena ikifika usiku hivyo hivyo
Lakini na ww uhakikishe kila kitu kipo ndani unga mchele mafuta sio unarudi ndio utoe hela ya unga halafu Unalalamika msosi unachelewa

Kuoa ni kukaribisha umasikini
 
Hii kauli hata mimi ilikuwa inanikera ,yaani uumize akili kutafta hela ,Pia ufikirie cha kupika wakati yeye ndo mama mwenye nyumba Aisee mimi nilipigana sana na hii kauli mpaka sasa haniulizi maana sina muda huo wa kuwaza chakupika ni jukumu lake ,jukumu langu nikutafta pesa tu
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unataman ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakin ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawil mbele dah!
Kwani mlilazimishwa kuoa? Vuneni mlichopanda na pambaneni na hali zenu. Ndio wanawake wa leo walivyo ivyo. Na ukifulia hata nyumbani ukirudi hautamkuta.
 
🤣🤣 hivi mbona mnatutisha ambao hatujaoa! Kumbe hizo ndo kila rangi mnazoona..!! Dah! Maisha haya hatari sana.
Hakuna mke wa kuoa siku izi. Hasa kwa sisi tunaopenda warembo.. wanajikuta sana hao watu..
 
bora hivyo anaanza kupika
Wangu ndo kwanza anakuuliza tupike nini MUMEWANGU

Amna swali linaloniudhi kama hilo Tupike nini mumewangu

huwa sijibu natoka zangu nje tu kupunga upepo na anifati tena 7bu anajua kashanivuruga
lakini cha kushangaza baada siku 2 anarudia tena hvyohvyo
Nishasema weee nimechoka
Kwani mlilazimishwa kuoa? Vuneni mlichopanda na pambaneni na hali zenu. Ndio wanawake wa leo walivyo ivyo. Na ukifulia hata nyumbani ukirudi hautamkuta.
 
Ni mwanaume asiyejielewa pekee anaweza kuanika udhaifu wa mke wake mtandaoni


Tujifunze, siri za ndani hazifai hata kufika sebuleni, tuzimalize ndani kwa ndani

Wanawake ni waelewa sana ukienda nao kwanza kwa kuwatibu kisaikolojia. Nenda nae taratibu, mweleweshe atakuelewa. Yamkini tabia hii alijijengea mwanzo mlipooana/kuanza kuishi pamoja na hukuikemea, akachukulia kama ndo lifestyle unayopendezwa nayo


Jifunze ulikosea wapi, then rekebisha makosa yako/Yenu

Tena hapa kwa sababu tupo mwisho wa mwaka, pangeni pamoja mipango yenu ya mwaka kesho, na hilo liwe moja ya ajenda yenu

Ova
Kwani amemtaja jina? Na yeye si anonymous? Ni vizuri watu ku-share changamoto kama hizi ili watu wajifunze kwa wengine.
 
Enzi za shule uteseke kama hivyo unarudi zako shule unanjaa unapita jikoni unakuta hakuna dalili ya kuni kupasuliwa na majivu yamepoa kabisa, ukiuliza una ambiwa hapa ni kwako! 😀😀😀

Halafu kwenye ndoa unakutana na same experience!
Ndio wanawake wa leo walivyo ivyo. Na ukifulia hata nyumbani ukirudi hautamkuta.
 
Mkuu mzoea unayaweka wewe,, weka sheria mkuu Kama unatoka kazini target yako nyumbani ufike saa mbili usiku,, inabidi uweke sheria kuwa ikifika saa mbili kamili unataka chakula kiwepo mezani hivyo yaani maana bila sheria hawawatu saingine wanajifanya filamu ni ya muhimu kuliko Mume
Wanawake wa siku hizi, atakutetemekea ivyo kama una $$$ nzuri kweli kweli. Ama sivyo, sheria zako anaziona za kizuzu tu. Na ukimletea za kuleta, anakutaftia mume mwenza asiyemwekea sheria kali kama zako.
 
Back
Top Bottom