Shairi: Nikile chakula kipi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Habari zenu watani, mabibi nanyi mabwana,
Miye nawasalimuni, kindugu siyo kitwana,
Na beti zangu someni, ni hizi za kiungwana,
Nina vyakula viwili, nichague kipi kwanza?

Ninayo njaa mwenzenu, na tumbo linanguruma,
Sasa nimepewa menu, si ya wali wala sima,
Si vya kula vya kikwenu, vya kigeni natazama,
Nina vyakula viwili, nichague kipi kwanza?

Cha moto hicho cha kwanza, meza imeandaliwa,
Harufu inapendeza, Hanifa kakipakuwa,
sasa nataka kuanza, msosi kuuchukuwa,
Nina vyakula viwili nichague kipi kwanza?

Lakini hicho cha moto, kinahitaji subira,
Hakimfai mtoto, wala kula kwa papara,
Nangojea kama loto, nisikile kwa hasira,
Nina vyakula viwili nichague kipi kwanza?

Kingine ni cha baridi, kimeandikwa mezani,
Mdomoni chakaidi, hakiingii kinywani,
Amenipa Mwanaidi, ati nikile jamani,
Nina vyakula viwili, nichague kipi kwanza?

Kasema ati kitamu, nikikila cha baridi,
Nitajilamba kwa hamu, kama ni siku ya Idi,
Kakipika kitaalamu, hivyo nisije kaidi,
Nina vyakula viwili, nichague kipi kwanza?

Mwenzenu sasa natingwa, midomo naumauma,
Naona sasa nategwa, ninayo hamu ya nyama,
Ninajiona mfungwa, wa njaa inayouma,
NIna vyakula viwili, nichague kipi kwanza?

Kalamu naweka chini, kichwa changu najikuna,
Kosa langu mimi nini, nachombezwa kiana,
Viwili vyote vya nini, ubaya twatafutana,
Nina vyakula viwili, nichague kipi kwanza?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
 
Mwanakijiji wa shamba, naona sasa washindwa,
tadhihirisha ushamba, tumbo baridi kuvimbwa,
wenzio watajiramba, vya moto ulivyoshindwa,
mlo ulo moto, shusha kwa maji baridi
 
Ewe sauti ya shamba ,pokea yako salamu,
uwanjani natinga, si kwa shari ila shwari,
naona wazidi tingwa, midomo waumauma,
kati ya viwili,chamoto chagua kwanza,

Raha jipe mwenyewe, Na usisubiri kupewa,
kiama kitakukuta,ukisubiri kupewa raha,
elimimika ewe washamba, mjini sasa umeingia,
kati ya viwili,chamoto chagua kwanza,

Yamwanaidi mpe iddi,washamba huyawezi kamwe,
ujanja wake nimebaini,maradhi kukupatia,
waumwa hoi kitandani,yeye afurahia kwaiddi,
kati ya viwili,chamoto chagua kwanza,

Mama nakupenda sana,duniani umeniweka,
maneno yako sawia,matamu kuliko asali,
togwa kazoea sana,majibaridi ayajua wapi?
kati ya viwili,chamoto chagua kwanza,

Tamati namaliza,jf hapakaliki,
watu wote wanasinzia,chabaridi wamevimbiwa,
maneno yangu yakweli, washamba nawe sikia,
kati ya viwili,chamoto chagua kwanza,

Msinipake jamani,nikosoeni kwa upole,
mwenzenu najaribu,nahitaji sapoti yenu,
vina na mizani sijui,wala mpangilio sijui,
kati ya viwili,chamoto chagua kwanza,
 
Wa kijiji pokea salam, Ukumbini naingia,
Ushauri kuja kukupa, kati ya hivyo viwili,
Lazima uwe mjanja, Na hawa wa mjini,
Chamoto chagua kwanza, Upate ladha halisi,

Watakuona mshamba, Ukichagua cha mwanaidi,
Kwani Wao walishaonja, wakaona hakifai,
Wamekaa kama mafisi, chamoto wakitamani,
Chamoto chagua kwanza, Upate ladha halisi,
 
Mwanakijiji wa shamba, naona sasa washindwa,
tadhihirisha ushamba, tumbo baridi kuvimbwa,
wenzio watajiramba, vya moto ulivyoshindwa,
mlo ulo moto, shusha kwa maji baridi

heeee????umesahau au..
 
Wa kijiji pokea salam, Ukumbini naingia,
Ushauri kuja kukupa, kati ya hivyo viwili,
Lazima uwe mjanja, Na hawa wa mjini,
Chamoto chagua kwanza, Upate ladha halisi,

Watakuona mshamba, Ukichagua cha mwanaidi,
Kwani Wao walishaonja, wakaona hakifai,
Wamekaa kama mafisi, chamoto wakitamani,
Chamoto chagua kwanza, Upate ladha halisi,

A kale dhidi ya kisasa.anyway..linaimbika
 
Hata kikiniunguza, cha moto nikile kwanza?
Nani ataniuguza, pale nitakapolazwa,
Naona mwanichuuza, naona kama nachezwa,
Cha moto nikile kwanza, hata kikiniunguza?
 
Hata kikiniunguza, cha moto nikile kwanza?
Nani ataniuguza, pale nitakapolazwa,
Naona mwanichuuza, naona kama nachezwa,
Cha moto nikile kwanza, hata kikiniunguza?

Usanii huja acha,hauachi kujiramba.
Kula umeshakula,vyote raza waijua.
Cha moto umeonja,cha baridi pia.
Vinono ume-jilia,kijiweni wa-tulingishia.
 
Hata kikiniunguza, cha moto nikile kwanza?
Nani ataniuguza, pale nitakapolazwa,
Naona mwanichuuza, naona kama nachezwa,
Cha moto nikile kwanza, hata kikiniunguza?

Mzee mwanakijiji, mlo moto ujilie
kiso ladha wakihoji, hata jasho sikutoe
cha moto homa ya jiji, cha baridi kikimbie
Kula mlo ulo moto, shushia maji baridi
 
Mzee Mwanakijiji, wamjini wankuchuuza,
Chamoto sihitaji, kijijini kwaida nakandamiza,
mjini kuna mafriji, majokofu mengi kupooza,
siwe mshamba wamji, vamoto kula kupuliza,
wamjini wanakuchuuza, jifaidie vya barafu. (kijijini hakuna)

nimejaribu kwa mara ya kwanza leo shairi.
 
kama anavyotaka majita 8*8, nimesahau jinsi inavyoitwa kiushairi. Kwa mfano:

Cha moto sikihitaji, kijijini nakandamiza
mjini kuna friji, majokofu ya kupoza
etc

hongera sana MQ.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom