HAPO JUU NI Godfrey Madaraka Nyerere (kushoto na Jaffar Remo Amin
walipokutana Butiama April i2009. Kwa mkoa wa Kagera wakisikia mtu anatamka IDD Amini baadhi wanakimbia ....Sasa hawa baadhi ya vijana wa Nyerere wanaotaka kurudisha uhusiano wanasahau vidonda vya diktator huyo? Mbona Jaffar hakuja wakati Nyerere akiwa hai?
Hakuna kitu nyerere alitaka kutawala east africa yote na obote alikubali hivyo kuingia kwa idd amin madarakani ikawa kikwazo ndio tz tukaenda vitani bila ya sababu!
Hakuna kitu nyerere alitaka kutawala east africa yote na obote alikubali hivyo kuingia kwa idd amin madarakani ikawa kikwazo ndio tz tukaenda vitani bila ya sababu!
Kwa kifupi, Rais Obote, aliangushwa na kamanda wa jeshi lake, Jenerali Idd Amin Dada, Januari 25, 1971, akiwa nchini Singapore, kuhudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Madola. Rais Nyerere alimpa hifadhi ya kisiasa.
Lakini Bwana Obote alikuwa na wafuasi wake huko Sudan. Hawa walikuwa na lengo la kuiangusha serikali mpya, kwa nguvu za silaha, ili Bwana Obote aweze kurejea madarakani.
Muda si muda, Sudan ilibaini kuwa kufanya hivi ni kukiuka lengo na madhumuni ya OAU (sasa AU). Isitoshe, ilikuwa dhahiri kwa uongozi wa Sudan kwamba, kusaidia wafuasi hawa wa Bwana Obote, kungelihatarisha usalama wa Sudan na raia wake; pengine hata kuathiri usalama wa mataifa ya jirani. Kwa kuzingatia hayo; kati ya mambo mengine; serikali ya Sudan iliamua kuwanyima ruksa wafuasi Bwana Obote, kuendesha shughuli zao kutoka nchini Sudan.
Ni katika hatua hii, uongozi wa Tanzania ulipoamua kuwakaribisha hapa kwetu. Walipokuwa hapa, wakapewa silaha na mafunzo ya kijeshi, hatimaye wakaruhusiwa kuanza mashambulizi kusini mwa Uganda, kupitia Mkoa wa Kagera (rejea makala ya The Times hapo chini. Uk.2 paragrafu ya 2, kutoka chini).
Ushambulizi huu uliendelea kwa muda. Lakini la muhimu ni kwamba, washambulizi hawa walipolemewa na nguvu za jeshi la Uganda, kila lilipojibu mashambulizi yao, ilibidi warudi tena (sema walikuwa waki retreat) Tanzania, kupitia njia hiyo hiyo (i.e. Kagera), waliyoitumia kufanya mshambulizi hayo.
Ni katika hatua hii Idd Amin alipoamua kuvamia, na kuteka sehemu ya Kagera (baada ya kulivunja daraja linalounganisha sehemu hiyo na Tanzania). Katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni wazimu, Amin, alidhani angelikaa kwenye eneo alilolivamia ili kuzuia mashambulizi zaidi kutoka Tanzania. Ni hapa alipomeza ndoana.
Kwani, uongozi wa Awamu ya Kwanza, ulikuwa ukimsubiri Amin afanye hivi, ili upate kisingizio cha kumuangusha Amin ili rafiki ya uongozi huo, Obote, arejeshwe madarakani. Hili lilifanyika, ingawaje kwa gharama kubwa sana kwa Tanzania.
Baadaye, majeshi ya Jamhuri ya Muungano yaliondolewa nchini Uganda kwa awamu. Hii ilitokana na Bwana Obote kukataa (wengine wanasema alikuwa na uwezo mdogo, kifedha) kuheshimu ahadi yake ya kuilipa Tanzania $600 milioni: gharama ya vita vya kumrejesha madarakani (tazama uk 2, paragrafu ya kwanza, ya makala niliyoyataja hapo juu).
Lakini kutokana na vita hivi, hali ya kiuchumi nchini Tanzania ilikuwa ngumu mno. Ugumu huu, uliwafanya baadhi ya vijana wakati huo kuhoji kama kuwepo kwa majeshi ya Tanzania katika mataifa matano, kwa wakati mmoja (wakati wa vita hivi, majeshi ya Tanzania yalikuwa nchini Msumbiji, Ushelisheli-Seychelles-na visiwa vya Komoro; na jingine hapa nyumbani, kulilinda Taifa), kulienda sambamba na maslahi ya Taifa.
Kwa mfano, haikueleweka (na kweli, hadi leo haieleweki) kwa nini nchi hizi, hazikulipa gharama za majeshi yetu kuwepo nchini mwao kwa vile, kinadharia, ni nchi hizi zilizokuwa zikifaidika, kiulinzi, na kuwepo kwa majeshi yetu nchini mwao.
Wengine walihoji kwa nini Tanzania igharamie vita vya Uganda, lakini ujenzi (reconstruction) wa Uganda baada ya vita, ifanywe na wengine ambao hawakushiriki katika vita hivyo; ujenzi uliofanywa kwa kutumia vifaa na kampuni za ujenzi za mataifa hayo na siyo vifaa au makampuni ya Kitanzania? Je! jambo kama hili lilikuwa likidhoofisha au kuimarisha uchumi wa Jamhuri ya Muungano?
Pengine Tanzania haikuwa na fedha za kuikopesha Uganda, ili Uganda nayo iweze kununua vifaa na, au, kutumia kampuni za ujenzi kutoka Tanzania. Lakini hili, kwa kwa baadhi ya vijana wakati huo, hawakuelewa (au hawakueleweshwa) kwa nini jambo hili halikufikiriwa kwa kina kabla ya uamuzi wa kuyasaidia majeshi ya Obote, yaliyofukuzwa huko Sudan, kufanyika.
Je! uongozi wetu wa kisiasa ulitilia maanani usalama wa raia wake (hasa wale wanaopakana na Uganda) kabla ya kufikia uamuzi huo? Je! uongozi huu ungelifikia uamuzi kama huo kama, mathlani, Kagera ingelikuwa ni mkoa ambapo uongozi huo unatoka?
Pengine uamuzi wenyewe ulichukuliwa kwa kuzingatia zaidi siasa ya wakati huo ya 'Ukombozi wa Bara la Afrika'. Lakini kwa nini iwe ni Tanzania tu, ambayo ilichukua mzigo huu wa 'Ukombozi wa Bara la Afrika' badala ya bara zima. Mtanzania wa kawaida angelifaidikaje na siasa hii?
Siyo hiyo tu, lakini kwa kawaida, watu wanategemewa kwanza kuzifikiria familia zao kabla ya kufikiria wengine (tuseme 'charity begins at home').
Haya yote yaliibuliwa na vita hivi ambavyo, kama nilivyoonyesha hapo juu, chimbuko lake ni kuruhusu majeshi ya Bwana Obote kufanya ushambuli kusini mwa Uganda, kutoka ardhi ya Tanzania. Haya ni maelezo tu, ya baadhi ya watu waliyokuwa nayo wakati huo. Uhalali wa vita hivi, au vinginevyo, ni swala la wana JF kutafakari.
Iddi Amin alikuwa mshenzi,ni sawa vita ilituweka tuwe maskini nchi yetu,ila ama kwa hakika ktk maisha yake nadhani hakuwasahau Mossad wapelelezi wa kiisrael walipokuja kuokoa mateka wao pale Entebbe 1976(Operation Entebbe),Hadi akanza kuua wazungu na wakenya waliokuwa wakiishi Uganda akiamini ndio waliwasaidia waisrael kuokoa raia wake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.