Nikimjua aliyesababisha na kutoa amri ya kupigwa viboko nakufa nae

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,944
3,820
Yaani siombi ije kutokea ,lakini ikiwa kiongozi yeyote yule halafu nimjua kuwa yeye ndio ametoa amri ya nichapwe viboko hadharani,nakufa nae hadharani na ulimwengu utasikia ,huu udhalilishaji umepitwa na wakati.

Kwa kuwa tu umekuwa na cheo sasa unathubutu kuchapa watu bakora,kama ni kujitoa muhanga basi nitajitoa tu,maisha ya kuchapana viboko kwenye nchi huru tena bila ya kufuata sheria.mtu anaamua tu ,mcharazwe viboko.

Kuna askari kakamatwa na viroba,bangi,gongo ,anakwiba umeme,nimevuta hisia hawa watu wanaochapa watu viboko kwanini wasisachiwe kama alivyofanyiwa polis na kukutikana na hati,wachapa viboko hawa itakuwa hawana tofauti na huyo askari kwa maana wanahifadhi bangi,gongo na viroba na wanapotoa amri za kuwachapa watu viboko hadharani kabla ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria basi itakuwa wameshavuta bangi na kunywa kangara.

Tufuateni sheria,mahakama zipo mambo ya kukamatana na kutuchapa viboko hadharani, tutakuja kuuwana mchana kweupe at the close range.

hayo mambo walifanyiwa mababu zetu na mkoloni na waliyapinga hadi kupata au kuwa huru.
Naikumbuka filamu ya Kunta Kinte.
 
hata mimi anaweza kunichapa nikiwa mahututi labda. si vinginevyo
na akifanikiwa lazima nilipe kisasi, tena kwake mwenyewe
 
Hivi hao askari hawajapelekwa lokapu au hawajapewa hata kesi ya uhujumu uchumi ?
 
Back
Top Bottom